Habari kutoka Muhtasari wa Habari

Nini Tofauti ya Kusoma na Kuelimika?

  22 Aprili 2015

Pedro Muller anatafakari kuhusu matatizo yanayoukabili mfumo wa shule, taasisi anayosema ilimaanisha mazingira tofauti ya kihistoria. Kwa kusema hayo, anabainisha umuhimu wa dhana hizi mbili zinazofanana lakini zikimaanisha nyakati mbili tofauti: “Kusoma” na “kuelimika”: El educar se va más allá de memorizarse un par de nombres y olvidarlos al siguiente...

Umoja wa Ulaya Hautatoa Nafuu ya Kodi ya VAT kwa Vitabu ya Kidigitali

  20 Aprili 2015

Mnamo Machi 5, 2015, Mahakama ya Haki ya Umoja wa Ulaya ilitoa hukumu kwamba punguzo la kodi ya ongezeko la thamani (VAT) lililotolewa kwa vitabu vinavyochapishwa halitahusisha vitabu vya kidijitali, kwa kuzingatia kwamba kila kinachosambazwa au kutolewa kwa mfumo wa kieletroniki au kwa mtandao wa intaneti ni huduma. Amalia Lopez anahoji...

Mwizi Akamatwa, Aomba Msamaha na Kusamehewa

  19 Aprili 2015

Labda alidhani ingekuwa vyepesi kuiba shampoo mali ya mmiliki wa duka nchini Peru, lakini mambo yalimwendea mrama mwizi huyu. Mtu mmoja akiwa ameongozana na mwenzake waliingia kwenye duka lililoko kwenye jiji la Huancayo nchini Peru, wakisema walikuwa wanataka kununua pombe, na mmiliki alipokuwa amepumbazwa kidogo, jamaa walibeba boksi la shampoo....

Jiandae kwa Mkutano wa MozFest Afrika Mashariki 2015

MozFestEA ni tukio litakalofanyika kuanzia Julai 17 – 19, 2015 kwenye Chuo Kikuu cha Victoria, Kampala, Uganda likiwa na maudhui makuu, “Kutafuta Majibu ya Changamoto za Afrika, kwa pamoja mtandaoni”: MozFest Afrika Mashariki ni tukio la kila mwaka linalowaleta pamoja wataalam wa elmu, wabunifu, wasomi na mafundi wa Afrika Mashariki...

Shambulio la Kigaidi Laua Watu Watano Mjini Bamako

Shambuliko la kigaidi lilitekelezwa kwenye mgahawa jijini Bamako, makao makuu ya Mali, limechukua maisha ya watu watano usiku wa siku ya Ijumaa mnamo Machi, 6. Shambulio hilo lilifanyika usiku wa maneno kwenye mkahawa unaoitwa took Terrasse kwenye mitaa ya Bamako na watu zaidi ya kumi wamejeruhiwa vibaya. Washukuiwa wawili wamekamatwa...

Kuhusu habari zetu za Muhtasari wa Habari

Hizi ni habari mpya zilizoandikwa kwa muhtasari.