· Januari, 2013

Habari kutoka Muhtasari wa Habari kutoka Januari, 2013

Msumbiji: Uhamasishaji wa Kiraia Kuwasaidia Waathirika wa Mafuriko

sos chokwe

Baada ya mvua kubwa iliyosababisha mafuriko kusini mwa Msumbiji yaliyowaacha maelfu ya raia bila makazi na wengi kupoteza maisha, kikundi cha kiraia cha Msumbiji Makobo kimeanza kampeni ya mshikamano inayoitwa “S.O.S. Chókwè” kukusanya misaada ya hisani kwa ajili ya waathirika.

Mwandishi wa Kike wa Yemeni Asumbuliwa kwa “Kutokuheshimu Dini”

Samia Al-Agbhari

Samia Al-Agbhari..mwandishi wa Yemeni anakabiliwa na mashambulizi ya kipropaganda. Picha iliwekwa kwenye mtandao wa Facebook na Afra Nasser

(more…)

“Wanasemaje Bamako?” Mazungumzo na Awa anayeishi Mali

Mazungumzo ya kila siku kwa njia ya skype(kwa Kifaransa)  kati ya Awa Traoré aliyeko Bamako na Anne Morin akiwa Ufaransa (kupitia anuani ya @annagueye)

Anne Morin na Awa Traoré wanabadilishana mawazo kuhusiana na maisha ya kila siku mjini Bamako, ujira usiokidhi mahitaji, gharama za maisha na hali ya kisiasa isiyotabirika wakati huu ambapo vita vinanukia nchini humo.

Rais wa Chadi Awateua Wanawe Kushika Nafasi Nyeti

Djamil Ahmat anaripoti kuwa rais Déby wa Chadi amemteua mwanae wa kiume Mahamat Idriss Déby, 24, kuwa brigedia jenerali  [fr] pamoja na maafisa wengine wanne. Tchadanthopus anaongeza kuwa mwanae mwingine Zackaria Idriss Deby alisemekana kukabidhiwa umakamu wa rais [fr]  nafasi ambayo inampa madaraka yote wakati baba yake anapokuwa nje ya nchi.

Kuhusiana na Vuguvugu la Mabadiliko ya Umma

Gaurav Mishra anachambua nguvu ya vuguvugu la mabadiliko linaloanzia kwa watu wa kawaida na namna inavyofanya kazi kuleta mabadiliko chanya katika utendaji wa vyombo vikuu vya habari kwa kutumia vyombo vya habari vya kiraia.

Mauritania:Ghadhabu Dhidi ya Kauli ya Balozi wa Marekani

Picha ya maandamano dhidi ya Ubalozi wa Marekani mjini Nouakchott – Iliwekwa kwenye ukurasa wa Facebook ya Vijana wa Kukusanya Nguvu ya Kidemokrasia

(more…)

Jukwaa la Kiafrika Lenye Makala za Bure za Kitaaluma

Video inayoonesha namna www.hadithi.org inavyofanya kazi kuboresha upatikanaji wa zana za utafiti kwa Afrika

Januari 24, ni siku ambayo inategemewa kuwa ya kuzindua rasmi Hadithi, ambalo ni jukwaa la kuhifadhia zana za bure za kitaaluma mjini Nairobi, Kenya. Wasomi mbalimbali na wadau wa mitandao watakusanyika pamoja kujadili upatikanaji wa zana huru za kitaaluma katika elimu ya juu nchini Kenya. Hadithi itasaidia kutafuta, kuona na kushusha makala kutoka katika taasisi za kitafiti duniani kote. Kujiandikisha kwa tukio hili, itafute Hadithi mtandaoni kupitia Facebook na tovuti ya Eventbrite.

Mashoga Washambuliwa Kaskazini mwa Kameruni

Oscarine Mbozo’a anaripoti [fr] katika blogu ya L'Actu kuwa shoga mmoja akiwa ameambatana na mwenzi wake walizomewa karibu na soko mnamo tarehe 6, Januari 2013, mjini Maroua, Kaskazini mwa Kameruni:

Goche Lamine, mfanyabiashara wa madawa, alikamatwa na mwanafunzi wa shule ya sekondari aitwaye Sanda, mwenye umri wa miaka 17. Umati wa watu uliokuwepo sehemu hiyo baada ya kugutushwa na mtoto aliyekuwa akipiga kelele “samaroka! Samaroka (yaani mashoga katika lugha ya ki-Fulfulde), uliwakimbilia watu hao na kuanza kuwarushia mawe.

Watu 60 Wauawa kwa Msongamano nchini Abidjan

Magogo ya miti yaliyokuwa yameanguka barabarani yanaonekana kusababisha msongamano mkubwa na ulioua watu 60 na kujeruhi wengine 49 wakati wa sherehe za kuukaribisha mwaka mpya mjini Abidjan, Côte d'Ivoire. Kutokana na ukweli kuwa eneo hilo halikuwa na mwanga wa kutosha inawezekana ndio sababu iliyochangia tukio hilo la msongamano ulisababisha mkanyagano wa watu.

Israel Yoroba jijini Abidjan anaripoti kuhusu msongamano huo wa kutisha [fr] wakati watu wengi wakiwa wamekusanyika kusubiri kushuhudia milipuko ya fataki kuashirika mwaka mpya katika wilaya ya Plateau. Alama habari #drameplateau ilianzishwa kutoa nafasi ya kupatikana kwa habari za wakati huo huo kuhusu tukio hilo la kusikitisha na namna ya kuwasaidia waathirika. Hili nijanga la tatu la namna hii tangu mwaka 2009 [fr] nchini Côte d'Ivoire.