Tamasha la Blogu Indonesia

Indonesia ina uwanja wa blogu uliosisimka na wenye msisitizo mkubwa kwa jamii. Tamasha la mwaka la wanablogu (Pestablogger) la Indonesia liliwavutia wanablogu na wapenzi wa teknolojia kutoka sehemu zote za taifa.

Ukumbi uliojaa wa tamasha la blogu la Indonesia


Taswira kutoka kwenye tamasha la blogu.


Hii ilikuwa ni mara ya tatu kwa tukio hili la mwaka kufanyika na ni vizuri kuona idadi ya washiriki inaongezeka kila mwaka.

pestablogger09

pestablogger09


Kipindi cha majadiliano juu ya maadili ya kublogu

Kipindi cha majadiliano juu ya uanahabari wa kiraia

Mwanahabari wa kiraia akielezea uzoefu wake kwa wanablogu

Kipindi cha majadiliano juu ya kuunganisha kwenye utengano ndani ya Indonesia kwa kutumia blogu. Washiriki pia walijadili njia ambazo Indonesia inaweza kutumia kuiunganisha na dunia ya nje.

Tristam (aliyewakilisha shirika la wadhamini), Chip, (mkereketwa wa teknolojia kutoka Vietnam) na Retty (Mwanablogu wa Indonesia) wakiwa katika majadiliano. Tukio hili la Indonesia halikushuhudia viwango vya ushiriki kutoka nje ambavyo Kampuchea au Thailand huvishuhudia. Hata hivyo, watu waliojaa udadisi wanatiririka na tunatumaini kupata watu zaidi kutoka maeneo ya Kusini Mashariki ya Asia wakati ujao.

Msanii wa Batik akitengeneza shati la tamasha la blogu

Wanablogu wanachukua mapumziko kutoka kwenye majadiliano na kuburudika na muziki.

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.