Guatemala: Kuvunja Milango ya Madanguro

Julio Roberto Prado ni mwanasheria wa Ki-Guatemala, ambaye mara nyingi anachunguza na kuendesha mashtaka yanayohusu usafirishaji binadamu, hasahasa, unyanyasaji wanaofanyiwa wanawake na watoto. Yeye anaandikwa kwenye blogu yake akitumia jina tofauti na la kwake, jambo ambalo linamsaidia kueleza kwa bayana zaidi undani wa mambo magumu yanayowakabili wahanga wa biashara hiyo ya usafirishaji binadamu. Makala yake ya siku za karibuni kwenye blogu yake Noticias Para Dios inaeleza baadhi ya mambo ya kuoana na sauti za kusikia katika kazi zake za kila siku [es], jambo lililomsukuma kuomba kutoka kwa jaji waranti ya kupekua katika madanguro. Makala yake pia inaonyesha ni kwa jinsi gani kufanya kazi katika mazingira yenye kusababisha msongo mkubwa wa mawazo na mazingira magumu kama hayo kunavyoweza kuathiri moyo wa kazi katika juhudi za kumaliza usafirishaji na unyanyasaji wa binadamu wengine.

Tenía puestos mis zapatos negros, vamos, todos saben que cuando los llevo es porque romperé alguna puerta. Ese día sería para rescatar a una niña de once años y a su hermana de quince de uno de los más grandes prostíbulos de la ciudad.

Nilivaa viatu vyangu vyeusi, hivyo ndivyo nilivyovaa, kila mmoja anajua kwamba ninapovivaa basi kuna mlango utakaovunjwa. Leo lengo ni kuwaokoa msichana mdogo mwenye umri wa miaka 11 na dada yake mwenye miaka 15 kutoka katika moja ya madanguro makubwa kabisa yaliyopo hapa jijini.

Hapa anatushirikisha mpango wake wa siku nzima akiwa pamoja na baadhi ya wanasheria wenzake wanaoshinikiza utii wa sheria:

A los hombres les gustan tiernas, dice uno de los policías. Me cuenta que el otro día fue hacia Retalhuleu una ciudad del interior del país. Allí entró a un sitio donde fue a rescatar a mujeres encadenadas en las camas, donde las obligaban a coger con los clientes. Estaban todas flacas, me dice. Me daban tanta tristeza, no comían, amarradas, con sus trajes típicos a los camastros. Pero qué se puede esperar de esos lugares, si hay algunos donde subastan vírgenes los primeros viernes de cada mes.

Unajua wanaume wanapenda sana wanawake wanapokuwa wangali vijana kabisa, anaeleza mmoja wa askari polisi. Ananieleza kwamba kuna siku alikwenda kwenye mji mmoja wa ndani unaoitwa Retalhuleu, ambako aliingia mahali alikolazimika kuwaokoa wanawake waliokuwa wamefungwa kwenye vitanda kwa minyororo, na walikuwa wakilazimishwa kufanya ngono na wateja. Wanawake wote hao walikuwa wamekonda, alinieleza. Walinihuzunisha sana, hawakuwa wakila chakula, walikuwa wamefungwa huku wamevaa mavazi maalumu kwa ajili ya kazi yao hiyo. Je, mtu ungetarajia nini katika maeneo kama hayo, wakati ambapo katika baadhi ya sehemu kulifanyika hata upigaji mnada wa mabinti bikira katika siku za Ijumaa za kila mwezi.

Ili kupata waranti hiyo ya upekuzi, Prado hana budi kupanga foleni ili kumwona jaji na kueleza hali ya mambo. Akiwa kwenye foleni, anajaribu kuchunguza yanayoendelea kuhusu baadhi ya wahanga waliokuwa pale na waliojikuta katika mazingira magumu:

Al llegar, una enorme fila de gente me espera. Me dispongo a aguardar por mi turno, para hablar con el juez y explicarle que necesitamos entrar al bar. Delante de mí, una señora luce todavía golpeada. Reparte su tiempo entre llorar y mecer a su hijo de brazos, mientras otra niña pequeña se prende de su pierna. Quisiera fumar. Quisiera encender un cigarro y apagármelo en el brazo izquierdo y despertar de una maldita vez.

Oigo que la mujer ha sido golpeada por su marido. Atrás siguen una muchacha con sus padres. La abusaron. Recuerdo que es fin de mes. Que acaba de pasar un fin de semana largo.

Ninapowasili, nakuta msululu mrefu ukinisubiri. Nasubiri zamu yangu ya kuzungumza na jaji na kueleza kwamba tunahitaji kuingia kwenye baa [kwa lengo la kuokoa watoto]. Mbele yangu yupo mwanamke mmoja anayeonekana kwamba alipigwa sana. Akiwa pale, alikuwa akilia na huku akimbembeleza mtoto wake mdogo wa kiume aliyekuwa amempakata, wakati huo huo binti mwingine mdogo alikuwa amejishika kwenye mguu wa mama huyo. Napata kiu ya kuvuta sigara. Nataka kuwasha sigara na kuizima kwenye mkono wangu wa kushoto ili kujiamsha mara moja.

Namsikia mwanamke yule aliyepigwa na mumewe. Nyuma yangu yupo msichana aliyesindikizwa na wazazi wake. Nakumbuka kwamba kumbe ni mwisho wa mwezi. Na ilikuwa ni wikiendi moja ndefu sana.

Simulizi hizi zimekuwa na athari yake juu ya mwanasheria huyu:

Permanezco sin hablar. Cuando trabajas con el dolor ajeno, te empiezas a vaciar por dentro. Le dejas espacio al dolor, le permites habitarte. A mí me llena el dolor de doce niños abusados y veintidós niñas prostituidas. Son los casos que llevo investigados con solución. Los otros no me habitan, me succionan.

Nabaki kimya. Unapokumbana na machungu yanayowakabili wenzako, unafika mahali unaanza kujisikia utupu ndani mwamo. Unabakiza nafasi kwa ajili ya uchungu wa wengine, unaruhusu uchungu huo kuishi ndani mwako. Nimejazwa uchungu wa watoto 12 waliotendewa vibaya na wasichana 22 walioingizwa kwenye ukahaba. Hivyo ndiyo visa ambavyo nimekuwa nikivitafiti ili kuvipatia ufumbuzi. Visa vingine haviishi ndani yangu, vinayanyonya maisha yangu.

Hatimaye, zamu yake ya kumwona jaji inafika ili kumwomba waranti ya upekuzi, anafanikiwa kuipata. Hata hivyo, anahuzunishwa na yale aliyoambiwa na jaji:

Me dice que me permitirá entrar.

Ya de pie, me despido y abro la puerta. Antes de salir, el juez me dice: “ese lugar es lindo, hay buenas muchachas allí. Si encuentra algún amigo mío dentro, ahí se lo encargo”. Se ríe.

Trato de sonreír pero más bien me sale una mueca de asco.

Ananieleza kwamba nitaruhusiwa kuingia [kwenye danguro hilo].

Nanyanyuka, namwambia kwa heri na naanza kufungua mlango ili kutoka. Kabla sijatoka kabisa, jaji ananiambia, “sehemu hiyo ni mahal pazuri, kuna wasichana moto sana pale. Kama utamwona rafiki yangu yeyote, tafadhali mtendee vema.” Kisha anacheka.

Najaribu kutabasamu badala yake sura yangu inakuwa kama ya mtu aliye na kinyaa.

Basi, wakati anatoka pale, picha nzima ya hali halisi inarudi kichwani mwake, hasa kuhusu visa vya aina hiyo:

Afuera, la señora golpeada, calma a su hijo de brazos y la muchacha abusada llora con su madre.

Es su turno de hablar con el juez. Les toca explicarle su dolor. Mientras que para mí, al salir a la calle, una invasión de aire, humo y ruido me recuerdan que es lunes. Un día cualquiera, que se repetirá hasta la saciedad.

Subo al auto y voy por las niñas. Sé que hoy tampoco podré dormir.

Pale nje, yule mwanamke aliyekuwa amepigwa vibaya, anajaribu kuwabembeleza watoto walio mikononi mwake, yule msichana aliyebakwa bado anaendelea kulia huku akiwa mikononi mwa mama yake.

Ni zamu yao kuzungumza na jaji na kumweleza machungu waliyopitia. Kwa upande wangu, wakati ninatoka nakuta maisha yakiendelea, upepo unavuma nje, moshi, na kelele zinanikumbusha kwamba leo ni Jumatatu. Siku nyingine yoyote hali hiyo ingejirudia mpaka mwisho.

Naingia kwenye gari na kuanza safari ya kwenda kuwaokoa wasichana wale. Najua kwa hakika kabisa kwamba usiku wa leo sitaweza kulala pia.

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.