Ukraine: Gereza la Lukyanivska – “Mahali Watu Wanapotendewa kama Wanyama”

Mnamo tarehe 2 Aprili, mwaka huu, kituo cha televisheni cha TVi kilitangaza habari Kostiantyn Usov's documentary [uk, ru] inayohusu hali ya maisha na namna wafungwa wanavyotendewa katika gereza la lililopo Kyiv linalojulikana kama Lukyanivska (vilevile linajulikana kwa Ki-Ukrenia kama Lukyanivsky SIZO, au mahabusu),ambapo pia askari katika taasisi hiyo wanajulikana kwa kupenda kwao rushwa.

Filamu hiyo ambayo inaptikana kwenye YouTube, inaonyesha picha za video zilizochukuliwa kwa simu ya mkononi kwa njia za siri na harakaharaka na idadi fulani ya wafungwa katika miezi kadhaa iliyopita kufuatia kuombwa na mwandishi wa habari.

Watu wengi miongoni mwa wale ambao wamekwishaona filamu hiyo ya Usov, kwa ufupi, walishtushwa mno na yale waliyoona.

LEvko wa blogu ya the English-language Foreign Notes aliandika yafuatayo katika makala aliyopita jina la, “Gereza la Lukyaniv lililogeuka kuwa tundu la jehanamu”:

Mwandishi shupavu wa habari za uchunguzi wa kutoka TVi Konstyantyn Usov hivi karibuni alifaulu kuingiza kwa siri simu kadhaa za mkononi kwenye gereza linalosifika kwa ukatili la Lukyaniv, ambapo kuna kitengo cha uchunguzi maalumu, mahali ambapo [ex-PM Yulia Tymoshenko] alitiwa kizuizini, na ambapo [ex-minister of internal affairs Yuriy Lutsenko] bado anaendelea kushikiliwa. Katika filamu yake ya televisheni inayoweza kusababisha jinamizi inaweza kupatikana hapa….

Hali katika baadhi ya vyumba vya gereza hilo ni mbaya mno … za kutisha … tafadhali usiitazame muda mfupi kabla ya kwenda kulala …

Kumbuka, mahabusu wanaoonyeshwa bado hawajahukumiwa – huenda wengi wao hawana hatia ingawa hata hivyo wamekuwa kizuizini kwa miaka mingi ….

Ni vigumu kuamini kwamba binadamu wanaweza kutendewa vibaya kiasi hicho tena katika taasisi ya serikali katika mji mkuu wa nchi ya kidemokrasi barani Ulaya katika karne ya 21 … ni jambo linalotia kinyaa na aibu kubwa. […]

Gereza la Lukyanivska lilipata kufahamika kwa macho ya kimataifa mwaka jana, pale Waziri Mkuu wa zamani, Yulia Tymoshenko alipowekwa kizuizini katika gereza hilo na hasa wakati wa kesi yake. Miriam Elder wa gazeti la The Guardian alizungumzia kuhusu taasisi hiyo ya mahabusu mnamo tarehe 16 Oktoba, 2011:

[…] Tymoshenko bado yupo katika gereza la Lukyanivska, ambalo linatumika zaidi kama kituo cha mahabusu wanaosubiri kesi zao. Waziri Mkuu huyu wa zamani amewekwa kwenye chumba chenye ukubwa wa mita zipatazo 15 pamoja na wanawake wengine wawili, wote wakisubiri kesi za uhujumu uchumi.

Kuna dirisha dogo ambalo limewekewa safu tatu za nondo. Hakuna maji ya moto na kuta nene za karne ya 19 zinafanya hali ndani ya gereza hili iwe ya baridi na yenye unyevunyevu. Tymoshenko anatumia muda wake wa siku kujisomea. […]

Mwezi Desemba 2011, picha ya video iliyopigwa kwa siri na kuvujishwa ilimwonyesha Tymoshenko akiwa katika kitengo cha matibabu cha gereza la Lukyanivska. Video hiyo ilirushwa hewani kupitia televisheni na vilevile mitandao ya kiraia ya huko Ukraine. kwa upande wake Reuters ilitoa habari mnamo tarehe 15 Desemba:

[…] Picha hiyo ya video ilikuwa moja kati ya mbili zilizorushwa hewani na televisheni ili kuonyesha kwamba Tymoshenko alikuwa akitendewa vema na kuwa aliishi maisha mazuri sawa na kwenye hoteli za kifahari.

[…]

Katika picha hiyo, askari magereza wanaonekana wakishughulika kumsaidia mpiga picha za video kufanya kazi hiyo, kiasi hata cha kumusaidia kufunika tundu la ufunguo katika mlango wa kuingilia eneo hilo.

Tyomoshenko mwenye umri wa miaka 51, alikuwa amefunikwa na mashuka, na alionyesha wazi kuwa hakufurahishwa na kitendo cha kuchukuliwa kwa filamu ile, ingawa maneno yake hayakuweza kusikika.

Katika sehemu moja ya picha hiyo ya video, ambayo ilionyesha chumba kilicho na samani za maana ikiwa ni pamoja na jokofu, Tymoshenko anaweza kusikika akisema: “Nilikuwa nimewekwa mahali penye hali mbaya sana, sitaki mwonyeshe picha hizi zinazodanganya kuhusu hali halisi sasa.” […]

Lakini katika filamu yake, Kostiantyn Usov, anaonyesha hali halisi ilivyo katika gereza la Lukyanivska, kama mahali ambapo maelfu ya raia wa Ukraine ambao hawana fursa ya kuonekana kwenye vyombo vya habari vya nyumbani na hata vile vya kimataifa, wanavyopitisha miaka katika mazingira ya mlundikano, na hali zisizo za kibinadamu wakati wanaposubiri hukumu zao. Yeye aliandika akisema [uk] pale alipozungumzia utengenezaji wa filamu hiyo katika blogu yake Ukrainska Pravda:

Mahabusu ya Lukyanivsky SIZO. Mahali ambapo watu wanahifadhiwa kama wanyama.

Gereza la Lukyanivska ni taasisi ya kuweka watu kizuizini. Kuwekwa katika vyumba vyake visivyo na mwanga wala si adhabu, bali ni hatua ya kutoa kinga tu. Ndiyo kusema, yeyote anayeshukiwa kwa lolote anaweza kutupwa ndani yake, na katika Ukraine ya sasa, haina maana kwamba mtu huyo lazima awe mhalifu wa kweli.

[Gereza la Lukyanivska] linashika nafasi ya kwanza katika ripoti za ukatili, unyama, hali mbaya kwa maisha ya binadamu na vifo visivyo na maelezo katika vyumba vya gereza hilo, na […] hapa ndipo ambao utawala wa [Rais Victor Yanukovych] umekuwa [ukiwaweka] maadui wake – na ndiyo sababu tulilifanya jambo la kuwaonyesha watu hali halisi ya Lukyanivka, kuwa lengo letu. Kuonyesha hali halisi, na si yale ambayo wao wanataka kutuonyesha tena kupitia vyombo vya habari wanavyovichagua wenyewe.

Tuliunda mtandao wa wapelelezi wetu ndani ya gereza, ili kuhakikisha tuna watu wetu kwenye kila jengo, katika kila ghorofa kwenye mahabusu ya SIZO katika muda mfupi. Kutoka [uraiani], [tulipenyeza] simu zenye uwezo wa kuchukua picha za video ili ziwafikie wapelelezi wetu, na mahabusu hao walitupatia vidokezo (kwa njia ya video) vya maisha yao, na polepole, kila video ikiwa na urefu wa sekunde 10 hadi 15, kwa kipindi cha miezi sita. […]

Usov amekuwa akipokea picha hizo alizotengenezea filamu iliyo kwenye blogu yake Ukrainska Pravda, na vilevile katika Facebook, Twita, YouTube na penginepo.

Watu wengi wanamsifu Usov kwa ujasiri wake. Kwenye YouTube, mtumiaji anayejiita slafkorood aliandika [uk]:

Ninaweza tu kufikiri kazi kubwa ambayo Usov na timu yake [kutengeneza filamu hii] walifanya, kazi yake hii haitapita bure, yeye ni mtu jasiri, walau tu tungekuwa na watu wengi zaidi kama yeye.

Watu wengi wana wasiwasi juu ya usalama wa mwandishi huyu wa habari. Kwenye Facebook, Roman Plechun aliandika [uk]:

Kostiantyn, je, huogopi kwamba “utawala” utaanza kukufuatilia? Ningependa tu kufahamu ulipata wapi ujasiri ili kufanya kazi hiyo!?

Mtumiaji wa YouTube anayejiita BenderZT aliandika hivi [ru] kuhusu yale yatakayotokana na filamu hiyo:

Kuna msemo mzuri katika hitimisho [la filamu yenyewe], kwamba [Gereza la Lukyanivska] ni picha ndogo tu inayoonyesha hali halisi ilivyo katika nchi nzima. Ni jambo la kuhuzunisha kutokana na ukweli huu…

Mtumiaji wa Facebook anayeitwa Yevgeny Titorchuk aliandika [ru]:

[…] Ni filamu inayotia huzuni sana kuitazama na kuona maovu na kupoteza maana kwa mfumo ambao haujali hata kidogo masuala ya utu. Na jambo la kutisha zaidi ni kwamba, mfumo huu umetengenezwa na kuendelezwa na binadamu wenywe.

Kuhusu blogu ya Usov Ukrainska Pravda, mtumiaji Facebook anayejiita Lyubomyr Drozdovskyy alijaribu kutoa ufafanuzi [uk] kuhusiana na ukatili unaoshtua wa maisha katika gereza la Lukyanivska kama yalivyoonyeshwa kwenye filamu:

Kusema ukweli, maslahi ya kifedha [wanayopata askari magereza] si sababu ya pekee kwa hali mbaya iliyo kwenye mahabusu ya SIZO. Sababu nyingine ya hali hiyo ya kutisha katika SIZO ni kutengeneza mazingira yasiyovumilika ili kwamba mtu anayewekwa humo pengine angebembeleza ili walau ahamishiwe [kwenye magereza ya kweli], ambapo hali zina unafuu fulani. Kwa mfano, kama kuna mtu mwenye kesi ambayo haina ushahidi wa maana ili kumpata na hatia, lakini [wakati huo huo watawala wanataka kuona kwamba anakutwa na hatia kwa ajili ya maslahi yao, mathalani kujipatia sifa kwa kesi ambazo zimepatiwa ufumbuzi]. Kwa hiyo, wanamsweka mtu katika mahabusu ya SIZO, na baada ya miezi michache ya kipindi cha mateso, [mtu huyo] anakuwa tayari hata kutoa maelezo ya kujikandamiza [mwenyewe], anatoa kauli inayomtia mwenyewe hatiani, anakiri kutenda jambo [asilolitenda] – ili tu apate fursa ya kuondoka kutoka kwenye mahabusu ya SIZO, hata kama ni kwenda kufungwa [gerezani].

Katika maoni mengine kwenye blogu ya Usov, Ukrainska Pravda, mtumiaji skilachi aliandika kwamba [uk]:

Karibu kila kitu kiko kama kilivyokuwa miaka nane iliyopita. Bado ninakumbuka kila moja ya siku 254 [nilizowekwa mle]. […] Baada ya kuachiwa kwangu huru, nilitamani: kwamba kila mfanyakazi wa siku za usoni wa [Wizara ya Mambo ya Ndani], ofisi ya mwendesha mashtaka, mahakama au taasisi yoyote inayohusina na kuweka watu rumande, basi “waonje” hata kwa miezi michache maisha ya kwenye taasisi hiyo kabla [kuanza kazi kama walinzi wa sheria na mfumo wa mahakama]. Pengine wangejifunza kutumia njia mbadala ya kuchukua hatua za kinga dhidi ya watuhumiwa. Lakini hii ni kama vile [kuota ndoto za Alinacha]. Kwa wale ambao wamewahi kuonja jehanamu hii, nawatakia nyote afya njema. Kwa wale watakaoshindwa kuepa kuingia humo, kumbukeni kujitahidi kubaki mkiwa na utu wenu.

Yaelekea kuna mwitikio kutoka kwenye mamlaka kuhusiana na filamu ya Usov. Idara ya Magereza ya Ukraine, hata hivyo, ilitoa tamko [uk] kupitia taarifa kwa vyombo vya habari mnamo tarehe 2 Aprili, inayosomeka kama “njia ya kupuuzia” ujumbe kama ule wa Usov:

Kyiv SIZO – taasisi yenye mvuto zaidi kwa vyombo vya habari

Katika siku za hivi karibuni, kumekuwa na taarifa, maoni na habari za hapa na pale zinazotolewa na vyombo vya habari kuhusiana na kazi za taasisi [za Idara ya Magereza]. Nyingi ya hizi ni maoni kuhusu hali, ambazo kwamo, wale watu waliokamatwa na wale wengine waliotiwa hatiani wanamoishi, na pia kuhusu vitendo vya wafanyakazi wa taasisi hizo.

Uchambuzi wa machapisho hayo [filamu] unaonyesha kukosa ujuzi na kutotimiza sharti la kupata maoni ya upande wa pili, na mara nyingine kupuuzia kabisa kwa taaluma ya habari na waandishi […]. Kwa sababu hii, [wawakilishi wa idara ya magereza] wanakana taarifa zote zilizotangazwa au kutolewa kama maoni ya ziada zinazoihusu. […]

Kuhusu picha zilizotolewa hivi karibuni kuhusu gereza la Lukyanivska katika ngazi ya kimataifa, LEvko wa Foreign Notes anaunganisha na habari hii iliyokuwa kwenye gazeti la Kyiv Post kuhusu mkutano uliofanyika tarehe 3 Aprili kati ya wawakilishi wa Freedom House na mmoja wa mahabusu wenye hadhi ya juu zaidi aliye SIZO, waziri wa zamani wa mambo ya ndani, Yuri Lutsenko. LEvko anaandika:

[…] Watu kutoka Freedom House waliomtembelea Yuriy Lutsenko gerezani siku ya Jumanne hawana budi kutazama video [ya Usov] … baada ya kutembelea gereza hilo: “Idara [ya Ukraine] ya Magereza na Mahabusu ilisisitiza kwamba wageni hao walisema kwamba Ukraine ilichukua hatua kuhakikisha kwamba hali katika mahabusu na magereza na zahanati zinazoshughulikia mahabusu zilikuwa zikienda sambamba na viwango vya kimataifa.”

Washe***i na waongo wakubwa ninyi…

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.