Habari kuhusu Haki za Binadamu kutoka Disemba, 2012
Mwandishi wa Guinea Atoweka Kiajabu nchini Angola
Yuko wapi Milocas Pereira? Swali hili linarudiwa rudiwa kupitia blogu mbalimbali kwa majuma kadhaa sasa, lakini majibu yamekuwa vigumu kupatikana. Katika mitandao ya kijamii harakati zililipuka kuzishinikiza mamlaka za nchi ya Guinea kuchunguza mazingira ya kupotea kwa mwandishi huyo na mhadhiri wa Chuo Kikuu miezi sita liyopita katika jiji la Luanda, alikokuwa akiishi tangu mwaka 2004.
Kitabu-pepe Kipya cha GV: Sauti ya Kiafrika ya Matumaini na Mabadiliko
"Sauti ya Kiafrika ya Matumaini na Mabadiliko", kinakupa mtazamano wa kipekee kuhusu watu na habari za eneo la Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara kupitia posti zetu zilizo bora zilizoandikwa kwa lugha ya Kiingereza kwa mwaka 2012. Hii ni zawadi sahihi kabisa ya kuukaribisha mwaka mpya.
Video ya Kuomba Ujenzi wa Vyoo vya Umma huko Jharkhand, India
Amit Topno, mwakilishi wa jumuiya ya hiari “inayopiga picha za video” aliripoti kwamba wakati wa kijiji cha Nichitpur katika Jimbo la Jharkhand hawana choo chochote cha umma kinachotumika. Wanavijiji wanaziomba...
Walimu wa Mauritania Wavunja Ofisi ya Waziri wa Elimu
Kundi la walimu wa sekondari lilivunja na kuingia kwenye ofisi ya Waziri wa Elimu katika maandamano ya kipinga kuhamishwa kiholela kwa walimu wapatao 120 baada ya kushiriki kwao mgomo uliofanyika mwaka jana.
Utambulisho wa Jamii ndogo ya Balkan
Waandishi vijana kumi na watano kutoka katika nchi zipatazo sita tofauti wametengeneza mfululizo wa masimulizi binafsi kuhusu masuala ya namna jamii zenye watu wachache (kwa mapana yake) zinavyoweza kuwakilishwa kutoka...