Irani: Vuguvugu la Kijani Laupinga Utawala Tena


Upande wa upinzani wa Vuguvugu la Kijani nchini Irani mnamo tarehe 4 Novemba mwaka huu (13 ya Abani) uliendesha maandamano makubwa ya mitaani, baada ya kutumia fursa ya maandamano rasmi yaliyoendeshwa siku hiyo ya kuadhimisha kumbukumbu ya miaka 30 ya ukaliaji wa Ubalozi wa Marekani jijini Teherani. Maandamano hayo ya upinzani yalikabiliwa na matumizi ya nguvu kupita kiasi ya kuyavunja yaliyofanywa na vikosi vya usalama.

Kama ambavyo sasa imekuwa jambo la kutarajiwa, vyombo vya habari vya kiraia vya Irani vilirekodi ‘historia’ hiyo kupitia simu zao za mkononi.

Waandamanaji jijini Teherani walikanyagakanyaga picha ya Kiongozi Mkuu wa Kidini nchini humo, Ayatollah Ali Khamenei, kitendo ambacho wala kisingefikiriwa miezi michache tu iliyopita.

Ujumbe kwa Obama: Ama uko upande wetu au uko upande wao.

Kiongozi wa upinzani, Mehdi Karoubi, akiwa katikati ya watu.

Vikosi vya Usalama vikishambulia waandamanaji.

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.