Habari kutoka 12 Septemba 2008
Jordan: Ubloga wa Video wa Malkia Rania
Chombo cha habari cha Blogger Times kinachoendeshwa na mabloga wa Kiarabu, kimemtaja Malkia Rania wa Jordan kuwa bloga maarufu zaidi wa video za kutoka Uarabuni katika chombo cha Video mtandaoni, YouTube, kufuatia mafanikio ya mlolongo wa video za YouTube aliouanzisha kuondoa dhana potofu dhidi ya Waarabu.
Paraguai: Rais Lugo Kutopokea Mshahara
Utawala wa Rais Ferdinand Lugo umeanza na tangazo kuwa hatapokea mshahara wake wa mwezi. "Sihitaji mshahara huo, ambao unapaswa kumilikiwa na masikini," alisema Lugo. Mabloga nchini humo wanatofautiana mitazamo, wakati mmoja anausifu uamuzi huo, mwingine anajiuliza ni vipi Rais lugo atajilipia gharama binafsi za maisha.
Paraguai: Kuapishwa Kwa Lugo Kwenye Flickr
Rais wa paraguai alianza kutumia Flickr mnamo januari 2008 kama njia ya kuorodhesha nyendo zake wakati wa kampeni. Baada ya kuapishwa kama rais wa nchi siku ya tarehe 15 Agosti, anaendelea kutumia chombo hiki cha uandishi wa kijamii. Karibia picha 2,500 baadaye na zote chini ya haki miliki huria, Lugo anategemea kuwajumuisha WaParaguai nyumbani na ughaibuni katika urais wake.