Indonesia: Sarafu za Kudai Haki

Mapema leo, Prita Mulyasari, mama wa nyumbani aliyeshtakiwa kwa kuandika barua pepe ya kulalamikia huduma mbaya iliyotolewa na hospitali, alipatikana na hatia ya kuchafua jina la hospitali hiyo ya binafsi na Mahakama Kuu ya Tangerang. Mahakama hiyo ilimwamuru kulipa faini ya Rupia milioni 204 (sawasawa na dola za Marekani 21,680) kwa hospitali hiyo inayojulikana kwa jina la OMNI International Alam Sutera.

Mshahara wa mfanyakazi wa kiwandani katika jiji la Jakarta ni kiasi cha dola za Marekani 106 kwa mwezi.

Watumiaji wa mtandao nchini Indonesia wanafanya harakati kukusanya kiasi hicho katika muundo wa sarafu kwa sababu wamekasirishwa sana na uamuzi wa mahakama na wanatumaini kwamba sarafu zitaielemea hospitali hiyo, alieleza mwanaharakati mmoja kupitia gazeti moja linalochapishwa nchini humo linalojulikana kama Kompas.

“Pale haki inapokiukwa, tunakusanya sarafu”, anasema kauli mbiu ya Koin Keadilan, Sarafu kwa ajili ya Haki, ambayo ni tovuti mpya iliyojikita katika kukusanya sarafu hizo ili kulipa faini aliyotozwa Prita.

Picha iliyoko kwenye www.koinkeadilan.com

Picha iliyoko kwenye www.koinkeadilan.com

Tangazo la mtandaoni lililowekwa kwenye tovuti linasema:

Tentang cara, kita bisa dan boleh berbeda pendapat. Misalnya tentang perlu atau tak perlu dalam pengumpulan koin. Yang pasti kita sama-sama di posisi ini: rasa keadilan kita terlukai. Spirit kita pun sama, bahwa keangkuhan kekuasaan yang ingin mengenyahkan kebebasan berpendapat melalui kriminalisasi harus kita lawan.

Tunaweza kutofautiana kuhusu njia. Kama ni lazima kutoa michango hiyo katika muundo wa sarafu au hapana. Lakini tunakubaliana jambo moja: haki inakandamizwa. Tuna hisia moja, kwamba madaraka na kiburi ambavyo vinataka kufutilia mbali uhuru wa kujieleza kwa kuugeuza kuwa jinai, havina budi kupigwa vita.

Kelele hizo za kupinga na twiti za mshikamano zinatumwa kupitia #freeprita na #helpprita.

AdibHidayat: Rencana acara akan dibuat di Hard Rock Cafe Jakarta. Detail akan kami update secepatnya. Konser Amal Pengumpulan Coin #freeprita

Kuna tamasha linalopangwa kufanyika katika mgahawa wa Hard Rock katika jiji la Jakarta. Taarifa zaidi zitafuata baadaye kidogo. Tamasha la Hisani la Kukusanya Sarafu.

Treespotter: Wapendwa Wote, tafadhali tumbukiza sarafu kwa ajili ya Prita – tumbukiza sarafu kwa ajili ya hekima ya kiwango cha kawaida. Unaweza kutumbukiza sarafu nyingi vilevile. Anahitaji kiasi cha tani 2.5 cha sarafu hizo. http://koinkeadilan.com/
el15abeth: Vyombo vya habari vya kiraia havina ukomo … tunajua kwamba Prita hana hatia. Hukumu hiyo itazidi kutoa sura mbaya ya hospitali hiyo.
#freeprita

hiYano: #freeprita gambaran sebuah “dpr online” yang bisa lebih “berbahaya” daripada “dpr jalanan” jangan pernah remehkan kami yang “online”

#freeprita ni kielelezo cha bunge la watu la mtandaoni ambalo linaweza kuwa la “hatari” zaidi kuliko bunge la mtaani, kamwe usiwapuuzie wale walio mtandaoni.

Wataalamu wa sheria walisema kwamba hukumu dhidi ya Prita chini ya Sheria ya Mambo ya Mtandaoni (Cyber Law) haikuwa ya haki kwa sababu bado sheria hiyo haitaanza kufanya kazi kabla ya mwezi April mwaka 2010.

Blogger Aditya anatushirikisha mawazo yake kuhusu nguvu ya uendeshaji blogu ndogondogo:

Saya percaya dengan kekuatan jejaring sosial untuk menyebarkan kabar ini seluas-luasnya, paling tidak se-massive gerakan facebookers untuk gerakan “cicak vs buaya”. Tapi, saya tidak tahu apakah uang sejumlah itu dalam bentuk koin busuk pula akan terkumpul dalam waktu cepat.

Bukan saya mau meremehkan gerakan ini, tapi tahu sama tahu, biasanya yang seperti ini hangat-hangat di awal saja. Mudah-mudahan tidak ya!

Ninaamini katika nguvu ya mtandao wa kijamii katika kusambaza aina hii ya habari kwa mapana, walau kama inavyoonekana kwenye vuguvugu kubwa za wale walio kwenye facebook wakimuunga mkono Gecko v. Crocs (Maelezo ya mwandishi: mapambano ya kupiga vita ufisadi kati ya raia wa mtandaoni wanaounga mkono mpinga rushwa kwa upande mmoja na polisi kwa upande mwingine). Lakini, sina hakika kama kiasi hicho cha fedha katika muundo wa sarafu kinaweza kukusanywa mapema.

Siyo kwamba nataka kupuuzia vuguvugu hili, lakini sote tunajua, kitu cha namna hii kinaweza kuishia kupoteza joto lake na kuwa baridi kama kipolo cha viazi. Hata hivyo, natumaini hilo halitatokea!

Akihitimisha makala yake, Adithya anawaomba wasomaji wake:

Kawan, jika dan hanya jika, Anda peduli dengan persoalan kebebasan berpendapat dan perlindungan atas hak-hak konsumen, bergeraklah.

Marafiki, kama na kama tu, unajali kweli uhuru wa mtu wa kujieleza na kutetea haki za mlaji, basi hakikisha jambo hili halifi bali linaendelea.

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.