6 Novemba 2009

Habari kutoka 6 Novemba 2009

Irani: Vuguvugu la Kijani Laupinga Utawala Tena

Upande wa upinzani wa Vuguvugu la Kijani nchini Irani mnamo tarehe 4 Novemba uliendesha maandamano makubwa ambapo maandamano hayo yalikabiliwa na matumizi makubwa ya nguvu ya kuyazuia yaliyofanywa na vikosi vya usalma. Kama ambavyo sasa inatarajiwa, uandishi wa habari wa kiraia nchini Irani haukukosa kitu kwani ulirekodi 'historia' hiyo kupitia simu zao za mikononi.

Amerika ya Kati: Kasi Kubwa ya Ueneaji wa Jangwa

  6 Novemba 2009

Ueneaji wa jangwa unasambaa kimyakimya lakini kwa kasi kubwa mahali pengi duniani na Amerika ya Kati haijaweza kukwepa hali hii iliyo na athari mbaya za kutisha. Wakati ambapo majangwa ni maumbo ya asili, ueneaji wa jangwa ni mchakato wa kuharibika kwa nyanda za ardhi kutokana na mabadiliko ya hali ya hewa na uharibifu unaofanywa na binadamu.

Kutambulisha Sauti Zinazotishwa

  6 Novemba 2009

Leo, kitengo cha utetezi cha Global Voices, kinazindua tovuti mpya inayoitwa Threatened Voices, yaani, Sauti Zinazotishwa ili kusaidia kufuatilia unyamazishaji wa uhuru wa kujieleza wa mtandaoni. Inaonyesha ramani ya dunia na mwingiliano wa saa unaosaidia kuonyesha taarifa za vitisho na ukamataji unaofanywa dhidi ya wanablogu duniani kote, na ni mhimili mkuu wa kukusanyia taarifa kutoka katika asasi na wanaharakati walioamua kujitoa muhanga kwelikweli.

Tamasha la Blogu Indonesia

  6 Novemba 2009

Tulitembelea tamasha la blogu la Indonesia au PestaBlogger 2009. Hii nim ara ya tatu kwa tukio hili la mwaka kufanyika. Tukio hili lilishuhudia wanablogu kutoka kila sehemu ya Kisiwa hiki ambacho pia ni Taifa wakimiminika mjini Jakarta ili kusherehekea, kujadili na kujumuika.