Habari kuhusu Haki za Binadamu kutoka Oktoba, 2012
India: Mgogoro wa Mtambo wa Nyuklia wa Kudankulam Waendelea.
Mradi wa Nguvu za Nyuklia mjini Koodankulam katika wilaya ya Tirunelveli iliyo katika Jimbo la kusini la Tamil Nadu nchini India umeanza kufanya kazi mwezi uliopita lakini maandamano ya kuupinga mradi huo umeendelea na kamata kamata inasababisha waandamanaji kuishia jela. Juma hili limeshuhudia maandamano yakienea India yote kwa ushirikiano na watu wanaopinga matumizi ya Mtambo wa Nyuklia.
DRC Kongo: Misuguano Kati ya Kinshasa na Paris Mkutano Unapoanza
Le Potentiel anaandika kwamba [fr] tathmini ya Uvunjaji wa Haki za Binadamu nchini DRC Kongo iliyofanywa na Rais wa Ufaransa Hollande haikuchukuliwa kijuu juu na serikali ya Kongo wakati ambapo...
Guatemala: Waandamanaji Wazawa 7 Wauawa Totonicapán
Raia wasiopungua 7 wameuawa, takribani watu 32 wamejeruhiwa na 35 walidhuriwa na sumu mnamo tarehe 4, Oktoba, 2012 wakati majeshi ya muungano yalipotumia nguvu kuwatawanya waandamanaji kutoka katika njia panda maarufu inayoeleka jiji la Guatemala City.