Taiwan: Kufukuzwa kwenye nyumba kwa nguvu kwa familia kwaitia dosari Sheria ya Ufufuaji Miji

Kitendo cha kinyama cha kufukuzwa kwa familia ya Wang kilichofanywa na serikali ya Jiji la Taipei kiliuonyesha wazi umma jinsi haki za raia zilivyo tete mbele ya mradi wa ufufuaji miji. Kumekuwa na ongezeko kubwa la maoni ya umma yanayomtaka Waziri Mkuu, Chong Chen, kupitia upya Sheria ya sasa ya Ufufuaji Miji [zh].

Upotoshaji wa maoni ya wakazi

Hsieh-Li Wang alionyesha jinsi [zh] Sheria ya sasa inavyoyaruhusu makampuni ya ujenzi kuendelea na mipango ya ufufuaji miji hata pale ambapo wakazi wengi hawataki kujiunga kwenye mradi huo:

Nyumba ya akina Wang kabla ya kubomolewa. Picha na mtumiaji wa Flickr anayeitwa munch999(CC BY-NC-SA 2.0).

Nyumba ya akina Wang kabla ya kubomolewa. Picha na mtumiaji wa Flickr anayeitwa munch999 (CC BY-NC-SA 2.0).

都更條例的大陷阱在此:都更條例第十條第二款規定的「十分之一所有權人同意,再加上土地或建物樓地板面積超過十分之一,即可申請更新」。這是什麼意思?來自五分埔的都更受害戶李昭玫說,「就是只要有錢人或建商想都更,買下幾戶,灌進大量人頭,然後佔多數,就可以開啟都更大門。」李昭玫的社區就遇到幾戶灌進七十多個人頭的個案。

Mtego wa Sheria hiyo uko hapa: kwa mujibu wa Kifungu cha 10 mstari wa pili ‘Pale ambapo walau asilimia 10 ya wenye nyumba ambao kwa pamoja wanamiliki zaidi ya asilimia 10 ya ardhi wanapokubali kujiunga na mradi, basi hao wanaweza kuomba kujiunga na mradi wa ufufuaji miji.’ Je, kifungu hiki kina maana gani? Chao-Wen Lee, ambaye ni mmoja wa wahanga wa mradi wa ufufuaji miji huko Wufenpu, alisema, ‘hiyo ina maana kwamba kikundi cha watu fulani matajiri au kampuni ya ujenzi inapotaka kutekeleza mpango wa kufufua mji, wanaweza kununua baadhi ya nyumba katika eneo hilo na kuwaweka watu wengi kuwa wamiliki wenza; watu hawa wanapokuwa ndiyo wengi miongoni mwa wamiliki, basi hapo hakuna namna ya kuzuia mpango wa kufufua miji kutekelezwa.’ Mathalani, katika jamii ya Chao-Wen Lee, zaidi ya asilimia 70 ya wakazi waliandikishwa kama wamiliki wa baadhi tu ya nyumba.

Kwa kutumia Kifungu cha 25 cha Sheria ya Ufufuaji Miji, serikali inaruhusiwa kupitisha mradi wa ufufuaji miji pale asilmia 80 ya wakazi waliohusishwa wanapokubali kujiunga na mradi [zh]. Kwa wale watakaopinga kujiunga na mradi, wataadhibiwa kwa kufukuzwa kwa nguvu na serikali. Yo-Yu Hsih, anayesomea sheria aliikosoa sheria hiyo [zh] akisema inasababisha uzandiki wa watu walio wengi kukiuka haki za wachache.

採行多數決同意之目的,無非係要使珍貴稀少的土地資源有效利用,避免在都更劃定範圍內發生少數綁架多數,阻礙都更進行,延滯都市發展。

按多數決同意的制度多有走向多數暴力的風險,其並無法兼顧全體所有權人之利益…目前都更條例第22條第1項僅有多數決原則而無相關保護少數人之制度,如此對少數人甚為不利,恐已違反最小侵害原則。

Lengo la mwanzo la uamuzi wa wengi lilikuwa kutumia rasilimali ya ardhi, iliyo haba, kwa ufanisi zaidi. Ililenga pia kuzuia vitendo vinavyoweza kuashiria kupokwa kwa haki ya walio wengi na watu wachache ambao wanataka kuzuina kuendelezwa kwa ufufuaji miji na majiji.

(Hata hivyo) Uamuzi wa wengi unaweza kusababisha uzandiki unaosababisha maslahi ya wachache kupotea … Hivi sasa, Kifungu cha 22, mstari wa 1 wa Sheria ya Ufufuaji Miji kinapitisha uamuzi wa wengi pasipo kutoa kinga yoyote kwa wale walio wachache. Jambo hili litawaweka walio wachache katika hali ya kuonewa huku haki zao zikitishiwa. Ninasikitika kusema kwamba Sheria hii imekiuka kanuni za sheria za kuingilia haki za wengine.

Bango likiwa nje ya nyumba za akina Wang. Linasema 'nyumba yangu ilinunuliwa nilipokuwa na umri wa miaka 40, na ilibomolewa nilipokuwa na miaka 70.' Picha na mtumiaji wa Flickr anayeitwa munch999 (CC BY-NC-SA 2.0).

A poster outside Wang's houses. It says ‘my house was bought when I was 40, and it was torn down when I was 70.’ Photo by Flickr User munch999 (CC BY-NC-SA 2.0).

Kuhusika kwa Serikali

Hsieh-Li Wang alihoji [zh] kwa nini Sheria iliruhusu serikali kuwatumia polisi ili kulinda maslahi ya wawekezaji:

更爭議的是,第三十六條規定,建商可向政府申請,由公權力代為拆除拒遷戶。讓不少專家認為,都更條例的多數決和過度支持建商,有違背憲法對人民財產保障的基本權利.

Kifungu cha 36 cha Sheria ndiyo chenye utata zaidi: kampuni ya ujenzi inaweza kukata rufaa kwa serikali ili iweze kuvunja nyumba kwa nguvu pale wakazi wake wanapokataa kuondolewa. Wataalamu wengi wanaamini kwamba Sheria, ambayo inahalalisha matumizi ya njia ya uamuzi wa wengi na ushiriki wa serikali katika kuwaunga mkono wawekezaji, imekiuka kinga inayotolewa na Katiba kuhusiana haki za mali za raia.

Chama cha Haki za Binadamu cha Taiwan kilidai ufanyike upitiaji wa kina wa Sheria ya Ufufuaji Miji kwa mujibu wa Katiba. Katika Chombo cha Kutunga Sheria cha Yuan, mbunge Mei-Nyu You alijenga hoja [zh] kwamba Waziri wa Mambo ya Ndani afanyie marekebisho Sheria ya sasa ya Ufufuaji Miji:

今天如果你的房子出租,遇到一個奧客不肯搬走,你能不能用公權力直接把他趕走?…你得要先去法院告他打官司,拿到勝訴後再向法院聲請強制執行,法院還會給他一個緩衝期讓他搬遷,這是尊重人民居住的權利.

Leo hii, kama umempangisha nyumba yako mtu ambaye anagoma kuhama, unaweza kukata rufaa kwa mamlaka ili kumhamisha mpangaji huyo? v…Unahitajika kumfungulia mashtaka mpangaji huyu. Kama ukishinda kesi, basi unaweza kuomba amri ya mahakama itumike kumhamisha. Kwa kawaida, mahakama itampa mpangaji muda maalumu wa kuhama, na hivi ndivyo Katiba yetu inavyotoa kinga kwa haki za ukaazi.

今天我的房子好好的,沒有礙到誰,沒有因為交通、安全、房子破舊需重建的問題,完全沒有。只是因為建商看中我的土地,看中我的容積率,就叫我非遷(不可),然後就越過司法權,直接用行政權介入來拆房子,這樣符合程序的正義嗎?

Leo hii nyumba yangu iko katika hali nzuri na wala haizibi nyumba za majirani, barabara au kuhatarisha usalama wa raia. Lakini, mara tu mwekezaji akiitamani ardhi yangu na jinsi inavyoweza kumpa nafasi, anaweza kabisa kuniondoa mimi kutoka kwenye nyumba yangu (pasipo ridhaa yangu). Mwekezaji huyo anaweza hata kuizunguka mahakama kwa kwenda kukata rufani kwa mamlaka za utawala na kupata nguvu ya kuja kubomoa nyumba yangu. Je, hapa kweli kuna haki kwa mujibu wa Katiba?

Kutetea haki za kikatiba

Torrent alikosoa siasa za uchaguzi za vyama vya siasa na kurejea [zh] kutegemea nguvu ya raia katika kulinda haki zao za kikatiba:

Mchoro wa Graffiti wa kupinga mradi wa ufufuaji miji. Picha na mtumiaji wa Flickr anayeitwa theAthena (CC BY-NC-SA 2.0).

Graffiti against an urban renewal project. Photo by Flickr User theAthena (CC BY-NC-SA 2.0).

與民眾權益攸關高居憲法總綱後的第二章人民之權利義務,越來越成為其它章節爭奪戰中的口號…台灣社會已經縱容這些人的謊言太久,他們告訴我們只要搶到憲法第四章的總統大位、得到第六章立法權的多數,就能夠自然達到憲法第二章居住權、遷徙權、言論權、生存權、工作權、財產權,但他們永遠都有理由和藉口。

Sura ya pili ya Katiba yetu inafafanua haki na wajibu wa wa raia, ambazo kwa kiasi kikubwa zimegeuzwa kuwa ngebe kupitia kampeni mbalimbali za kisiasa … Jamii yetu iko kama inayounga mkono uongo unaotolewa na wanasiasa kwa muda mrefu sasa kupita kiasi. Walitueleza kwamba tunaweza, hatimaye, kufurahia haki zote zinazotajwa kwenye Sura ya Pili ya Katiba yetu, yaani baada ya wao [kushinda uchaguzi na] kushika madaraka ya urais kwa mujibu wa Sura ya Nne ya Katiba yetu na baada ya kupata viti vingi kwenye Bunge kwa mujibu wa Sura ya Sita ya Katiba yetu. Lakini, daima huwa wanaibuka na visingizio kibao ili kutotimiza ahadi zao.

所以我們要求改革不正義的都更,保障每一個人民的居住權。這才是寫台灣人民的歷史,才能從龐大的謊言中抗爭出空隙拿回屬於我們的憲法。

Hii ndiyo sababu tunadai yafanyike mabadiliko ya Sheria hii ya Ufufuaji Miji isiyo ya haki, maana tunataka kulinda haki za kila raia kuwa na makazi. Hatuna budi kuhakikisha kwamba tunaifanya Katiba yetu ifanye kazi inavyostahili, isichafuliwe na uongo wote huo wanaotoa kila mara, ili tupate kuandika upya historia ya watu wa Taiwan.

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.