Wakati Putin Akihubiri “Uhuru” na Maendeleo ya Teknolojia, Wataalamu Walalamikia Kupotea kwa Uhuru Mtandaoni

Katika hotuba yake ya mwaka kwa taifa, Vladimir Putin amewaahidi warusi mtandao wnye kasi zaidi na wakuaminika. wataalamu wanasema Kuwa hakika hautatolewa bure. // TASS/kremlin.ru under CC2.0

Februari 20, Vladimir Putin alihutubia bunge la urusi katika hotuba yake ya mwaka kwa taifa. Ameahidi uwekezaji mkubwa katika miradi ya kijamii na miundombinu hasa kwenye msingi wa teknolojia ya habari:

Уже в текущем году необходимо принять генеральную схему развития инфраструктуры цифровой экономики, включая сети телекоммуникаций, мощности по хранению и обработке данных. И здесь также нужно смотреть вперёд. Задача ближайших лет – организовать повсеместный доступ к высокоскоростному интернету, начать эксплуатацию систем связи пятого поколения, 5G.

Mwaka huu lazima tuwe na mpango madhubuti wa kuendeleza miundombinu ya kiuchumi ya kidigitali, ikiwemo mitandao ya simu, na utunzaji wa taarifa na kasi kubwa ya usambazaji. Hapa pia, tunapaswa kuangalia mbele. Kazi ya miaka michache ijayo ni kutoa upatikanaji wa mtandao wenye kasi kubwa kwa wote na kuanza kutumia mitandao ya simu yenye nguvu ya masafa ya 5G.

Yanaweza yakawa maendeleo mazuri ikiwa miundombinu ya mtandao imeimarishwa na kuhakikisha kwamba warusi wote wanatumia mtandao. Lakini maendeleo hayo yatapatikana katika Urusi kipindi cha udhibiti mkubwa wa habari mtandaoni

Mwezi wa Februari, taarifa mbili zilieleza kwamba uhuru mtandaoni umeendelea kuzorota sana . Hakika, inaonekana kuwa wakati Warusi wengi watakuwa na mtandao, utakuwa mtandao unaotawaliwa na masharti.

Utafiti mmoja uliofanywa na Agora, kikundi cha Haki za binadamu, kimeweka wazi njia mbalimbali ambazo mamlaka za Urusi zinazuia watumiaji binafsi, mitandao ya kijamii na vyombo vya habari mtandaoni. Agora inasema njia zaidi ambayo imekuwa ikitumika ni sheria na kanuni ambazo zinawalazimisha watoaji wa huduma za mtandao na wataalamu wakubwa wa mifumo ya mitandao kulinda na “kusimamia” maudhui mtandaoni kwa niaba ya serikali ya Urusi.

Zaidi ya mara moja, watoaji wa huduma za mtandao walilazimishwa kuzuia upatikanji wa tovuti za kuchapisha habari juu kesi mahakamani, au kuweka wazi rushwa serikalini. Katika kesi iliyohusu kigogo mkubwa watoa huduma walilazimika kuzuia upatikanaji wa tovuti ya Alexey Navalny, ambaye ni mwanaharakati mashuhuri wa upinzani na mpiga kampeni ya kuzuia rushwa. Ripoti ya Agora inasema:

Власти подготавливают почву для блокировки сервисов, которые считают основными катализаторами массовых протестов, пытаясь представить ее как требование соблюдать национальное законодательство. Делегирование полицейских и цензорских функций частным игрокам не только минимизирует ущерб репутации, но и, очевидно, более оправдано с точки зрения расходования ресурсов и эффективности контроля

Mamlaka zimeanzisha njia za kuzuia huduma mtandaoni ambazo wanaziona kama vichocheo vya maandamano ya watu wengi,inakuwa ni sharti la kufuata sheria za nchi wakati wanapotekeleza ukandamizaji huu. Kazi za kulinda na kudhibiti maudhui mtandaoni kufanywa na taasisi binafsi haipunguzi tu uhalibifu, bali pia huhakikisha uendeshaji na utumiaji mzuri.

Pia Agora inaona kuna ongezeko kubwa la vikwazo juu ya kutuma maudhui kwa mtu: jumla ya maudhui 662,842 yalidhibitiwa mwaka 2018, ukilinganisha na maudhui 115,706 katika mwaka 2017. Hii ni pamoja na kufungiwa kwa tovuti, URL za watu binafsi, Makala mtandaoni, jumbe za mitandao ya kijamii zilizonekana kuwa na “msimamo mkali” au “uchochezi” n.k.

Mifano michache ya habari njema, ni ibara ya 282 (“Uchochezi wa chuki au uadui pamoja na kufedhehesha heshima ya mtu”) moja ya vipengele vibaya vya sheria za jinai Urusi, inahusika sana kwa mashtaka juu ya mazumngumzo mtandaoni, ilibadilishwa katika marekebisho yaliyofanyika mwezi Desemba 2018. Hii imefanya mashtaka yanayohusiana na mazungumzo mtandaoni kupungua. Hata hivyo, wataalamu wa sheria wana wasiwasi juu ya uwezekano wa kufanya sheria za Urusi kuwa ”huria”.

Taarifa ya Agora inatabiri kuwa waendesha mashitaka wa serikali wanaweza kubadili na kutumia ibara nyingine za jinai na uendeshaji ambazo sio kali sana kuwaadhibu wapinzani. Hii itawasaidia kuwafanya watumiaji binafsi na taasisi kukaa kimya bila kuchochea upinzani kutoka kwa umma.

Pia Agora inaona kwamba jukwaa la teknolojia ya habari la magharibi linaendelea kuridhia madai ya mamlaka za Urusi, mwenendo ambao huko nyuma Runet Echo aliuzungumzia. Ikitaja uwazi wa taarifa ya Google , Agora inasema kwamba mwezi Juni 2018 Google ilithibitisha kutendea kazi asilimia 79 ya maombi ya serikali ya kuondoa habari, wakati maombi kama hayo kutoka kwenye mamlaka za Marekeni ni asilimia 62 tu iliyofanyia kazi. Taarifa ya Google inaonesha kuwa maombi ya serikali ya Urusi ya kuondoa maudhui yaliongezeka maradufu kwa zaidi ya mara tano katika miezi sita katika mwaka wa 2016 kutoka 2,045 hadi 11,164 mwezi Desemba.

Pongezi kwa Google, kwa kutokubalina na maombi 94 ya serikali ya Urusi ambayo yaliainishwa kama “ukosoaji kwa serikali.” Pia Google hutoa baadhi ya mifano ya maudhui wanayoyaondoa, na sehemu muhimu ambayo ni hatarishi kwa umma: matangazo kwa ajili ya kamari haramu ambayo hufedhehesha watu waliochuma ruba (sarafu ya urusi) kwa taabu, propaganda mbaya ya ubaguzi, masoko ya madawa ya kulevya mtandaoni yanayouza madawa hatari, n.k..

Lakini Google walikubaliana na maombi ya kuondoa video za wanaharakati waliokuwa wakiitisha maandamano dhidi ya rushwa— kwa sababu maandamno haya yalitamkwa kiholela kuwa “yamezuiliwa” na kwa hiyo ni uvunjaji wa sheria ya katazo iliyolenga kukandamiza upinzani wa umma.

Twitter, Google and Facebook wote wameonesha nia ya kuondoa maudhui au kutopatikana kwa watumiaji wa Urusi kutokana na kupokea maombi kutoka kwenye mamlaka ya Urusi ili kutii sheria za nchi. Kuna dalili kidogo sana kampuni hayo kuangalia chanzo cha kizuizi kwa baadhi ya sheria hizi au hata kupima maombi haya dhidi ya katiba ya Urusi.

Taarifa nyingine iliyotolewa na jamii inayolinda mtandao (OZI) inaonesha giza nene katika utabiri wake: Ina kichwa cha habari “Mwaka Mpya usio na matumaini,” na inaonesha anguko kubwa na la muda mrefu la uhuru wa kutoa maoni mtandaoni tangu kuanza kwa vigezo mwaka 2016. OZI inaorodhesha matukio saba ambayo yaliadhiri uhuru wa kuongea mwezi Januari: kuanzia baadhi ya vifungu vipya vya sheria hadi mashauri ya kihistoria, kama vile mashtaka ya Yana Antonova, bigwa wa upasuaji wa Watoto wa Krasnodar, ambaye alishtakiwa kwa kutumiwa video na Open Russia, mtandao wa kijamii wa kiharakati uliotangazwa kuwa “taasisi isiyofaa.”

Kwa kuwa na mahusiano na “taasisi isiyofaa ” — pia orodha ya serikali inajumuisha taasisi ya majaliwa ya demokrasia ya taifa na msingi wa jamii iliyowazi — ni kosa linalostahili adhabu na sheria iliyoanzishwa 2015 ikiwa na adhabu mbalimbali, kuanzia faini kubwa hadi kifungo gerezani. Hata pia kutumiana video kupitia Facebook kunahesabiwa kama “kushirikiana na taasisi isiyofaa kama iliyomkumba Antonova.

Pia, taarifa ya OZI ilisistiza uharibifu mkubwa uliosababishwa na “muswada wa Klishas”, ambao uliletwa kama sehemu ya sheria zenye vizuizi ambazo sasa zinafanyiwa marekebisho na Bunge la Urusi. Ukiwa na jina la mwandishi aliyeuandika, Senator Andrey Klishas, muswada huo unalenga kujenga miundombinu “huru” kwa mtandao wa Urusi , hasa kuulinda usingiliwe na wageni. The other, Muswada wa ”kupambana na habari za uongo” nao uliandikwa na Klishas nao pia una utata sana na umelaumiwa karibu na wataalamu ulimwenguni kote. Hata hivyo miswada yote ilipitishwa iliposomwa kwa mara kwanza, shukrani kwa chama tawala cha Umoja wa Urusi kilizuia kutokana na kuwa na wabunge wengi katika bunge.

Inaonekana serikali ya Urusu inatumaini nguvu yake ya kudhibiti shughuli za mtandaoni-kiasi kwamba sasa inawahakikishia utoaji na upatikanaji wa mtandao kwa Warusi wote, bila kuhofia mabaya yanayoweza kutokea.

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.