Habari kuhusu Haki za Binadamu kutoka Agosti, 2012
Iran: ‘Marufuku Isiyo Rasmi ya Kutembea’ ya Tehran Wakati wa Mkutano wa NAM
Mkutano wa 16 wa Umoja wa Nchi Zisizofungamana na Upande Wowote ulianza mnamo tarehe 26 Agosti, 2012 jijini Tehran huku kukiwa na ulinzi mkali. Umoja huo madhubuti (NAM) unaoundwa na nchi ni mabaki ya mvutano uliokuwepo enzi za Vita Baridi kati ya Mashariki na Magharibi, na umoja huu unachukuliwa na Iran pamoja na mataifa mengine kama jukwaa mbadala kwa ajili ya kuendesha mijadala kuhusu masuala mbalimbali yanaoukabili ulimwengu hivi sasa. Iran inasema inapanga mazungumzo kuhusu mpango wa amani ili kukomesha vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini Syria, lakini hakuna uwakilishi kutoka upande wa waasi ulioalikwa kwa sababu Tehran ni rafiki wa karibu wa utawala wa Rais Bashar Assad wa Syria.
Tanzania, Ethiopia: Meles Zenawi ‘Atuma Twiti’ Kutoka Kilindi cha Kaburi
"@zittokabwe tafadhali uwe bora kuliko mimi nilivyokuwa. Huku juu hakuna utani, tayari ninalipia makosa yangu." Twiti iliyotumwa na Waziri Mkuu wa Ethiopia Meles Zenawi baada ya kifo chake kwenda kwa Mbunge wa Tanzania Zitto Kabwe na kuibua mjadala mtandaoni.
Mauritania: Wafanyakazi wa Migodini Wapinga ‘Aina Mpya ya Utumwa’
Zaidi ya wafanyakazi 2,300 wako kwenye mgomo nchini Mauritania katika mji wa kaskazini wa Zouerat, jambo ambalo limesababisha kuzorota kwa maeneo mengine kumi ya Kampuni la Taifa la Madini na Viwanda, huku kazi zikiwa kwenye mvurugiko mkubwa. Madai yamejikita katika suala zima la maslahi bora ya wafanyakazi.
Saudi Arabia: Mwanaharakati Reema Al Joresh Atiwa Kizuizini katika Sikukuu ya Idi
"Hamjambo? Polisi wamenikamata mimi na watoto wangu." - Reema Al Joresh, mke wa mfungwa ambaye amekuwa kizuizini kwa miaka nane bila kufunguliwa mashtaka, alikuwa akielekea msikitini ili kutoa zawazi 500 pamoja na barua ya kueneza taarifa kuhusu itiaji nguvuni wa kiholela katika ufalme huo.
Morocco: Wanafunzi Wadai Marekebisho kwenye Mfumo wa Elimu
Mwezi Julai, kikundi cha wanafunzi wa nchini Morocco kilizindua ukurasa wa Facebook ulioitwa "Umoja wa Wanafunzi wa Morocco kwa ajili ya Mabadiliko ya Mfumo wa Elimu". Pungufu ya mwezi mmoja, kikundi hiki kilivuta uungwaji mkono mkubwa hasa kupitia mitandao ya kijamii.