Warsha ya Wanablogu wa Uarabuni: Tafakuri ya Twita kwa Siku ya Kwanza

Wakati siku ya kwanza ya Warsha ya Pili ya Mwaka ya Wanablogu wa Uarabuni ikifungwa, tutaangalia tafakuri za washiriki kwa siku nzima, kujua wamejifunza nini na namna wanavyojisikia.

Siku ilianza kwa kishindo, wakati waandaaji wa Global Voices Sami ben Gharbia, Amira Al Hussaini, na wafadhili wetu kutoka Mfuko wa Heinrich Böll waliwakaribisha washiriki kutoka kote Uarabuni na nje ya mipaka. Kufuatia utambulisho, watoa mada Noha Atef wa idara ya Utetezi ya Global Voices na Eman Abdulrahman wa Global Voices (na mwanzilishi wa Koleana Laila) walishirikisha dondoo na mawazo kuhusu namna ya kutengeneza kampeni bora mtandaoni. Mshiriki wa Kimauritania weddady aliandika kuwa Kolana Laila inatafuta kujenga ushirikiano kote Uarabuni katika twita yake:

Unaweza kupata habari zaidi kupitia kolenalaila.com

Unaweza kupata habari zaidi kupitia kolenalaila.com

Siku nzima, kulikuwa na warsha mahsusi, kuhusu kila kitu kuanzia namna ya kukabiliana na ugumu na kuficha jina (mada iliyotolewa na Jacob Applebaum) mpka uanahabari wa kiraia (mada iliyotolewa na Amira Al Hussaini na Salam Pax) njia za kuhifadhi video mbadala wa YouTube (ilitolewa na Slim Amamou na Marcin Gajewski). Kwa hili la pili, Lina ben Mhenni alikuwa na maoni haya:

Njia mbadala ya YouTube

Njia mbadala ya YouTube

Hata hivyo, mada iliyowafanya washiriki washikwe na hasira, ilikuwa ni ile iliyotolewa na mshiriki wa ki-Syria Razan Ghazzawi juu ya tafiti inayotengeneza ramani ya ulimwengu wa blogu wa Kiarabu iliyofanywa na Kituo cha Berkman kwa Ajili ya Intaneti na Jamii. Ingawa kulitokea mjadala mkali (ambao unaweza kupatikana kwa kutafuta kwenye alama #ab09 kwenye Twita), hapa kuna dondoo kidogo: mshiriki wa Misri lastoadri alishangaa kwenye Twita ikiwa washiriki walikuwa wamefahamishwa kikamilifu kuhusu utafiti huo:

lastoadri akijiuliza kwa sauti

lastoadri akijiuliza kwa sauti

Nasser Weddady aliona mantinki muhimu iliyoletwa na Razan:

weddady amnukuu Razan Ghazzawi

weddady amnukuu Razan Ghazzawi

Mwisho, Muiraki Salam Pax alikubaliana na Razan katika suala hilo, akisema:

Salam Pax akikubaliana na mtoa mada kwa kuandika:

Salam Pax akikubaliana na mtoa mada

Salam Pax akikubaliana na mtoa mada

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.