Habari kuhusu Haki za Binadamu kutoka Disemba, 2009
Uganda: Rais Kuzuia Muswada Unaopinga Ushoga
Muswada Unaopinga Ushoga wa 2009 uliopendekezwa nchini Uganda bado unasubiri uamuzi wa mwisho utakaotolewa na bunge la nchi hiyo, lakini gazeti la Daily Monitor lilitaarifu Jumatano kuwa Rais Yoweri Museveni ameihakikishia Idara ya Mambo ya Nje ya Marekani nia yake ya kuukwamisha muswada huo
Palestina/Gaza: Matayarisho ya Maandamano ya Uhuru Gaza
Ni kama wiki moja hivi mpaka Maandamano ya Uhuru Gaza yatakapoanza. Lengo lake ni kuonyesha mshikamano na Wapalestina na kuongeza ufahamu kuhusu vikwazo vinavyoizingira Gaza. Katharine Ganly anatazama baadhi ya matukio yaliyotokea katika maandalizi ya maandamano hayo.
Singapore: Kampeni ya “Kataa Ubakaji”
Nchini Singapore, mara nyingi kumbaka mke wako hakuchukuliwi kama tendo la kubaka. Waandaji wa kampeni ya “Kataa Ubakaji” wanataka kukomesha sheria inayokinga ubakaji ndani ya ndoa kwa kuzindua kampeni ya kukusanya saini ambazo zitawasilishwa kwa watunga sera. Wengi wa raia wa mtandaoni wanaiunga mkono kampeni hii.
Morocco: Mwanablogu Mwingine Atupwa Gerezani
Mnamo tarehe 14 Desemba, siku ya Jumatatu, mwanablogu Bashir Hazzam na mmiliki wa mgahawa wa Intaneti Abdullah Boukhou walihukumiwa kifungo cha miezi minne jela kwa huyo wa kwanza na mwaka mmoja kwa huyo wa pili pamoja na kulipa faini ya MAD 500 (sawa na dola za Marekani 63) kila mmoja katika mahakama ya Goulmim.
Misri: Makao Makuu ya Kuzimu Duniani
Wanablogu na wanaharakati wengi wa Kimisri wamekuwa wakikamatwa na Usalama wa Taifa katika nyakati tafauti kwa sababu mbalimbali –za kweli au za bandia –Wa7da Masreya aliwahoji wanablogu mbalimbali na kuweka makala ya kina kuhusu mbinu za utesaji na hila za kisaikolojia ambazo wanablogu wale wamekuwa wakikumbana nazo kwenye makao makuu ya Usalama wa Taifa katika wilaya ya Jiji la Nasr.
Iran: Maandano ya Siku ya Mwanafunzi kwenye YouTube
Maelfu ya waandamanaji hawakuujali utawala wa Kiislamu leo kwa kuandamana wakati wa siku ya mwanafunzi, wakiimba kaulimbiu dhidi ya Ali Khamenei, kiongozi wa Jamuhuri ya Kiislamu, na wakipinga sera ya mambo ya nje ya serikali.
China: Uvunjaji Nyumba kwa Kutumia Mabavu
Visa viwili vya uvunjaji nyumba kwa mabavu vimeibua hisia za kutaka kulindwa zaidi kwa haki za raia na utatuzi wa migogoro nchini Uchina. Watumiaji wa mtandao wa Kichina wanatoa maoni.
Warsha ya Wanablogu wa Uarabuni: Tafakuri ya Twita kwa Siku ya Kwanza
Wakati siku ya kwanza ya Warsha ya Pili ya Mwaka ya Wanablogu wa Uarabuni ikifungwa, tutaangalia tafakuri za washiriki kwa siku nzima, kujua wamejifunza nini na namna wanavyojisikia. Siku ilianza...
Indonesia: Sarafu za Kudai Haki
Raia wa mtandaoni (Netizens) wamezindua kampeni ya kukusanya fedha zilizo katika muundo wa sarafu ili kumuunga mkono Prita Mulyasari, mama wa nyumbani raia wa Indonesia aliyeandika malalamiko yake mtandaoni dhidi ya hospitali iliyotoa huduma mbaya, na ambaye alipatikana na hatia na mahakama moja ya kosa la "kuchafua jina" la hospitali hiyo binafsi.
Guatemala: Kuvunja Milango ya Madanguro
Blogu inayojulikana kama Noticias para Dios inatoa habari za ndani, kama vile mambo yenyewe yanavyotokea pasipo kuficha kitu, kuhusu maisha ya kila siku ya mwanasheria wa Ki-Guatemala anayejaribu kuwaokoa watoto kutoka kwenye madanguro ambako wamekuwa wakiishi baada ya kuchukuliwa kutoka makwao.