Wanaharakati Watafuta Majibu, Mwezi Mmoja Baada ya Uchunguzi wa Kifo cha Aliyekuwa Mwandishi wa Habari.

Ahmed Hussein-Suale Divela [Picha na: Kamati ya Kulinda Waanadishi wa Habari]

Mwezi mmoja baada ya ya kupigwa risasi akiwa kwenye gari yake huko Madina nchini Ghana, Ahmed Hussein-Suale Divela, Mgana aliyekuwa mwandishi wa habari za kiuchunguzi, wanaharakati wanahitaji majibu na maelezo ili kujua mazingira ya kifo chake cha kutisha.

Kikundi cha Maendeleo ya Umoja wa Waandishi wa Habari kilifanya matembezi ya mshikamano na amani katikati ya mwezi Februari mjini Accra kutoa ujumbe kwa jeshi la polisi kwamba wauaji wa Divela hawajajulikana na kushtakiwa. Wanasema matembezi hayo yataendelea hadi kikundi hicho kipate majibu.

Mauaji ya Divela yanatoa tahadhari kwa uhuru wa waandishi wa habari nchini Ghana ambapo mauaji ya kikatili ya waandishi wa habari ni nadra; hayo ni kutokana na Kamati ya Kulinda Waandishi wa Habari .

Hata hivyo, mhamasishaji wa kikundi, Kofi Asante anasema kwamba kikundi chake kina orodha ya “wanahabari 31 waliouliwa , Kumasi, baadhi yao waliuawa mwaka 2018 na imegeukia Ghana yenye sifa kuwa nchi ya kwanza Afrika katika kutoa uhuru wa habari na ya 23 ulimwenguni.”

Je, Ahmed Hussein-Suale Divela alikuwa ni nani?

Ahmed Hussein-Suale Divela alifanya kazi katika gazeti la Wakala wa uchunguzi wa habari za siri la Tiger eyes lililoongozwa na Anas Aremeyaw Anas. Mbinu yao isiyo ya kawaida katika kufanya uandishi wa habari za kiuchunguzi ziliiwezesha kuweka wazi habari za watu wazito na wenye wasifu mkubwa katika Afrika.

Hivi karibuni Divela alihusika katika habari ya kiuchunguzi ambayo iliweka wazi habari juu ya Rais wa zamani wa shirikisho la mpira la Ghana Kwesi Nyantakyi ambaye pia alikwa ni mjumbe wa Halmashauri kuu ya FIFA ya kutuhumiwa kupokea rushwa ya dola za kimarekani 65,000. Baraza la maamuzi la FIFA lilimuhukumu Nyantakyi Maisha kutojishughulisha na masuala yanahusu mpira wa miguu.

Anas alitangaza kuuawa kwa Divela kupitia twita ambayo iliambatana na video inayoonesha mjumbe wa bunge la Ghana Kennedy Agyapong akiongea mbashara kwenye runinga mwezi Mei 2018:

Mwezi September 2018, Divela aliiambia Kamati ya Kulinda Waandishi wa Habari kupitia WhatsApp kwamba baadhi ya “watu wenye nguvu katika nchi ya Ghna walikuwa wanamtafuta ili kumdhuru” baada ya sura yake kuonekana kwenye kituo cha runinga cha NET 2 TV mwezi Mei 2018 na Agyapong.

Tangu sura yangu ionekane na umma ulinichukia […] watu wengi wamejaribu [kunishambulia]. Vitendo hivi vya jinai juu yetu ni vya watu ambao […] wana nguvu katika Ghana na wanaweza kufanya lolote na kutokamatwa. Ni kweli, ilizungumzwa katika baadhi ya mitaa kwamba mtu yule yule ambaye alichapisha [sura yangu] alisema alikuwa anafanya lolote liwezekanalo aniue .

Maneno ya mbunge yana nguvu

Agyapong, ambaye ni mwanachama wa chama tawala kipya cha Wazalendo, amekuwa mbunge kwa miaka 19. Katika mapambano yake dhidi ya rushwa, Agyapong anajulikana kwa kutengeneza mashtaka ya rushwa dhidi ya wanasiasa ambao ni wala rushwa. — hasa wale wa ndani ya chama chake .

Mjadala ulipamba moto hasa kuhusu maoni ya Agyapong aliyoyatoa mbashara kwenye runinga kama ndiyo yamepelekea kuuawa kwa Divela:

Kijana huyo ni hatari sana. Anaishi hapa Madina. Kama ukikutana naye mahali, pasua masikio yake. Kama akitokea maeneo haya, nawaambia, mpigeni.

Agyapong alithibitisha matendo yake na alisema maoni yake hayakumaanisha kusababisha madhara wala mvutano. Divela aliyasema hayo akiwa na mfanyakazi anayefanya kazia na Agypong. Katika video nyingine , Agyapong anapendekeza kwamba Anas ni mshukiwa mkuu katika kifo cha Divela. Aliahidi kulipa zawadi ya fedha ya Ghana ipatayo 100,000 (about sawa na US dollars) kwa yeyote ambaye atakayewapata wauwaji wa Divela iwe uthibitisho kuwa hakushiriki katika mauaji yake.

Agyapong aliondoka Ghana baada ya jeshi la polisi kumhoji — alikanusha vikali kuwa haikimbii Ghana au hakuthibishwa kuwa mshukiwa.

Watu sita wamekamatwa na kuachiwa kwa dhamana kufuatia mauaji ya Divela. Jeshi la polisi lilieleza kuwekwa nguvuni kwa washukiwa kulikuwa kunazingatia “tuhuma za msingi”.” Hata hivyo, vitambulisho vyao, bado vimeshikiliwa.

Uandishi wa habari hatarishi

Wakala wa uchunguzi wa habari za siri Tiger Eyes limekuwa likipokea vitisho kwa miaka kadhaa na lilishtakiwa kwa kutumia mbinu ambazo zinavunja miiko ya uandishi wa habari.

Wakati hakuna Ushahidi wa kuonesha kumuunganisha Agyapong moja kwa moja na mauaji ya Divela, maneno yake yana nguvu na yaliongelewa kwenye kituo cha runinga na yeye mwenyewe.

Taarifa ya CPJ inadhihirisha kwamba mwaka 2018, waandishi wa habari wapatao 53 ulimwenguni waliuawa, “34 kati yao waliuawa kwa kuadhibiwa kutokana na kazi azo.” Kati ya mwaka 2016 na 2017, waandishi wa habari 102 waliuwa kutokana na matokeo ya kazi zao. Zaidi ya waandishi wa habari elfu moja waliuwa muongo uliopita (2006-2017) hii ni kutokana na taarifa ya UNESCO .

Kuuliwa kwa mwandishi mashuhuri wa Washington wa Makala, Jamal Ahmad Khashoggi kwenye ubalozi wa Saudi Arabia nchini Istanbul tarehe 2 mwezi Oktoba, 2018, na mawakala wa serikali ya Saudi iliibua hasira ulimwenguni kote.

Awil Dihar Salad, mwandishi wa habari mkongwe nchini Somalia, aliuawa mwezi Disemba, 2018. Salad alikimbia Somalia mwaka 2005, akiogopa kuuwa, lakini baadaye aliporudi aliuwa.

Mapema mwezi Julai 2018, waandishi wa habari watatu wa Kirusi waliuwa katika Jamhuri ya Afrika ya kati wakati wa “shughuli za uchunguzi wa kikundi kilichoitwa Wagner, kikundi cha makadarasi wa jeshi wa kujitegemea .”

Kujihusisha na uandishi wa habari za kiuchunguzi inaweza kuwa kama kusaini kibali cha kifo. Serikali nyingi za kiafrika haziruhusu na huzuia hasa habari za namna hiyo zisichapishwe. Fikiria malipo ya chini sana ya waandishi wa habari, haina maana kwa waandishi wa habari wengi kuwa katika hatari hii kubwa.

Hata hivyo, kifo cha Divela hakitasahaulika ingawa kazi yake itaendelea kuishi. Waandishi wa habari na wanaharakati wataendelea kuwa na matembezi hadi ufumbuzi upatikane.

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.