Iran: ‘Marufuku Isiyo Rasmi ya Kutembea’ ya Tehran Wakati wa Mkutano wa NAM

Mkutano wa 16 wa Umoja wa Nchi Zisizofungamana na Upande Wowote ulianza mnamo tarehe 26 Agosti, 2012 jijini Tehran huku kukiwa na ulinzi mkali. Umoja huo madhubuti (NAM) unaoundwa na nchi ni mabaki ya mvutano uliokuwepo enzi za Vita Baridi kati ya Mashariki na Magharibi, na umoja huu unachukuliwa na Iran pamoja na mataifa mengine kama jukwaa mbadala kwa ajili ya kuendesha mijadala kuhusu masuala mbalimbali yanaoukabili ulimwengu hivi sasa.

Iran inasema kwamba imepanga mazungumzo kuhusu mpango wa amani wa kukomesha vita vya wenyewe kwa wenyewe vya nchini Syria, hata hivyo hakuna uwakilishi kutoka upande wa waasi utakaokuwepo kwenye mazungumzo hayo kwa sababu ya uhusiano wa karibu kati ya Tehran na utawala wa Bashar Assad, Rais wa Syria.

‘Marufuku ya kutotembea usiku isiyotangazwa’ ya serikali ya Tehran

Mkutano unafanyika kuanzia tarehe 26 hadi 31 Agosti jijini Tehran. Dola la Irani imelifunga jiji lake kuu kwa siku tano na imewatayarisha askari polisi wapatao 110,000 ili “kuhakikishia usalama Mkutano wa NAM.”

Logo for the XVI Summit of the Non-Aligned Movement. Source: IRNA. Public Domain.

Nembo ya Mkutano wa XVI wa Umoja wa Nchi Zisizofungamana na Upande Wowote. Chanzo: IRNA. Haki Huru za Umma.

Bonbast Akhtar anaandika:

kwa mujibu wa taarifa mbalimbali, kuna vizuizi kadhaa vya kiusalama jijini Tehran pamoja na kuwepo kwa ulinzi mkali kabisa. Ni kama vile kuna marufuku ya kutembea usiku lakini isiyotangazwa rasmi. Vikosi vya usalama pia vinakagua ndani ya magari mengi yanayopeleka watu mapumzikoni [Dola la Iran lilitangaza mapumziko ya siku tano wakati wa Mkutano wa NAM] Katika Barabara ya Chalous …waandamanaji mwaka 2009 [baada ya uchaguzi ulioelezwa kuwa na dosari nyingi wa rais] walividhalilisha vikosi vya usalama na kwa hiyo hivi sasa vikosi hiyo vinatka kudhirisha mamlaka na umuhimu wao.

Mwanablogu Sayeh Azadi alichapisha picha mbili kuhusu vikosi vya usalama na anaandika kuuliza kama ‘Umoja wa Ulaya na Marekani ziliwaorodhesha Basijs [kikosi maalumu cha jeshi cha kujitolea, aina ya wanamgambo] katika orodha ya magaidi, washenzi hawa wa utawala huu hawatathubutu kuwatishia watu.’

Maandamano ya kupinga utawala?

Suala la usalama siyo peke yake ambalo wanablogu wa Iran hujadili, kuna wanaoona kwamba kufanyika hapa kwa Mkutano wa NAM kunatoa fursa kwa watu kuandamana ili kupingia serikali iliyo madarakani.

Sabzarman anaandika [fa] uwepo wa maelfu ya wanahabari na wageni wa kimataifa ni fursa adimu kwa ajili ya Vuguvugu la Kijani kufanya sauti yake isikike ulimwengunni. Miongoni mwa mambo mengine, mwanablogu huyo anawaalika raia wa Iran kuandika miito mbalimbali katika lugha ya Kiingereza na kuweka rangi ya kijani kwenye mabango na kuta zilizo karibu na mahali Mkutano huo unapofanyika.

Kikudi cha wanafunzi na wanaharakati wa kisiasa walizindua kampeni ya Facebook wakimwalima Ban-Ki Moon, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa ambaye pia anashiriki kwenye Mkutano huu wa NAM, ili awatembelee viongozi wa upinzani waliotiwa nguvuni, Mir Hossein Mousavi na Mehdi Karroubi. Walichapisha barua hii ya wazi baadaye page:

Mh. Katibu Mkuu,
Mimi ni raia wa Iran, na kama mwana Iran mwenye uchungu na nchi hii, ningependa kukukaribisha kumtembelea Bw Mir Hussein Mousavi katika kipindi utakachokuwa hapa Tehran kwa ajili ya Mkutano wa 16 wa Umoja wa Nchi Zisizofungamana na Upande wowote (NAM). Bw Mousavi, ambaye ni kiongozi wa upinzani, hivi karibuni alilazwa hospitalini baada ya kupata matatizo ya moyo kufuatia miezi 15 ya kifungo cha nyumbani …Matamanio ya kidemokrasi na madai ya haki ya watu wa Iran yanastahili kuungwa mkono na jumuiya ya kimataifa, ikiwemo Umoja wa Mataifa na Katibu wake Mkuu. Kwa nafasi yako kama mamlaka ya kimataifa iliyoaminiwa na wajibu wa kulinda na kuhamasisha mikataba ya ulimwengu ya haki za binadamu zinakupa dhima ya pekee. Tunakutakia mafanikio katika kutekeleza kazi hii maalumu ya kihistoria.

Azadi Esteghlal Edalat anatoa wito [fa] kwa raia wa Iran ili waungane na kuwa kitu kimoja na kuugeuza Mkutano wa NAM kuwa wa kuutetemesha utawala wa nchi hiyo. Mwanablogu huyo anasema:

Mkutano wa NAM umetupatia nafasi ya pekee kabisa maalumu ya kuandamana dhidi ya maovu ya utawala na kuunga mkono Vuguvugu la Kijani. Ninatumaini watu watamiminika mitaani. Tufanye kila linalowezekana ili kuhakikisha tunafanikisha kuwa na maandamano.

Estade Mordan anasema [fa]:

Sielewi kwa nini hakuna anayejitokeza kufanya kitu. Mkutano huu ni fursa kubwa kufanya maandamano dhidi ya utawala. Je, tusubiri hadi lini ili atokee mtu wa kutufanyia kitu? Mousavi? Karrubi? Reza Pahlavi [mtoto wa mwisho wa Kiongozi wa Kidini wa Iran]? au Morsi sasa…Mimi kama mwanachama wa Vuguvugu la Kijani ninatoa mwito wa maandamano siku ya Alhamis tarehe 30 Agosti, 2012 kutoka eneo la Imam Hossein hadi Viwanja vya wazi vya Azadi, yaani kwa namna ile ile ambapo Mousavi alitoa wito kwetu kuandamana miaka mitatu iliyopita. Tuwafahamishe watu kupitia zana za vyombo vya habari vya kiraia na njia nyingine.

1 maoni

jiunge na Mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.