Kongo (DRC): Wakongo Waishio Nje ya Nchi Walipuka Kumpinga Kabila

Ingawa jumuiya ya raia wa Kongo (DRC) waishio ng’ambo hawakupewa haki yao ya msingi ya kupiga kura [fr] wakati wa uchaguzi wa Rais na wabunge uliofanyika Novemba 28, 2011, raia hao wameonyesha kujitolea kwao kwa kujihusisha na majadiliano ya kisiasa.

Kwa kutumia chaneli kadhaa za mtandoni, raia hao wa Kongo waiishio nje ya nchi yao wameunda majukwaa mbalimbali ya kukuza uelewa miongoni mwa raia wenzao pamoja na wanachama wa jumuiya yao kimataifa. Kwa hakika, raia hao wamefanikiwa kufanya sauti yao isikike.

Mnamo Desemba 7, Mabalozi wa Ufaransa, Uingereza na Ubeligiji walio jijini Kinshasa walimshinikiza [fr] kiongozi wa muda mrefu wa upinzani na aliyekuwa mgombea wa kiti cha urais Etienne Tshisekedi kuwasihi wafuasi wake kuacha ghasia katika miji mbalimbali nje ya nchi hiyo. Tshisekedi alishika nafasi ya pili katika uchaguzi huo kwa mujibu wa matokeo ya awali yaliyotangazwa na Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (CENI).

Kwa mujibu wa Nicolas-Patience Basabose, Mkurugenzi wa Chapisho la Le Congo Hebdo [fr] (Congo Weeklu), anayeishi Afrika Kusini, raia hao waishio nje ya nchi bado wana uhusiano imara na wenzao waishio nyumbani [fr]:

Les Congolais de l’étranger ont un rôle très politique à jouer car la plupart ne sont pas partis pour découvrir le monde en soit mais poussés par des conditions sociopolitiques pas très favorable. Les expats sont très connectés avec le pays surtout durant les 10 ans meurtrières de Kabila. Manifester et faire du bruit était sûrement la seule et unique chose que la diaspora pouvait faire pour faire peser leurs voix dans le processus électoral en court.

Wakongo waishio nje ya nchi wanayo nafasi muhimu sana ya kisiasa kwa sababu wengi wao hawakuondoka nchi mwao kwenda tu kuifahamu dunia, lakini walilazimishwa na mazingira yasiyopendeza ya kijamii na kisiasa nchini mwao. Wamekuwa wajihusisha kwa karibu sana na yanayoendelea nchini mwao, hasa wakati wa miaka kumi ya machungu katika kipindi cha [Rais] Kabila. Kuandamana na kupiga kelele pengine ilikuwa ni namna pekee waliyokuwa nayo ya kufanya sauti zao zisikike katika mchakato wa uchaguzi wa hivi karibuni.

Nchini Ufaransa, Ubalozi wa Congo (DRC) jijini Paris ulijaa waandamanaji wanaompinga Kabila wakisema walikuwa wanairejesha tena mikononi mwao mipaka ya nchi yao, na wakidai kwamba Tshisekedi alikuwa mshindi wa kweli wa uchaguzi huo. Waandamanaji hao walitumia mbinu ya kuvipotezea malengo vikosi vya usalama vya Ufaransa vilivyokuwa vinalinda jengo hilo, na walifika mahali hapo wakiwa kwenye gari kubwa la mizigo.
RPBIjou aliweka kwenye YouTube picha zifuatazo Desemba 5:

Maandamano yenye vurugu yalifanyika karibu na makao makuu ya Umoja wa Ulaya mjini Brussels, Ubeligiji (nchi ambayo iliwahi kuitawala Kongo (DRC) kama koloni lake) Tarehe 7 Desemba, mtumiaji wa You Tube aitwaye The Voice of Congo aliweka video ya raia wa Kongo wakiandamana Desemba 5, kwenye mitaa ya Brussels wakielekea kwenye jengo la Ubalozi wa Kongo DRC.

Wavuti ya Habari za nchi zinazozungumza kifaransa ya ki-Belgiji Lseoir.be [fr] iliripoti kwamba maandamano yaligeuka kuwa vurugu na baadhi ya waandamanaji waliwekwa chini ya ulinzi baada ya kuwarushia mawe maafisa wa polisi na kusababisha uharibifu wa maduka na miundo mbinu ya umma.

Maandamano mengine yaliandaliwa jijini London, (taarifa ya BBC) na nchini Italia.

Raia hao wa Kongo pia wana wajibu muhimu wa kiuchumi katika mustakabali wa nchi yao. Kwa mujibu wa utafiti wa kitaaluma [fr], uliofadhiliwa na Tume ya Ulaya na Wizara ya Maendeleo ya Ubeligiji, wa-Kongo wapatao 40,300 wanaoishi kwa mujibu wa sheria nchini Ubeligiji wanatuma wastani wa Dola za Kimarekani 130,000,000,00 kwa jamaa zao wanaoishi Kongo RDC. Kuna uwezekano mkubwa kwamba katika nchi hii, ambayo wastani wa pato la taifa ni Dola la kimarekani Bilioni 11, wananchi hao wanaoishi ng’ambo wanachangia sehemu muhimu ya utajiri wa taifa.

Maandamano ya wa-Kongo jijini London. Picha ya new chap kwenye Flickr (CC BY-NC-SA 2.0)

Kwa kuandamana katika miji mikuu nje ya nchi yao, wa-Kongo hao pia wanataka kupinga vikali mamlaka fulani za Kimagharibi na makampuni yao ya madini. Hapa kuna video iliyowekwa kwenye You Tube ambapo mmoja wa wa-Kongo waishio Alberta, Canada anayatuhumu makampuni ya Kanada kuwa yanayofanya kazi zao kinyume na sheria nchini Kongo:

Tunawapinga, tunawalaumu na kuwalalamikia hawa maafisa kwa kumwunga mkono na kujihusisha na serikali ya Joseph Kabila ambayo wa-Kongo wameikataa kwenye uchaguzi wa Novemba 28. Hawa watu ni wahalifu wanaoishi Kongo na ni wahalifu wanaoishi Kanada na ni wahalifu wa sheria za kimataifa. (…) Tunazo taarifa kutoka kwenye vyanzo vya uhakika kuhusiana na majina ya watu maarufu wa ki-Kanada ambao makampuni yao yanajihusisha na unyonyaji haramu wanaoufanya kwenye madini yetu nchini Kongo.

Siku moja baada ya tamko hili kutolewa hadharani, maandamano yalifanyika jijini Ottawa, mji mkuu wa Kanada. Kwa mujibu wa PeterRW aliyeweka video kwenye You Tube, “Kile kilichoanza kama maandamano ya amani…kimegeuka kuwa ghasia kwa sababu waandamanaji wameanza kurusha mawe na kuandika maandishi kwenye kuta za ubalozi wa Kongo”

Jijini Johannesburg hali kadhalika palishuhudiwa maandamano ya mamia ya raia wa ki-Kongo. Kati yao alikuwepo mmoja aliyekuwa uchi, aliyekuwa akipiga kelele “Kabila lazima aondoke”, na kumwomba Rais Zuma, ambaye anamwunga mkono rais anayemaliza muda wake, kuondoka Kongo. The voice of Kongo aliweka video hii:

Maandamano mengine yalitokea Afrika, hususani nchini Morocco.

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.