Habari kuhusu Haki za Binadamu kutoka Julai, 2013
Tamko la Kurekebisha Sheria Zinazokwaza Uhuru wa Vyombo vya Habari Nchini Vietnam
Zaidi ya wanablogu 60 wa Ki-vietinam walitia saini tamko la pamoja kuitaka serikali ya Vietnam kuboresha rekodi ya haki za binadamu na ahadi wanapowania uanachama katika Baraza la Umoja wa Mataifa ya Haki za Binadamu:...
Barua ya Wazi ya Kushinikiza Kuachiwa Huru kwa Mwanasheria
Mnamo Julai 23, 2013, zaidi ya raia 400 wa China wamesaini barua ya kushinikiza serikali ya China kumuachia huru Xu Zhiyong, ambaye ni mwanasheria mashuhuri na mpigania haki aliyekamatwa mnamo...
India: Chakula Chenye Sumu Chaua Watoto 24
Chakula kilichoua wanafunnzi na kuwaacha wengine katika hali mbaya kinasadikiwa kuwa kilichanganyikana na dawa ya kuulia wadudu. Tukio hili linaibua maswali kuhusiana na ubora wa chakula cha mchana wanachopewa wanafunzi wanaotoka katika familia masikini.
Watu Sitini Wauawa Kwenye Mapigano Mjini Nzérékoré, Guinea
Tovuti ya Guinee News inaripoti idadi ya vifo kufikia 60 kutokana na mauaji ya Nzérékoré, Guinea [fr] : Les cinquante deux corps qui étaient non identifiables ont été enterrés dans une...
Mama na Watoto Wake Wauawa kwa Kucheza kwenye Mvua
Mama na watoto wake wawili wa kike waliuawa kwa kufyatuliwa risasi mara baada ya watu watano waliokuwa wamefunika nyuso zao kuvamia nyumba alimokuwa akiishi mama huyu na watoto wake katika mji mdogo wa Chilas nchini Pakistan, tukio linalosadikiwa kuwa ni la mauaji ya kulinda heshima. Video iliyorekodiwa kwa simu inayowaonesha wasichana hao wakicheza kwenye mvua imekuwa ikisambaa kiholela na ambayo imeonekana kama ni kashfa na hivyo kuharibu heshima ya familia.
Misri: Wasalafi Washambulia Makazi ya Washia, Wanne Wauawa
Watu wanne nchini Misri ambao ni wafuasi wa imani ya Shia wameuawa leo nchini Misri mara baada ya nyumba waliyokuwa wanakutania kushambuliwa na Waislam wenye msimamo mkali, shambulio hili linafuatia wiki mbili za uchochezi dhidi ya waumini wa Shia. Kwa mujibu wa taarifa za awali, nyumba ambayo waumini hao wa Shia waliyoitumia kukutania, iliyopo huko Giza, Cairo, ilishambuliwa na kuchomwa moto. Kwa mujibu wa taarifa za habari za Al Badil, shuhuda mmoja alikaririwa akisema kuwa mmoja wa watu waliouawa alichinjwa na wengine watatu walijeruhiwa vibaya vichwani mwao. Tukio hili la kutisha lilizua ghadhabu kubwa mtandaoni.