Julai, 2013

Habari kutoka Julai, 2013

Mwandamanaji Amtaka Morsi Kuondoka Kwa Lugha ya Mafumbo

Maandamano makubwa ya kumtaka rais wa Misri Mohamed Morsi ajiuzulu yanaendelea nchini Misri kwa siku ya tatu sasa. Kwenye mtandao wa Twita, Assem Memon anaweka picha iliyopigwa kwenye maandamano: @AssemMemon: Bango la Maandamano. Neno ondoka limeandikwa katika lugha 14 za mafumbo. Picha imewekwa kwenye mtandao wa Twita na @ alaafareed pic.twitter.com/S7OOSDfpV6

Misri: Wasalafi Washambulia Makazi ya Washia, Wanne Wauawa

Watu wanne nchini Misri ambao ni wafuasi wa imani ya Shia wameuawa leo nchini Misri mara baada ya nyumba waliyokuwa wanakutania kushambuliwa na Waislam wenye msimamo mkali, shambulio hili linafuatia wiki mbili za uchochezi dhidi ya waumini wa Shia. Kwa mujibu wa taarifa za awali, nyumba ambayo waumini hao wa Shia waliyoitumia kukutania, iliyopo huko Giza, Cairo, ilishambuliwa na kuchomwa moto. Kwa mujibu wa taarifa za habari za Al Badil, shuhuda mmoja alikaririwa akisema kuwa mmoja wa watu waliouawa alichinjwa na wengine watatu walijeruhiwa vibaya vichwani mwao. Tukio hili la kutisha lilizua ghadhabu kubwa mtandaoni.

Kitu gani kinaifanya Brazil ifanane na Uturuki?

  1 Julai 2013

Nchi za Brazil na Uturuki zimetengwa na umbali wa maelfu ya kilomita, lakini zina kitu fulani cha kufanana: nchi zote mbili ziliingia mitaani kudai haki zao kama raia na sasa wanahangaika kujinasua na matumizi ya nguvu na unyanyasaji wa kupindukia unaofanywa na polisi. V rVinegar ni tovuti iliyotengenezwa kufuatilia maandamano na...