Mali: Kimya cha Wanablogu wa Nchini Humo

Wakati wananchi wa Mali wakiwa wanajiandaa na uchaguzi, walishangazwa na mapinduzi ya kijeshi mnamo 21, 2012 , na tishio la kujitenga kwa sehemu ya kaskazini ya nchi hiyo. Wakati wa mapinduzi hayo wagombea wakuu walikuwa wakisoma akaunti zao za Twita na Google+ pamoja na kurasa zao za Facebook, raia kwa upande mwingine walikuwa wakihuisha blogu zao pamoja kutuma ujumbe wa twita.

Wakati habari kutoka kaskazini zikipatikana kwa kiasi kidogo, kutokana na kukatika na kukosekana kwa umeme, Sehemu ya kusini mwa nchi hiyo huduma ya intaneti inawezesha watu kuhamasishana.

Kifaa cha kupokelea mtandao wa intaneti kikiwa nchini Mali kupitia @Mbokoniko kwenye twita

The ‘Collectif des Ressortissants du Nord’ (Umoja wa wananchi wa Kaskazini) au COREN una wanachama 303 katika kundi lao la Facebook wakati wa kuandika makala haya. Kwa majuma machache yaliyopita, COREN imeweza kuwahamasisha wananchi wa Mali kote ndani ya mipaka hiyo, kwa kutumia ukurasa unaonekana kutangaza matukio yanayofuata pamoja na kuonyesha mshikamano kama inavyoonyeshwa katika habari mpya iliyowekwa na mwanachama wa kundi hilo aitwaye Oumar Maigar:

Mettez le drapeau du Mali sur votre profil pour soutenir son unicité

Tumia bendera ya Mali kama picha ya utambulisho wako kuunga mkono umoja

Wakati mtandao wa intaneti umetawaliwa na blogu, ujumbe wa twita na video kutoka nchi mbalimbali, watumiaji wa intaneti wenyeji wa Mali wangali kimya. Mji mkuu, Bamako, umeathirika kwa kukatika kwa umeme kwa kile kinachodaiwa kuwa kuadimika kwa mafuta. Kufuatia hali hii, kipaumbele si kutuma ujumbe, ila kutafuta taarifa kuhusu viongozi wapya wa kaskazini.

Tovuti ya Tuareg iliendesha Vuguvugu la Ukombozi wa Taifa la Azawad, kwa kifupi MNLA, haiko hewani kwa takribani juma moja. (Angalizo: Tangu tarehe 10/04.2012 tovuti hiyo imerudi hewani kwa mara nyingine). Hata hivyo, vuguvugu hilo linaendelea kuweka video kwenye akaunti yake ya mtandao wa YouTube iitwayo Azawad17janv2012 [fr]. MNLA wameamua kujitangaza uhuru kupitia kituo cha televisheni ya Kifaransa, France 24. Tangazo hilo liliwashtusha wananchi wa Mali waliosambaza maoni ya hasira na kejeli kupitia mtandao wa intaneti, kama haya yafuatayo kwenye twita:

@Skante2: Propagande du MNLA, les médias devraient alors inviter tous les séparatistes du monde sur leur plateau. On verra l'embouteillage.”

Propaganda za MNLA, vyombo vya habari ni lazima katika hali hiyo viwakaribishe watu wanaounga mkono mpango huo wa kujitenga katika vituo vyao vya televisheni. Watapata watazamaji wengi.

Lakini kilichovutia hisia za watu ni picha za vuguvugu la ki-Islaam la Ansar Dine ambalo liliutwaa mji wa Timbuktu. Picha zilipigwa na AFP-Tele kwa sasa zimetazamwa mara 7,200 na zimejadiliwa kwa upana katika mitaa ya Bamako.[fr]

Wakati sintofahamu hiyo ikitawala mwenendo wa mambo Kaskazini mwa Nchi hiyo, baadhi ya watu wameweza hata hivyo kujitengenezea faida, kama inavyooneshwa na ujumbe huu wa mtumiaji wa twita aitwaye @flagsonline:

@flagsonline Punguzo la bei kwa Bendera za Azawad, kwa asilimia 20, namba ya vocha:az125115 Jinunulie sasa! #azawad #flag #vexillology

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.