Mama na Watoto Wake Wauawa kwa Kucheza kwenye Mvua

Mama na watoto wake wawili wa kike wameuawa kwa kufyatuliwa risasi mara baada ya watu watano waliokuwa wameficha nyuso zao kuvamia nyumba yao iliyopo katika mji mdogo wa Chilas huko Gilgit, Pakistan, tukio lililo taarifiwa kuwa ni mauaji ya kulinda heshima ya familia.

Wasichana hao wenye umri wa miaka 15 and 16, iliripotiwa kuwa waliuawa mnamo tarehe 24 Juni, 2013 kufuatia kusambaa kwa video iliyorekodiwa kwa simu ikiwaonesha wakiifurahia mvua katika bustani yao, hali iliyochukuliwa kuwa ni kosa na hivyo kuvunja heshima ya familia.

Serikali ilidai kuwa, muuaji alikuwa ni binamu wa wasichana hao ajulikanaye kwa jina la stepbrother Khutore ambaye alionekana kukerwa na video ile na hivyo kuwaomba rafiki zake wanne, kwa maoni yake, arudishe heshima ya familia yake. Marafiki zake walishakamatwa na kukiri makosa yao lakini Khutore hajataka kukiri kosa hilo la mauaji.

Kwa mujibu wa taarifa ya kila mwaka ya Tume ya Haki za binadamu ya Pakistan, mauaji ya ya kulinda heshima yanabaki kuwa ni “namna ya ukatili dhidi ya wanawake nchini Pakistan unayoendelea kushamiri na unaochukiza kabisa ” Mwaka 2012, wanawake 913 waliuawa kwa kulinda heshima ya familia zao, ikiwa ni pamoja na kuuawa kwa watoto 99, taarifa hiyo inaeleza.

Shafiqul Hassan Siddiqui alifafanua kwa kina sababu zinazopelekea kufanyika kwa mauaji ya heshima nchini Pakistan kwenye blogu ya Dunya:

Ni matokeo ya kulipiza kisasi. Asilimia 95% ya visasi hivi huelekezwa kwa wanawake. Mmoja wa ndugu wa familia (kwa kiasi kikubwa mwanaume), na kwa idhini ya watu wa familia nyingine, mwanamke anahukumiwa na kuuawa kwa sababu zisizo na msingi. Kwa familia yote, wakati huu unakuwa ni wa kujivunia pale wanapomtoa sadaka mtu wa familia yao kwa kuwa, mwanamke huyo aliwaondolea heshima. Kuna sababu nyingi za msingi zinazozingatiwa katika kutekeleza mauaji haya ya heshima.

Two Pakistani Teenage Sisters Noor Basra and Noor Sheza shot because of dancing in the rain. Screenshot from YouTube Video uploaded by NewsMedia24

picha iliyonaswa kutoka kwenye video inayodaiwa kuwa ndiyo iliyopelekea mauaji haya ya kinyama ya wasichana hawa. Video hii ilipakiwa kwenye matandao wa Youtube na na NewsMedia24

Akizungumzia mauaji ya hivi karibuni, Mkuu wa Kitengo cha Shirika la New York Times Pakistan, ndugu Declan Walsh (@declanwalsh) alitwiti:

@declanwalsh: Ukichaa kabisa- wasichana wawili na mama yao wameuawa kaskazini mwa Pakistan kufuatia kuonekana kwao wakifurahi kwa kucheza kwenye mvua. http://beta.dawn.com/news/1020576

Lubna Khan (@Lubnagigyani), ambaye ni mwanablogu wa masuala ya kijinsia, alitoa maoni yake kuhusiana na mauaji haya:

@Lubnagigyani: Ni tukio ovu kabisa la aina yake. Binadamu wanaoheshimiwa hawatekelezi mauaji kwa hali yoyote.CRIME of the heinous kind. Honourable humans do not KILL under any circumstances-egoistic machoism being the last

Mwanablogu wa mambo ya kisiasa, Zeesh (@zeesh2) alilizungumzia jambo hili akitumia msemo”mauaji ya heshima”:

@zeesh2: Mauaji ya heshima ni dhana inayotumiwa vibaya- hisia zinatumiwa vibaya- kama kweli wana heshima, wajiue wao wenyewe kuliko kuua wengine

A theatre performance displaying Violence on Women' during a protest. -- Hyderabad, Pakistan. Image bby Rajput Yasir. Copyright Demotix (6/8/2011)

Kikundi cha maonesho ya sanaa kikiigiza uonevu dhidi ya wanawake wakati wa maandamano huko Hyderabad, Pakistan. Picha na Rajput Yasir. Copyright Demotix (6/8/2011)

Gedrosia (@gedrosian), mtumiaji wa Twita kutoka katika jimbo la Balochistan, aliongeza kuwa, video hizo za simu zilizofichuliwa zimeshakuwa na madhara makubwa kwa wanafunzi wa kike katika maeneo yaliyo na msimamo mkali kuhusiana na dhana ya mauji ya heshima added that leaked mobile videos have had dire consequences for female students in conservative areas too:

@gedrosian: Kuna matukio kadhaa pia huko Balochistan ambapo kuna picha kutoka vyuoni/ shuleni ziliwekwa hadharani na wasichana waliondoshwa kutoka vyuoni

Akiandika siku chache kabla ya kutokea kwa mauaji haya ya hivi karibuni, The Future alitoa suluhisho la kumaliza mauaji ya kiheshima:

ninahisi kuwa mageuzi yanahitajika katika utaratibu wa namna wanaume wanavyotafakari kuhusiana na nguvu iliyo kwenye dhana hii.I feel that a revolution is required in the thinking pattern of the male members to change the existing notion of power. Kigezo katika tukio hili siyo kukweza upande mmoja wa jinsia dhidi ya jinsia nyingine, bali kinachotakiwa ni kuweka usawa miongoni mwa genda zote katika kufanikisha malengo ya pamoja, jamii iliyo bora na kuandaa wakati mzuri ujao wa vizazi vya sasa kwa kujivunia tamaduni zao wenyewe.blockquote>

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.