Misri: Wasalafi Washambulia Makazi ya Washia, Wanne Wauawa

Watu wanne nchini Misri ambao ni wafuasi wa imani ya Shia wameuawa nchini humo hii leo mara baada ya nyumba waliyokuwa wanakutania kushambuliwa na Waislam wenye msimamo mkali , hali iliyotokana na uchochezi dhidi ya watu wa imani ya Shia.

Kwa mujibu wa vyanzo mbalimbali vya habari, nyumba ambayo washia waliyokuwa kikikutania huko Giza, jijini Cairo, ilishambuliwa na kuchomwa moto. Kwa mujibu wa habari kutoka Al Badil, mtu mmoja alikaririwa kutoka kwenye chumba cha kuhifadhia maiti[ar] ambaye alisema kuwa, mmoja kati ya watu waliouawa kwa kuchinjwa na wengine watatu walijeruhiwa vibaya vichwani mwao. Tukio hili la kuhuzunisha liliibua hasira kwa watumiaji wa mtandao wa intaneti.

Hazem Barakat aliandaa waraka wa tukio hili la kinyama, aliweka picha za watu walioonekana kutokwa na damu nyingi pamoja na kuweka video inayoonesha shambulio hili (Warning: Graphic video) mtandaoni. Katika ukurasa wa Twita, anasema kuwa alitishwa kwa kuweka mtandaoni tukio hili alilolishuhudia. Anaongeza [ar]:

انا على اتم الاستعداد للشهاده امام النيابه وهقول كل اللى حصل بالتفاصيل وهقول على الشيوخ اللى حرضت على القتل

@7azem122: nipo tayari kuthibitisha kwa mwendesha mashitaka wa umma na nitasema kwa kina kile kilichotokea na nitataja wazi kuwa makasisi ndio waliochochea mauaji haya.

People gather at the alley in which the house where the Shia were killed in Cairo today. Photograph shared on Twitter by @7azem122

watu wakiwa wamejikusanya katika barabara nyembamba karibu na nyumba ambayo washia hao walipouawa leo huko jijini Cairo. Picha iliwekwa katika mtandao wa Twita na @7azem122


Anaendelea kusema kuwa:

التحريض على الشيعه بدأ من اسبوعين فى جميع المساجد والنهارده كان التنفيذ شيوخ ولاد دين كلب ” قتلوهم وعندهم اطفال لسه صغيرين :(

@7azem122: Uchochezi dhidi ya watu wa imani ya Shia ulianza wiki mbili zilizopita katika misikiti yote na siku ya leo wamekamilisha mpango wao. Makasisi hao ni watoto wa Mbwa. Waliwatumia watoto kwenye mauaji haya ya kikatili.

Masaa matano yaliyopita aliTwiti:

السلفيين بدأو يكسرو سقف البيت اللى فيه الشيعه مشهد سيريالى رهيب


@7azem122
: Waislam wenye msimamo mkali wameanza kuvunja paa la nyumba walipo watu wa imani ya Shia. Tukio hili, kama vile ni la kusadikika, lakini ndio hali halisi.

Police remained idle as a home where Shia Egyptians were meeting today was attacked by Salafists, says Hazem Barakat (@7azem122)

Hazem Barakat anasema kuwa, polisi hawakutimiza wajibu wao kufuatia Salafists kushambulia nyumba waliyokuwa wakikutania waumini wa Shia huko Misri (@7azem122)

Pia aliwatuhumu askari polisi pamoja na maafisa wengine kuwa walifahamu fika tukio lile na pia walishuhudia mauaji yale.

Tukio hili liliwaghadhabisha watumiaji wengi wa mtandao wa intaneti.

Mwandishi wa Tashtiti, Daktari Bassem Youssef anatwiti:

النهاردة شيعي بكرة صوفي بعده قبطي قبله بهائي و بعدين مسلم مش موافق على تطبيق الشريعة بفكركم و بعدين واحد شكله مش عاجبك.

@DrBassemYoussef: Leo ni kwa waumini wa Shia; kesho itakuwa Sufi, na kisha waumini wa Kopti, na kabla yake Bahai. Kisha itakuwa ni zamu ya waislam ambao hawakubaliani na namna usimamiavyo sheria ya sharia (mafundisho ya kiislam) ikilinganishwa na msimamo wako na kisha itakuwa zamu ya mtu ambaye hapendezwi tu na muonekano wake.

Mwanablogu wa Misrir Zeinobia alitoa mawazo yafananayo na yaliyotangulia kusemwa:

و النهاردة الشيعة و بكرة جارك اللى مش متفق معاك سياسيا و فكريا

@Zeinobia: na leo ikiwa ni kwa waumini wa shia, kesho itakuwa kwa jirani yako ambaye mmetofutiana kisiasa na kiweledi.

Ahmed Abou Hussein anauliza:

لما شيخك يكفر المتظاهرين ويلقب الشيعة بالأنجاس ماتستغربش انهم يقتلوا. يا مرسي السؤال مش انت فقدت شرعيتك ولا لأ، السؤال انت فقدتها كام مرة؟

@abouhussein7: Kasisi wako [Rais Mohamed Morsi] anasema kuwa, waandamanaji ni wapagani na kuwa waumini wa Shia ni wafuska na hivyo usishangae wanapouawa. Morsi, swali siyo labda umeshapoteza uhalali kama Rais. Swali ni kuwa, ni mara ngapi umeshapoteza uhalali kama Rais?

Ahmad Khalil anashangazwa na jinsi watu wanavyoyachukulia mauaji:

السلفيين قتلوا ٤ شيعة ، الغريب فى الامر ان من يستنكر هذا الفعل يقول دم المسلم حرام يعنى دم المسيحى حلال ، الافكار الطائفية اصابت الجميع

@ahmad_khalil: Wakereketwa wa harakati za Kiislam wameshawaua waumini wanne wa Shia. Kinachoshangaza ni kuwa kuna baadhi ya watu ambao miongoni mwao ndio wanaolaani kitendo hiki na kwa upande mwingine watu hawa wanaamini kuwa kumwaga damu ya Muislam ni Haramu (yaani hairuhusiwi katika Uislam). Yaani ni kama vile, kumwaga damu ya Mkristo ni halali (yaani inaruhusiwa katika Uislam). Mawazo ya kimadhehebu ya aina hii yamemtesa kila mmoja.

Sherif Azer aandika [ar]:

فيه احداث و تصريحات كتير حصلت في الفترة الاخيرة كانت بتمهد للهجوم على #الشيعة في مصر.عدم الاستعداد لموقف زي ده في حد ذاته جريمة #مصر

@sherif_azer: kuna matukio mengi na kauli zilizotokea kipindi fulani kilichopita yaliyokuwa sehemu ya matayarisho ya tukio la kushambuliwa kwa waumini wa Shia huko Misri. Matayarisho ya tukio hili hayachukuliwi kama ni kosa la jinai.

Na Adel Salib anashangaa ni kwa nini watu wanapatwa na mshituko kufuatia kushambuliwa kwa waumini wa Shia huko Misri wakati kabla ya hapo polisi waliwashambulia na kuwaua wakristo wazawa wa Misri:

مندهش من المندهشين ان الشرطة وقفت تتفرج علي قتل الشيعة ؛ اذا كان الشرطة كانت من شهرين بتضرب الكتدرائية انتم عالم مغيبين ولا بتستهبلوا ؟

@Adel_Salib: mtu fulani anaweza kushangazwa kuwa polisi walikuwa wakishuhudia wakati waumini wa Shia walipokuwa wakiuliwa, wakati kwa upande mwingine miezi miwili iliyopita, polisi walishambulia Parokia. Umelaaniwa au ni upumbavu?

A screenshot of a tweet by Mohammed Saber, an anchor at an Egyptian Television celebrating the murder of Shia in Egypt. Photograph shares by @Gemyhood on Twitter

picha iliyopigwa kutoka kwenye Twiti iliyowekwa na Mohammed Saber, ambaye ni mtangazaji na msimamizi wa matangazo katika Televisheni ya Misri akisherehekea mauaji ya waumini wa Shia waishio Misri. Picha imewekwa na @Gemyhood katika mtandao wa Twita


Ali anaongeza:

زعلان ان المسلمين السنة بيتدبحوا في بورما ..وفرحان ان المسلمين الشيعة بيتحرقوا أحياء و يتمثل بجثثهم .. انت لازم تقوم تشوف دكتور بيطري كويس

@ali4592000: una hasira kuwa waumini wa kiislam wa Sunni wanauawa huko Burma na kuwa na furaha kuwa waumini wa kiislam wa Shia wanachomwa moto wakiwa hai nchini Misri na kisha miili yao kunajisiwa? Unapaswa kumtafuta daktari mzuri wa wanyama.

Rawah Badrawi ashirikisha historia fulani:

@RawahBadrawi: Kairo ilijengwa na watu wa Shia enyi watu msiostaarabika. Walianzisha nusu ya maeneo ya Urithi wa Kairo ikiwa ni pamoja na Al Azhar.

Naye mwanablogu wa Yemeni, Noon Arabia anahitimisha:

نحن نعود إلى زمن الجاهليه. الإسلام بريء مما يحدث الآن من سفك الدماء. #مصر #لبنان #سوريا

@NoonArabia: We are returning to the age of Jahiliyya [ignorance]. Uislam hauna hatia kwa watu wanaouawa huko Misri, Lebanon na Syria.

Kwa kweli, siyo kila mmoja aliyeshitushwa na shambulizi hili. Mwanablogu Mohamed Beshir aweka Twiti ya mtangazaji wa Televisheni ya Misri ajulikanaye kwa jina la Mohammed Saber, ambaye anasherehekea mauaji ya waumini wa Shia na kutaka wengine zaidi wa shia wauawe.

دة مذيع ف التلفزيون المصري سعيد بقتل الشيعة والناس بترد عليه يأكد ويبشرهم

@Gemyhood: Huyu ni mtangazaji wa Televisheni ya Taifa ya Misri akifurahia mauaji ya waumini wa Shia

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.