Wanawake Wanaongoza Maandamano Nchini Sudan

“Hapana kwa udikteta na wala rushwa,” mchoro na Tibyan Albasha. Umetumika kwa ruhusa.

Tangu Disemba 2018, maandamano yaliyoanza kwa sababu ya ongezeko la bei ya mkate yamekuwa ya kitaifa yakiupinga uongozi wa Omar Al Bashir uliodumu karibu miongo mitatu.

Mwishowe, siku ya Alhamisi 11 Aprili 2019, Bashir alilazimishwa kujiuzulu.

Serikali ya Bashir ilitumia mbinu kandamizi kuzima maandamano hayo. Zaidi ya waandamanaji 40 wameuawa, mamia wakiwekwa vizuizini na kuteswa.

Pamoja na mashambulizi ya kikatili, wanawake hawakuwa nyuma kwa kujiweka imara katikati ya moyo wa maandamano hayo.

Waliongoza maandamano hayo wakiimba Zagrouda, namna ya ushangiliaji ambao hufanywa na wanawake katika ulimwengu wa Waarabu kuonesha furaha.

Wakati wa mwezi Machi, wanawake walivaa nguo nyeupe za kitamaduni,  thobe katika kuwaunga mkono waandamanaji na haki za wanawake. Majukwaa ya mitandao ya kijamii yalijaa picha za waandamanaji wa kike wakiwa wamevaa nguo nyeupe, wakitumia hashitagi #Maandamanomeupe (#مارس_الابيض)

Wanawake ambao huandamana mara nyingi hupambana na ukatili wa polisi. Mamlaka zimeshawafyatulia gesi za kutoa machozi na risasi za moto na walishawahi kuwatishia kuwabaka. Imeripotiwa wanawake wanapigwa, wanawekwa alama usoni na nywele zao kukatwa wakiwa ndani ya vituo vya mahabusu. Kila siku video mpya za wanawake wa Kisudani wakiwa wanapigwa na kudhalilishwa zimekuwa zikisambazwa katika mitandao ya jamii:

Lakini pia hashitagi hizo hizo zimekuwa zikitumika kuonesha ushujaa wa wanawake wa Sudan.

Wiki hii, picha na video kutoka kwenye maandamano imesambaa mitandaoni. Msichana wa miaka 22, mwanafunzi wa uhandisi anayeitwa Alaa Salah aliinua mkono wake wa kuume huku akiongoza umati wa watu kuimba “Thawra” (Kiarabu linamaanisha ‘Mapinduzi’). Video na picha zingeweza kuishia kuenea mtandoni lakini wanaharakati wa Sudani wameanza kumwita “Kandaka,” jina walilopewa malkia wa Wanubi wa Sudani ya kale.

Michoro iliyoshirikiswa katika mitandao ya kijamii imemgeuza Salah kuwa “Mnara wa Uhuru wa Sudan.”

Kutoka mtaani mpaka Runingani

Nyuma ya runinga, ni vikundi vya Facebook ambavyo vilishawahi kutawaliwa na mijadala kuhusu ndoa na michepuko, kwa sasa vinatumika kuonesha ukatili wa polisi. Wanawake katika makundi haya wametoa video na picha za mamlaka katili za ulinzi. Huwa Wakishatambulika, muhusika hupigwa na hufukuzwa nje ya mji. Athari za makundi haya imeonekana – maajenti wengi wa usalama kwa sasa wanaficha nyuso zao.

Mamlaka za Sudani zimejaribu kuzima mitandao ya kijamii nchini, lakini wanawake walivuka kikwazo hicho kwa kutumia (VPN) Virtual Private Networks, ambapo huficha eneo la mtumiaji.

Mapinduzi hayawezi kukamilika bila sanaa:

 

Pitia bandiko hili huko Instagram

 

Heri ya Siku ya wanawake… Kwa wanawake wote na wanamapinduzi popote walipo .. Shikilieni حركات نسوان ; )

Bandiko limeshirikishwa na Alaa Satir (@alaasatir) on

 

Wachoraji wa kike, wapiga picha na wanamuziki walitengeneza kazi za sanaa kupongeza waandamanaji mtaani. Walitumia sanaa kuenzi uvumilivu wa watu, hasa wanawake. Walitumia sanaa kutunza matukio na picha za wahanga na kuonesha uhalisia wa kuishi chini ya mamlaka kandamizi.

Wanawake wako mstari wa mbele, kushoto na ni kitovu cha mapinduzi. Wakati watu walipoanza maandaman, walikuwa kama wanasema ‘wanawake wanatakiwa kubaki nyumbani’. Lakini ilikuwa kama tumesema hapana ” alisena Islam Elbeiti mwanamuziki wa Jazz mwenye miaka 24.

Kupigania haki za wanawake Sudan

Machi 12 mahakama ya dharura ya Sudan ilikutana na msukosuko wa maandamano nje ya mahakama kutoka kwa familia za wanawake hao, na kuahirisha adhabu ya viboko kwa wanawake tisa ambao walikuwa wamehukumiwa viboko 20 na kifungo cha mwezi mmoja kwa kosa la kuandamana.

Kuchapwa viboko ni mojawapo ya adhabu hasa kwa wanawake huko Sudan, na hutolewa kwa makosa kama vile kuvaa nguo zisizo za heshima au uzinzi.

Mwaka 2014, mwanamke mmoja, alihukumiwa kifo kwa kosa la kuolewa na mwanaume asiye muislamu, kitendo kinachochukuliwa kama uzinzi. Mwaka 2015, mwanamke huyo alichapwa viboko 75 kwa kosa la kuolewa bila idhini ya baba yake.

Mwaka 2017, wanawake 24 walikamatwa kwa kosa la kuvaa suruali, ikiwa ni kinyume na sheria kali za Sharia.

Wakati mwingine ukatili huu huwa zaidi ya viboko: Wanawake wengi wa Sudan wamehukumiwa kifo kwa kupigwa mawe.

Kukingana na Reuters, Bashir aliitetea nafasi yake kwa kuikubali Sharia nchini Sudani mwaka 2011:

Tunataka tuwe na katiba ambayo inakidhi mahitaji yetu na wale wanaotuzunguka. Na mahitaji yetu yako wazi, katiba ya Kiislamu kwa asilimia 100% bila kuchanganya mambi ya ujamaa, au mambo ya dunia au umagharibi (ustaarabu)

Vifungu vya adhabu nchini Sudan ambavyo hutafsiriwa kutoka kwenye Sharia (Sheria ya Kiislamu) inaruhusu wasichana wenye miaka 10 kuolewa, na inasema kuwa mke kubakwa na mumewe haiwezi kuchukuliwa kuwa ni kosa.

Pamoja na hayo, wanawake wanakumbana na”sheria za maadili” ambazo zinawafunga na kuwakandamiza katika maisha yao ya kila siku.

Kwa sababu hizi, wanawake wa Sudan wako mstari wa mbele katika maandamano wakipigania mabadiliko.

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.