Saudi Arabia: Mwanaharakati Reema Al Joresh Atiwa Kizuizini katika Sikukuu ya Idi

 

Mwanaharakati wa Ufalme wa Saudia ambaye pia ni mtumiaji Twita, Reema Al Joresh, alitiwa mbaroni kwa muda mfupi mapema leo [19 Agosti 2012] wakati alipokuwa anaelekea  kwenye msikiti kusherehekea Sikukuu ya Idi el Fitr — ambayo ni maalumu kwa Waislamu mara baada ya Mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani. Al Joresh ni mkosoaji mkubwa dhidi ya wizara ya Mambo ya Ndani ya Saudi kwa kuwekwa watu kiholela kizuizini. Aidha, yeye ni mke wa mfungwa ambaye amekuwa kizuizini kwa miaka nane bila ya kufunguliwa mashtaka.

 

 

Alikusudia kutoa zawadi zipatazo 500 pamoja na barua ya kukuza uelewa wa watu kuhusu suala la kukamatwa kwa watu kiholela nchini Saudi Arabia.

Saa 5:11 alfajiri (saa za Saudia), Al Joresh alituma twiti:

السلام عليكم الشرطة مسكونا انا وعيالي
Hamjambo? Polisi wamenitia mbaroni mimi na watoto wangu.

Photo posted by Reema Al Joresh on Twitter as she tweeted: We have been arrested

Picha imewekwa na Reema Al Joresh wakati akituma twiti: Sisi tumekamatwa [ar]

Alama ashiria ilianzishwa mara moja na watumiaji twita wa Saudi walioonyesha hisia zao za kuchukizwa na vitendo vya aina hiyo.

Abdulaziz al-Shihri alitwiti:

المباحث لا مروءة أهل الجاهلية ولا أخلاق أهل الإسلام ، اللهم أرحنا من هذا الجهاز كما أرحت المصريين من أمن الدولة #ريما_الجريش
“Askari kanzu hawana si tu ukarimu uliokuwepo kabla ya Uislamu, bali hata maadili ya baada ya kuwepo Uislamu. Ee Mungu, hebu tupumzishe – kama Wamisri -kwa kuwaondolea mbali hawa “

Mohammad al-Ogaimi aliongezea:

#ريما_الجريش كان يتابعها 800 والآن 2100 .. بقمعك يصل صوتك أكثر ..
Alikuwa na wafuasi 800 wa Twita, sasa anao 2100. Pamoja na ukandamizaji wenyu, sauti zao zitakwenda mbali zaidi.
Screen shot showing Al Joresh's followers on Twitter

Picha ya ukurasa wa Twita wa Al Joresh ukionyesha idadi ya wafuasi alio nao kwenye Twita

Maoni hayo yanahusu idadi ya wafuasi alikuwa nao Al Joresh kwenye Twita. Wakati wa kuandika posti hii, walikuwa wameongeza na kufikia karibu 3500 huku wakiendelea kuongezeka.

Wakati Reema alipoachiliwa, aliandika mfululizo wa twiti kueleza yaliyotokea:

Saa 10:30 alfajiri, mimi nilielekea kwenye msikiti wa Eid na zawadi zangu. Mita 100 kutoka kwenye nyumba yangu, gari lilijaribu kutuzuia na wakatuelekezea bunduki. Binti yangu Sara akawaambia: “Mmemuiba baba yangu na sasa mmekuja kutuiba sisi?”. Walijaribu kumnyamazisha binti yangu [mwingine] Marya, ambaye alikuwa analia. Walimtoa mwanangu Mo'ath na dereva nje ya gari kisha polisi alijaribu kuchukua simu yangu, lakini Mo'ath alimwambia asiniguse hata chembe […] walichukua zawadi na […] polisi alikuja katika kiti cha mbele na alimwamuru dereva kuelekea katika ofisi ya Mkuu wa Upelelezi huko Buraidah. Kwa saa moja, walinihoji na kujaribu kutafuta mabomu ndani ya yale masanduku […] Walinitaka niandike kukiri kwangu makosa.

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.