Jordan: Ubloga wa Video wa Malkia Rania

Chombo cha habari cha Blogger Times kinachoendeshwa na mabloga wa Kiarabu, kimemtaja Malkia Rania wa Jordan kuwa bloga maarufu zaidi wa video za kutoka Uarabuni katika chombo cha Video mtandaoni, YouTube, kufuatia mafanikio ya mlolongo wa video za YouTube aliouanzisha kuondoa dhana potofu dhidi ya Waarabu.

Kwa mujibu wa makala hiyo:

Malkia Rania wa Jordan kaketi ndani ya ofisi yake kubwa huko Amman, jordan, na kamera tatu kubwa zikimuelekea. Kamera ya kwanza na ya pili zilikuwa kwa ajili ya BBC, wakati kamera ya tatu ilikuwa kwa ajili ya wafanyakazi wa ofisi yake. Kamera hizo tatu zilikuwa zikirekodi mapya katika mlolongo wa programu yake inayorushwa katika mkondo maalum kwenye YouTube, unaojulikana vyema kama Vlog. Hii ni video yake ya 7 tangu alipoanza kutangaza katika YouTube, mwezi wa Machi uliopita, ambamo anazungumza kwa Kiingereza akiwaomba watazamaji kujadili dhana ambazo wamezisikia kuhusu dunia ya Kiarabu, ili kwamba aweze “kuzipopotoa moja baada ya nyingine.”

Pengine mke wa Mfalme wa Jordan Abdullah wa Pili, si mtu maarufu pekee ambaye anatumia chombo cha YouTube, ambacho kinaangaliwa na mamilioni ya watu. Kuna wanasiasa na wafalme katika sehemu mbalimbali za dunia ambao wametengeneza tovuti binafsi katika mtandao wa intaneti.

Lakini jambo la kipekee kuhusu Malkia Rania ni kwamba yeye ni Muarabu pekee maarufu anayetumia mtandao wa intaneti kwa ajili ya mazungumzo na ulimwengu wa magharibi ili kutetea mtazamo wa wastani wa Kiislamu.

Malkia Rania ansema kwa utani: “Mwanangu wangu wa kiume aliye kwenye umri wa balehe ni mkimya ambaye huwa si muongeaji sana kwa asili yake, lakini mtazamo wake juu ya risala niliyotoa ulikuwa “vyema”, na kwa hivyo basi mtazamo wa wanaongalia pia unabidi uwe mzuri vilevile”. Inaonekana kwamba wageni wengi katika YouTube walikubaliana na alivyosema (mwanawe Malkia), kwani takribani watazamaji milioni 2 waliangalia mlolongo huo wa video uliorushwa katika YouTube; ambao ulijumisha pamoja na kanda zake mwenyewe, michango kutoka kwa wanamuziki, wachekeshaji na raia mbalimbali wa Jordan.

Makala hiyo inaendelea:

Kuonekana kwa Malkia Rania katika mkondo wake wa intaneti, kulimpa fursa ya kukosolewa kutoka kwa mamilioni ya watu. Kama alivyoniambia: “wakati wazo hili liliponijia kichwani, watu wengine waliniangalia kama vile nimerukwa na akili.” Akaendelea: “nadhani kwamba dunia yetu imo katika machafuko hivi sasa, vurugu zimechukua nafasi ya maongezi na hasira zimechukua nafasi ya huruma.”
“Natumaini kwamba mkondo huu utakuwa ni mkondo wa mawasiliano na daraja kati ya Mashariki na Magharibi, kwa sababu ninaamini kwamba dunia yetu inahitaji hili.”

Unaweza kumfuatilia Malkia Rania katika mkondo wake wa video.

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.