Irani: Je, Dola Inamwogopa Msichana wa Miaka 13?

Makala haya yamechapishwa kwa kuchelewa kutokana na sababu zisizozuilika.

Kuwapiga watu marufuku kusafiri nje ya nchi yamekuwa mazoea ya serikali ya Irani  kwa makusudi ya kuwaghasi wanaharakati wa asasi za kisiasa na zile za kiraia kwa miaka mingi. Lakini, mahakama ya usalama iliwasha moto upya kwa  kumpiga marufuku kusafiri nje ya nchi mume wa mwanasheria wa haki za binadamu aliyefungwa Nasrin Sotoudeh pamoja na binti yao mwenye umri wa miaka kumi na mitatu, Mehraveh Khandan. Nasrin Stoudeh amehukumiwa miaka kumi na moja gerezani.

Ensiloos aliandika [fa]:

Baba yake Mehraveh anasema kupitia ukurasa wake wa facebook kwamba hata kama binti yake, Mehraveh, alitenda kosa la jinai, angefikishwa mbele ya mahakama ya watoto wala sio kuswekwa jela la Evin.

Haghemoslamema anasema [fa]:

Lazima tuihuishe “kampeni ya kutetea watoto wasio na hatia” kuujulisha ulimwengu mzima ufahamu kuhusiana na utawala wa kiislamu [Utawala wa Irani]. Mwanablogu huyo anauliza kwa hasira kosa hasa la Mehraveh ni lipi:  Ni kule kuwa mtoto wa Nasrim Stoudeh, ni kule kuwa mtoto wa miaka 13, je ni kuwapenda wazazi wake, kumtunza kakaye mdogo…kiukweli ni Ali Khamenei mwenyewe anayeweza kujua kosa la huyu msichana…tusikatishwe tamaa na kesi hii ya Mehraveh, vinginevyo, wafungwa wote wa kisiasa watapelekwa katika gereza la Evin.

Mwanablogu huyo pia alichapisha picha ya Mehraveh akiwa na kakake:

Mehraveh Khandan and her brother. Image from haghmosalamma.blogspot.ca.

Mehraveh Khandan na kaka yake. Picha kutoka kwa haghmosalamma.blogspot.ca.

GreenCity aliandika [fa] mnamo Julai 8, 2012 kuwa Mkuu wa Halmashauri Kuu la Irani la Haki za Binadamu, Javad Larijani, alikanusha hadharani kuwepo kwa wafungwa wa kisiasa nchini Irani. Hivi leo, Jumatatu 16, Julai, kesi ya Mehraveh imemuumbua.

Jomhouriat aliandika [fa], “nchi yangu inajivunia msichana huyu asiye na hatia, ambaye kupigwa kwake marufuku kusafiri kwake kunaonesha jinsi Jamuhuri ya Kiislamu [Iran] inavyoporomoka.”

Sio mara ya kwanza watoto wa Nasrin wameoonyesha maumivu wanayokumbana nayo familia za wafungwa wa kisiasa. Kadri ya mwezi mmoja uliopita, watumiaji wa mtandao wa kijamii wa Irani waliweka video ifuatayo ikimwonyesha Nasrin Sotoudeh akijaribu kucheza na  mwanawe wa kiume wa miaka minne kupitia dirishani walipomtembelea akiwa jela.

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.