Namna Utoaji Bure wa Kifungua Kinywa Nchini Yemen Ulivyorudisha Wasichana 500 Shuleni

Wanafunzi wakipata kifungua kinywa shuleni. Picha na Faten kwa ajili ya Solidarios sin Fronteras. Imetumika kwa ruhusa..

Pamoja na ukosefu mkubwa wa rasimali unaosababishwa na vita nchini Yemeni, familia nyingi zinalazimika kuondoa watoto wao shuleni. Mara nyingi wasichana wanapelekwa kuolewa wakiwa na umri mdogo wa miaka13. Lakini shule moja katika mji mkuu Sana’a ilipata njia kama tiba ya tatizo hilo.

Shirika lilisilo la kiserikali Solidarios sin Fronteras (lenye makao yake Hispania na Yemeni) kwa kiasi kikubwa linaendeshwa na wasamalia na hufadhiriwa na michango ya watu — wengine wakichangia kiasi kidogo kama euro moja kwa mwezi—, shirika hilo limeanza kutoa kifungua kinywa kwenye shule za wasichana ambao wana umri wa miaka kuanzia sita hadi kumi na sita. Kabla ya mradi huo kuanza, moja ya tano ya wasichana hao wamekuwa hawahudhurii masomo. Kidogo kidogo, wasichana hao walianza kurudi shuleni, na tangu septemba 2018, wanafunzi wote 525 wanaendelea kuhudhuria madasani. Mwanzilishi wa Salidarios alisema.

Nimeongea kupitia Whatsapp na Eva ambaye miaka mingi iliyopita nilikutana naye katika mji wa Barcelona na Faten ambaye yupo Yemeni hawa niwaanzilishi wawili wa shirika hilo. Waliniambia namna mradi wao wa “kifungua kinywa kwa ajili ya kulinda na kuelimisha “ ulivyoanza. Pia, waliniomba kutotaja majina yao kamili na jina la shule kwa sababu za usalama.

Mwezi Machi, 2018, mmoja wa walimu wa shule hiyo alimwendea Faten na kumweleza juu ya mwanafunzi wa kike ambaye kipindi cha mchana alikuwa akionekana kudhoofika na kuchoka sana. Ghafla, aliacha kuhudhuria shuleni. Hakuwa msichana wa kwanza kuacha shule, ingawa alikuwa bado mdogo sana. Mwalimu huyo aliongea na familia ya yule binti. Familia ile ilikuwa haina fedha na ilikuwa imepata ofa ya kumuoza binti yao.

Wakati akiongea na Faten, Mwalimu yule alionesha matumaini juu ya utoaji wa chakula kila siku shuleni unaweza kumotisha familia kuwaacha binti zao kuendelea na shule. Faten anasema, hapo ndipo wazo lilipoibuka:

Wengi wao [wa wasichana hawa] ni wa wafanyakazi wa kiwanda cha nguo, ambacho kiliharibiwa kabisa [na mabomu]. Familia za wafanyakazi hao hawajalipwa mishahara kwa miaka mitatu. Je, wanawezaje kulipa gharama za chakula? […] Kitu muhimu sana ni kwamba tunawasaidia ili wamalize elimu yao. Pia, familia zao zina furaha, kwani kuendelea kuwepo shuleni kunawazuia kukaa nyumbani au kuolewa wakiwa katika umri mdogo.

Mwezi Machi 2018, Umoja wa Mataifa ulitangaza kuwa mgogoro wa kijamii katika Yemeni ni mbaya sana ulimwenguni. Kuna tatizo la ukosefu wa ajira na mfumko wa bei upo juu, asilimia 80 ya familia nchini Yemeni zina madeni na asilimia 65 ni vigumu kununua chakula .

Solidarios sin Fronteras ilipata ushauri kutoka kwa mtaalamu wa watoto juu ya namna ya kuandaa kifungua kinywa. Faten hununua bidha za vyakula kila asubuhi na wanandoa hutumia jiko lake kuandaa, kujaza kwenye vifungashio na kusafirisha chakula. Wakati wa mapumziko ya dakika 45 kazini, huenda haraka shuleni kuwasaidia walimu kugawa chakula. Muda mwingine pia, ndugu zake huja kumsaidia.

Huu moyo wa kufanya mwenyewe umesaidia taasisi kuendesha programu nyingine tatu. Pamoja na “Msaada wa chakula kwa familia ,” husambaza chakula kwa familia zilizo katika mazingira magumu katika mji wa Sanaa, Aden, Amran, Raydah, Hodeidah, Al Dorihimi na familia waliokimbia makazi yao kutoka Taiz”Maji kwa ajili ya Yameni ” hushughulikia hifadhi ya maji katika kambi za Amrani na Raydah kwa ya wakimbizi wa ndani na Kujenga tena Socotra” hutoa simenti kwa ajili ya kujenga tena nyumba na kuchimba visima katika kisiwa cha Socotra kilichoharibiwa na kimbunga mwaka 2015.

“Kuna nini kama tukifanya sisi wenyewe?”

Kifungua kinywa kilichoandaliwa kusambazwa shuleni kila siku asubuhi. Picha ilipigwa na Faten kwa ajili ya Solidarios sin Fronteras (Mshikamano usiokuwa na mipaka). Imetumiwa kwa ruhusa.

Mwaka 2012 Eva alikuwa na safari kuelekea Yemen ambapo alikutana na Faten. Akiwa katika mji wa Sanaa Eva alikuwa akiangalia sherehe ya kumbukumbuku ya kuzaliwa, msichana mwenye sherehe hiyo alimzawadia keki. Msichana huyo alikuwa Faten. Wakawa marafiki na tangu kipindi hicho wamekuwa wakitembeleana na mara ya mwisho ilikuwa 2015 wakati Eva aliposafiri kuelekea Sanaa. Faten anakumbuka:

Wiki chache baada ya vita kuanza, kama kawaida nilimuuliza Eva kupitia whatsApp, “tunaweza kusaidia chochote ?”. Akajibu kwamba atatafuta taasisi ya rafiki yake Noelia iliyoko Hispania, na mimi nitafute moja iliyopo hapa Yemen.

Eva ambaye ana uzoefu wa miaka 15 katika maedeleo ya kimataifa, hakuweza kupata taasisi zisizo za serikali anazoziamini zinazofanya kazi na jamii za Yemen. Kwa hiyo yeye na Faten pamoja na Noelia waliamua kuanzisha taasisi yao mwaka huo.

Wanawake hao watatu ni timu ya watendaji wanaojitolea na wanasaidiwa na wasamalia waaminifu kutoka katika nchi zao. Eva na Noelia ambao huishi Hispania hushughulikia upatikanaji wa vyanzo vya fedha: Hutumia mitandao ya kijamii , redio, magazeti ya vyombo vya habari na mihadhara kuelezea kazi yao ili kuvutia wachangiaji. Watu wengi huchangia kupitia mtandaoni na mfuko wa pamoja wa SSF kila mradi hujitegemea. Faten anahusika na kuratibu huduma zinazotolewa shuleni – mara nyingi nyumbani kwake. Wote watatu hutengeneza timu ya watendaji wakuu na hufanya shughuli zao katika taasisi isiyo ya kiserikali pamoja na kazi zao binafsi.

Mara kwa mara huwa wanatumiana picha , video, na zikiwa na taarifa mpya kwenye kurasa za mitandao ya kijamii juu ya SSF. Pia, husambaza maudhui yanayopanua uelewa kuhusu vita katika nchi ya Yemen, hasa hasa jukumu la Hispania na nchi nyingine ambazo husambaza silaha zinazosababisha migogoro katika nchi hiyo.

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.