Habari kuhusu Haki za Binadamu kutoka Aprili, 2013
Irani: Je, Dola Inamwogopa Msichana wa Miaka 13?
Kuwapiga watu marufuku kusafiri nje ya nchi yamekuwa mazoea ya serikali ya Irani kwa makusudi ya kuwaghasi wanaharakati wa asasi za kisiasa na zile za kiraia kwa miaka mingi. Lakini, mahakama ya usalama iliwasha moto upya kwa kumpiga marufuku kusafiri nje ya nchi mume wa mwanasheria wa haki za binadamu aliyefungwa Nasrin Sotoudeh pamoja na binti yao mwenye umri wa miaka kumi na mitatu, Mehraveh Khandan. Nasrin Stoudeh amehukumiwa miaka kumi na moja gerezani.
Serikali ya Bangladeshi Yawafuatilia Wanablogu, Yawatuhumu Kuukashfu Uislam.
Kadri mapambano makali kati ya wanaharakati wa Kiislamu na serikali yanavyoendelea kusababisha migongano ya kidini nchini Bangladesh, Mamlaka ya Mawasiliano ya nchi hiyo imechukua hatua ya kuwanyamazisha wanablogu wanaoonekana wapinzani wa Uislamu na serikali. Asif mshindi wa tuzo ya mwanablogu bora amekuwa akilengwa na hatua hizo kwa siku za hivi karibuni.
Uturuki: Polisi Watumia Mabomu ya Machozi Kuwatawanya AkinaMama Waandamanaji
Wafungwa wa kisiasa wa Kikurdi wamefikia siku yao ya 55 ya mgomo wa kula. Kuna mamia ya wafungwa wa kisiasa walio kwenye mgomo wa kula nchini Uturuki, na hii imesababisha maandamano mshikamano katika bara la Ulaya, na hususani ndani ya Uturuki. Mapema jana [4 Novemba 2012], wanawake ambao ni mama wa baadhi ya wafungwa wa kisiasa walifanya maandamano ya kukaa, na walijikuta wakipambana na mabomu ya machozi, pamoja na kunyunyuziwa maji ya kuwasha. Wa- Kurdi duniani kote wanapinga kimya kinachotumika kushughulikia adha yao.
Asasi za Kiraia za Urusi “Zakaguliwa” na Mwendesha Mashitaka
Wanaharakati wa DemVybor katika jiji kuu la eneo la Voronezh waliripoti kwenye blogu ya DemVybor[ru] kwamba Asasi Zisizo ki-Serikali zinakaguliwa na ofisi ya mwendesha mashitaka wa umma wa jiji hilo. Mashirika...
Bahrain: ‘Kususia michezo ya Olimpiki’
Wa-Bahraini wengi wanatoa mwito wa kususuia michezo ya Olympics. Kwanza, mwana wa mfalme, ambaye amekuwa akituhumiwa kwa kujihusisha na utesaji wa wanariadha, anahudhuria michezo hiyo. Pili, sehemu kubwa ya timu ya nchi hiyo imetengenezwa na wanariadha wa ki-Afrika.