· Mei, 2013

Habari kuhusu Haki za Binadamu kutoka Mei, 2013

Maelfu ya Wafanyakazi Waandamana Barani Asia

  4 Mei 2013

Global Voices inayapitia kwa haraka maandamano ya Siku ya Wafanyakazi Mei Mosi kwenye nchi za Cambodia, Filipino, Indonesia na Singapore. Mikutano, ambayo iliandaliwa kudai haki za wafanyakazi na makundi mengine ya utetezi, yalifanyika kwa amani katika bara lote la Asia ya Kusini Mshariki.

Ethiopia: Mwanablogu Ahukumiwa Miaka 18 Jela kwa “Kuvunja Katiba”

GV Utetezi  4 Mei 2013

Mnamo Mei 1, Mahakama Kuu ya Ethiopia ilitoa hukumu kali kwa mwandishi aliyeshinda tuzo Eskinder Nega, ambaye sasa atatumikia kifungo cha miaka 18 jela. Mohamed Keita wa Kamati ya Kuwalinda Waandishi anasema, “Kushitakiwa na hatimaye kutiwa hatiani kwa Eskinder na waandishi wengine ni dalili za utawala unaoogopa maoni ya raia wake.”