Habari kuhusu Haki za Binadamu
Wanawake Wanaongoza Maandamano Nchini Sudan
“Wanawake wako mbele, kushoto, na katikati mwa mapinduzi. Maandamano yalipoanza, watu walidai, "Wanawake wangebaki nyumbani.' Lakini sisi tulisema — hapana.”
Je, Felix Tshisekedi Atamaliza Machafuko Katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo?
President Felix Tshisekedi alisema kwamba hatua ya mahakama kuthibitisha ushindi wake ilikuwa ni ushindi kwa nchi yote na aliahidi kujenga taifa la umoja, amani na usalama.
Wanaharakati Watafuta Majibu, Mwezi Mmoja Baada ya Uchunguzi wa Kifo cha Aliyekuwa Mwandishi wa Habari.
Divela aliiambia asasi ya kuwalinda Waandishi (Committee to Protect Journalists) kupitia ujumbe wa WhatsApp kwamba "vigogo nchini Ghana walikuwa wanatafuta namna ya kumdhuru"
Wakati Putin Akihubiri “Uhuru” na Maendeleo ya Teknolojia, Wataalamu Walalamikia Kupotea kwa Uhuru Mtandaoni
Wakati Vladimir Putin akiwaahidi Warusi mtandao wenye kasi zaidi na wa kuaminika, taarifa mbili za makundi ya wataalamu wa kujitegemea waonesha kuzorota sana kwa uhuru wa kutoa maoni mtandaoni.
Mwanaharakati Raia wa Singapore Ahukumiwa Kifungo cha Siku 16 Jela kwa Kuzungumza na Joshua Wong Kiongozi wa Vijana wa HK
"Hakuna hukumu ambayo ningeweza kuichukulia kama ya haki, kwa sababu hakukuwa na kufunguliwa mashtaka kabisa."
Kijana wa Niger Akwama Uwanja wa Ndege nchini Ethiopia kwa Miezi Kadhaa
"Nimelala kwenye viti, wakati mwingine nimelala msikitini, sijaoga kwa miezi miwili sasa kwa sababu uwanja wa ndege hauna bafu."
Jumuiya ya Mashoga Nchini Guyana Yaandaa Maandano ya Kwanza Kujivunia Ushoga
"#Guyana imebaki kuwa nchi ya pekee barani Amerika Kusini ambako ushoga bado ni kinyume cha sheria. Nchini humo, pamefanyika maandamano ya kwanza ya kujivunia ushoga. Huenda hiyo ni hatua ya kuelekea kuuhalalisha ushoga..."
Polisi wa Nigeria Wamkamata Mwandishi wa Habari na Kaka Yake kwa Makala ya Gazeti Ambayo Hata Hivyo Hawakuiandika
"Polisi hawana mamlaka ya kuvamia nyumba za waandishi wa habari na kuwafungia kwa sababu tu kuna afisa wa serikali hapendi kile kilichoandikwa kwenye gazeti."
Namna Utoaji Bure wa Kifungua Kinywa Nchini Yemen Ulivyorudisha Wasichana 500 Shuleni
Kabla ya mradi kuanza, moja ya tano ya wanafunzi walikuwa wahahudhurii. Sasa, wote wamerudi darasani.
Mamlaka za Iran Zawakamata ‘Watumiaji wa Instagram’ katika harakati za Kudhibiti Mitandao ya Kijamii
Mamlaka ya Irani yatangaza kuondoa Instagram kwa sababu ya maovu ya "watumiaji mashuhuri wa Instagram". Siku chache baadaye, shirika la utangazaji la serikali afichua kukamatwa kwa "watumiaji mashuhuri wa Instagram."