Nchi za Brazil na Uturuki zimetengwa na umbali wa maelfu ya kilomita, lakini zina kitu fulani cha kufanana: nchi zote mbili ziliingia mitaani kudai haki zao kama raia na sasa wanahangaika kujinasua na matumizi ya nguvu na unyanyasaji wa kupindukia unaofanywa na polisi.
V rVinegar ni tovuti iliyotengenezwa kufuatilia maandamano na kukuza uungwaji mkono wa matukio hayo katika nchi husika: nchini Brazil, kupinga uwepo wa polisi [pt], na kusitishwa mara moja kwa vurugu nchini Uturuki [tr]