Habari kuhusu Haki za Binadamu kutoka Aprili, 2012
Senegali:Rais Wade Aandamwa Hata Baada ya Kukubali Kushindwa Uchaguzi
Wakati nchi nyingine zikionekana kushangilia "uungwana" wa Bbdoulaye Wade kukubali matokeo nchini Senegali, wanablogu wa nchi hiyo bado wamemkaba koo Wade kwa kuushambulia Urais wake wakikumbushana ghasia za kuelekea uchaguzi, kubinywa kwa uhuru wa habari na mifano mingi ya utawala mbovu.
Mali: Kimya cha Wanablogu wa Nchini Humo
Wakati mtandao wa intaneti umetawaliwa na blogu, ujumbe wa twita na video kutoka nchi mbalimbali, watumiaji wa intaneti wenyeji wa Mali wangali kimya. Mji mkuu, Bamako, umeathirika kwa kukatika kwa umeme kwa kile kinachodaiwa kuwa kuadimika kwa mafuta. Katika mazingira kama haya, kipaumbele si kutuma ujumbe, bali kutafuta kutafuta taarifa kuhusu viongozi wapya wa sehemu ya Kaskazini ya Nchi hiyo.
Taiwan: Kufukuzwa kwenye nyumba kwa nguvu kwa familia kwaitia dosari Sheria ya Ufufuaji Miji
Kufukuzwa kwa kinyama kwa familia ya Wang kulikotekelezwa na serikali ya Jiji la Taipei kulionyesha jinsi haki za raia zilivyo dhaifu mbele ya miradi ya ufufuaji mji. Kumekuwepo na maoni mengi yanayotaka Sheria ya Ufufuaji Miji irekebishwe.
Congo (DRC): Video zasaidia kumtia hatiani Thomas Lubanga kwa uhalifu wa kivita
Mnamo tarehe 14, Machi, mahakama ya kimataifa ya makosa ya kivita ilimtia hatiani Thomas Lubanga, kiongozi wa zamani wa waasi Kongo (DRC) Mashariki, kwa kosa la kuwatumia watoto katika vita. Jaji alisema picha za video zilizoonyesha mahojiano na askari hao watoto ziliziongeza uzito wa ushahidi ulioisaidia mahakama kutoa hukumu.
Ukraine: Gereza la Lukyanivska – “Mahali Watu Wanapotendewa kama Wanyama”
Mnamo tarehe 2 Aprili, Televisheni ya Ukraine ya TVi ilirusha filamu iliyotayarishwa na Kostiantyn Usov kuhusu hali ya maisha na jinsi mahabusu wanavyotendewa katika gereza la Kyiv la Lukyanivska, na pia kuhusu kuenea sana kwa rushwa miongoni mwa askari magereza. Kwa uchache, wengi katika wale ambao tayari wametazama video ya Usov walishtushwa sana na yale waliyoyaona.