· Januari, 2013

Habari kuhusu Haki za Binadamu kutoka Januari, 2013

Mwanaharakati wa Pakistani Khudi Ali Auawa Katika Mlipuko wa Bomu

Mnamo Januari 10, 2013 katika jiji la Quetta lililopo Kaskazini Mashariki mwa nchi ya Pakistani, watu 82 walipoteza maisha kwenye milipuko ya mabomu yaliyolenga eneo ambalo kimsingi lenye idadi kubwa ya Waislamu wa Shia jamii ya Hazara. Irfan Khudi Ali, mwanaharakati mashuhuri wa haki za binadamu ambaye bila kuchoka aliweka wazi uonevu wa kikabila unaofanywa kwa waShia wa Hazara nchini Pakistan, alifariki katika shambulio lililofuata. Kifo chake kimechochea watu kumpa heshima kwa juhudi zake kwa kuanzisha tena maandamano kupinga mauaji ya watu wa Shia nchini Pakistani.

14 Januari 2013

Mashoga Washambuliwa Kaskazini mwa Kameruni

Oscarine Mbozo’a anaripoti [fr] katika blogu ya L'Actu kuwa shoga mmoja akiwa ameambatana na mwenzi wake walizomewa karibu na soko mnamo tarehe 6, Januari 2013, mjini Maroua, Kaskazini mwa Kameruni: Goche...

11 Januari 2013

Mwaka Mpya na Mienendo ya Zamani Nchini Bahrain

Wakati nchi mbalimbali ulimwenguni kote zikiukaribisha mwaka mpya kwa fataki na shamrashamra, serikali ya Bahraini iliandaa utaratibu wa aina yake kwa waandamanaji nchini humo. kwa bahati, watumiaji wa mtandao wa intaneti walikuwa tayari, kuonesha na kuweka kumbukumbu ya baadhi ya matukio kwa ajili ya kushuhudiwa na sehemu nyingine yote ya ulimwengu.

8 Januari 2013

Bangladeshi: Msichana Mwingine Mzawa Abakwa na Kisha Kuuliwa.

Kwa mara nyingine msichana mzawa ameuawa nchini Bangladesh baada ya kubakwa kikatili. Mhanga huyo, Khomaching Marma (14) alikuwa mwanafunzi wa darasa la nane. Ubakaji huu wa kikatili uliosababisha mauaji kwa mara nyingine tena umeamsha hasira na ghadhabu nchini kote. Watumiaji wa mtandao pia wanapinga vikali vitendo hivyo.

2 Januari 2013

Hakuna Usalama kwa Waandishi wa Kiraia Nchini Bahrain

Baada ya video ya "kibao" cha polisi wa Bahrain kusambaa sana mtandaoni, Waziri wa Mambo ya Ndani alitoa tamko akiomba kuwa yeyote aliyepiga picha tukio hilo aliripoti haraka kwa mamlaka zinazohusika. Siku mbili baadae, na kinyume na kauli hiyo, watu wengi walishangazwa na kukamatwa kwa mpiga picha.

1 Januari 2013