Mamlaka za Iran Zawakamata ‘Watumiaji wa Instagram’ katika harakati za Kudhibiti Mitandao ya Kijamii

Picha ya shirika la utangazaji la Jamhuri ya Kiislam ya Irani (IRIB)ambayo ilitangaza kukiri kwa kulazimishwa kwa mahabusu ambao wanajulikana kama “watumiaji mashuhuri wa Instagram celebrities,” akiwemo Maedeh Hojabri mwenye umri wa miaka 18.

Habari hii iliandikwa na Mahsa Alimardani kwa ajili ya kifungu cha 19. Unaweza kuangalia habari halisi ya kifungu cha 19 hapa.

Wakati Maedeh Hojabri, Elnar Ghasemi, Shadab Shakib na Kami Yousefi ambao ni wairani na watumiaji mashuhuri wa Instagram walipokamatwa mwezi Mei 2018, ilionesha awamu mpya ya juhudi ya serikali katika kudhibiti mazungumzo kupitia mtandao wa Instagram.

Kamata hiyo ya watumiaji mashuhuri wa Instagram ilizua kelele duniani baada ya serikali kulazimisha Hojabri mwenye umri wa miaka 18 kukiri kutenda “kosa” kwa kutuma video zinazoonesha alivyokuwa akicheza dansi.

Wasiwasi umekuwa ukiongezeka kwa watumiaji wa Instagram tangu mwaka 2018 pale waandamaji waliposambaa nchi nzima na mamlaka za Irani kwa muda mfupi zilifunga majukwaa ya mtandao wa Instagram na simu za mizani na mitandao hiyo ndiyo mitandao mashuhuri katika Irani.
Mwishoni mwa mwezi Aprili, simu za mezani zilifungwa kabisa. Badala ya kufunga jukwaa hilo, inaonekana kuwa mamlaka zimeendelea na kuutumia kufuatilia kile wanachokifanya wairani na kudhibiti maudhui katika mtandao wa Instagram na kuwakamata wale ambao hawafuate sheria za nchi.
Mwezi Julai 2018, mahakama ilianza kutisha mtandao wa Instagram kwa kuionesha kuwa kuna “shughuli haramu” za wanaoitwa watumiaji mashuhuri wa Instagram.

Nini kilitokea kwa Maedeh Hojabri

Tangu mwezi Mei, Hojabri alikuwa hatumii mitandao ya kijamii – lakini majariwa yake yalikuwa hayajulikani hadi tarehe 9 Julai wakati shirika la utangazaji la Jamhuri ya Kiislamu Irani (IRIB) lilipoweka hewani video ya kurazimishwa kukiri ambayo ilijuimusha baadhi ya watumiaji wa Instagram waliowekwa kizuizini, akiwepo Hojabri.

Ingawa video hizi hazikuoneshwa hadi Julai, inaonekana mahabusu hao walilazishwa kukiri kwao muda mfupi baada ya kukamatwa. Mahabusu mwanamme aliyejukana kama Kami Yousefi inaonekana kuwa ni mwezi Juni alipokiri. Kuna muda mtu aliyekuwa nyuma ya kamera anamuuliza mahabusu wa kike kama familia yake ilikuwa inajua kama amekamatwa. Alijibu kwa kuiambia kamera: “walifahamu pindi walipokuja nyumbani kwetu asubuhi hii kunikamata.”

kivuli cha picha ya Maedeh Hojabri akilia na kukiri kwenye kituo cha utangazaji cha Taifa kutuma kupitia mtandao wa Instagram video yake ikionesha akidansi.

Tarehe 3 Julai 2018, makamu wa mwendesha mashtaka Jenerali Hajatoleslam Mohamad Mosadegh alionesha kwa wakala wa habari nchini Irani kuwa kumekuwepo na “shughuli chini ya watumiaji mashuhuri kwa kujinufaisha kwenye ulimwengu wa mtandao na kulaghai.” Makamu huyo alisema kwamba kwa sababu ya umuhimu huu Ofisi ya mwendesha mashtaka ilibidi “ikate mikono ya hawa watu [katika Instagram]na kurejesha imani kwa jamii.”

Hakuna mashtaka yaliyoripotiwa rasmi juu ya mahabusu. Hata hivyo siku wanatangaza,Touraj Kazemi ambaye ni mkuu wa idara(inayojulikana kama FATA) ya kutdhibiti uhalifu mtandaoni mjini Tehrani , , aliiambia wakala habari za wafanyakazi Irani (ILNA) kwamba viongozi wa kurasa katika Instagram zenye “jinai ” mbalimbali wamewekwa kizuizini hasa Tehran, na kwamba “hatua stahili” zilikuwa zinachukuliwa. Kazemi alioneha kuwa kamata kamata hii inawalenga “watumiaji mashuhuri mbalimbali wa kurasa za Instagram”. Mtaalamu wa saikolojia Dr. Hagh Ranjbar alihojiwa na IRIB katika taarifa yao ya tarehe 9 mwezi Julai ,alihusisha suala hili kama “maovu ya jamii za watumiaji mashuhuri wa kursa za Instaragram ambao wanajaribu kujiimarisha wenyewe.”

Video iliyoandaliwa na IRIB yakamatwa Uajemi .

Kutokana na kifungu cha 638 cha sheria ya kanuni ya adhabu ya kiislamu nchini Irani , kucheza dansi kunafikiriwa kuwa “tendo la dhambi” na adhabu yake ni miaka miwili na viboko 74 (hapa chini waweza pitia maelezo kamili ya sheria ya 638). Pia mashtakacharges yalitolewa mwezi Mei 2014 dhidi ya baadhi ya wairani ambao walitengeza na kushiriki kutuma video ya vichekesho juu ya wimbo wa “Happy” wa Pharrell Williams kwenye mindao ya kijamii.

Pamoja na mchakato huo, vitendo vya ukiukaji vinaendelea

Kulazimishwa kukiri kunachangia kwenye suala la muda mrefu juu la ukiukwaji kutokana na mchakato wa mfumo wa mahakama ya nchi na matumizi ya mfumo wa utangazaji wa nchi kukuza taarifa za seriali juu ya watetezi wa haki za binadamu, waandishi wa habari, wanataaluma na watumiaji wa mitandao ya kijamii. Siku zilizopita matangazo ya IRIB yamekuwa yakitumika kukuza nadharia za njama dhidi ya raia wenye uaraia wa nchi mbili Nazanin Zaghari Ratcliffe na Seyed Kavous-Emami.

Katika ripoti ya mwaka 2014 ya kituo cha hali za binadamu katika Irani ilionesha jinsi ”kukiri” kwa kulazimishwa mara nyingi umekuwa ukitolewa kwa mateso ya vitisho na kisha kutangazwa na IRIB ambacho ni chombo cha habari kinachoongozwa na serikali kuthibitisha mashtaka yaliyofanywa kisiasa.

Tangu Desemba wairani wamekuwa wakikumbana na vikwazo katika kupata mitandao na kuingia katika mazungumzo mtandaoni , mawasiliano ya nchi za nje, kudhibitiwa kwa jukwaa la kutumiana ujumbe ambao hutumiwa na watu wengi na watumiaji wengi wa mitandao ya kijamii kukamatwa, waandishi wa habari, wanaharakati na wateteaji wa haki za binadamu.

Katika mrejesho kwa taarifa ya mahakama kwamba Instagram ingeondolewa, waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia alitwiiti kwamba hizo ni habari za uvumi. Badala yake alisema kuna mawazo juu ya kurudishwa kwa Twitter ambayo imefungiwa tangu mwaka 2009.

Suala ambalo limekuwa likifuatiliwa la kuondolewa kwa mitandao mbalimbali ya kutoa huduma sio geni. Kurudishwa kwa mtandao wa Twitter lipo katika mchakato wa kujadiliwa katika kikao kijacho cha kuangalia maudhui yasiyofaa. Kilicho kipya ni mjadala wa habari hii ya uongo kutoka chombo cha habari fulani kinachoharibu maoni ya umma kutoka kwenye suala la uwazi juu ya jambo la kushuka thamani kwa fedha .

Taarifa kama hiyo ilitolewa na waziri huyu wiki kadhaa zilizopita kabla ya mahakama kufunga na kuzuia matumizi ya simu mwishoni mwa mwezi April.
Kiukweli, uongozi wa Rouhani kwa muda mrefu umekuwa ukizungumzia suala la uhuru wa mitandao lakini sasa matukio ya hivi karibuni yamefanya ahadi hii kuonekana kupotea.

Bahari zaidi

Kifungu cha 638 cha kanuni ya makosa kiislam nchini Iran:

Mtu yeyote akitenda tendo baya (dhambi) barabarani na maeneo ya umma, adhabu itakayotolewa kwa kosa hilo, itakuwa kufungwa jela miezi miwili au viboko hadi 74; na kama watafanya kosa ambalo sio la kuadhibiwa lakini linakiuka maadili ya jamii, watahukumiwa siku kumi hadi miezi miwili jela au viboko hadi 74.
Muhimu – wanawake ambao wataonekana barabarani na maeneo ya umma bila kuvaa hijab ya kiislamu, watafungwa siku kumi hadi miezi miwili jela au faini ya Ria elfu hamsini hadi mia tano.

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.