6 Julai 2013

Habari kutoka 6 Julai 2013

Mama na Watoto Wake Wauawa kwa Kucheza kwenye Mvua

  6 Julai 2013

Mama na watoto wake wawili wa kike waliuawa kwa kufyatuliwa risasi mara baada ya watu watano waliokuwa wamefunika nyuso zao kuvamia nyumba alimokuwa akiishi mama huyu na watoto wake katika mji mdogo wa Chilas nchini Pakistan, tukio linalosadikiwa kuwa ni la mauaji ya kulinda heshima. Video iliyorekodiwa kwa simu inayowaonesha wasichana hao wakicheza kwenye mvua imekuwa ikisambaa kiholela na ambayo imeonekana kama ni kashfa na hivyo kuharibu heshima ya familia.

Misri: Wafuasi wa Morsi Wapambana na Waandamanaji Wanaompinga Morsi

Mapambano yaliyotarajiwa kati ya wafuasi wa Muslim Brotherhood na waandamanaji waliotaka rais wa zamani wa Misri Mohamed Morsi aondoke yametokea leo [June 6, 2013]. Ilikuwa kama mchezo wa kuigiza na ulionekana moja kwa moja kwenye televisheni, na ulirushwa kwa moja kwa moja na vituo vya televisheni vya ndani na vile vya kimataifa. Watu wasiopungua 17 waliuawa na zaidi ya waandamanaji 400 wakijeruhiwa katika mapigano nchini kote Misri leo, tukio ambalo mitandao mingi ya kijamii inalielezea kama "lililotarajiwa" na "linalosikitisha."

China Yawaamrisha Vijana Kuwatembelea Wazazi Wao

  6 Julai 2013

Wiki hii, China imeanza kutumia sheria mpya inayowataka watoto waliokwisha fikia umri wa kujitegemea kuwa na mazoea ya kuwatembelea wazazi wao, hali iliyopelekea sheria hii kudhihakiwa na watumiaji wa tovuti ya jukwaa maarufu la wanablogu la China lijulikanalo kama Sina Weibo.