Habari kutoka 14 Disemba 2011
Zambia: Magari Mapya ya Kifahari ya Mtoto wa Rais Yasababisha Minong’ono
Taarifa zilizotangazwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Asasi ya Kiraia ya Committee of Citizens, Gregory Chifire, kwamba mtoto wa kiume wa rais wa Zambia, Mulenga Sata, hivi karibuni alijipatia magari mawili ya kifahari, zimevutia hisia mchanganyiko kutoka kwa wa-Zambia watumiao mtandao
Kongo (DRC): Wakongo Waishio Nje ya Nchi Walipuka Kumpinga Kabila
Wakati Kongo (DRC) ikingoja matokeo ya mwisho ya kura za Urais na wabunge, wa-Kongo waishio nje ya nchi hiyo, ingawa hawakuruhusiwa kupiga kura, wameonyesha kujitolea kwako kwa kuzifanya sauti zao zisikike. Julie Owono anataarifu.
Tanzania: Zinavyosema Blogu na Twita Katika Sherehe za Miaka 50 ya Uhuru wa Tanzania
Desemba 9, 2011, ni siku maalumu kwa Watanzania wakati Tanganyika, ambayo ni sehemu ya Muungano wa Tanzania ikitimiza miaka 50 ya uhuru. Katika mtandao, wanablogu na watumiaji wa twita wanasherehekea na kutafakari kwa kina mustakabali wa Tanzania.
Madagaska: Wajadili Uhalali wa Uwekezaji wa Kigeni wa Moja kwa Moja
Wakati Madagaska ikijaribu kutafuta suluhisho la matatizo ya muda mrefu ya kiasa, Wanablogu wa ki-Malagasi wanajadili thamani ya Uwekezaji unaofanywa Moja kwa Moja na raia wa Kigeni. Wa-Malagarasi wanaamini kwamba Madagaska, kama nchi nyingine za Kiafrika inao utajiri mkubwa wa rasili mali lakini tatizo likiwa ardhi yenyewe kupokonywa kwa sababu ya utawala mbovu na biashara zisizoangalia maslahi ya wananchi.