Unaona lugha zote hapo juu? Tunatafsiri habari za Global Voices kufanya habari za kidunia zimfikie kila mmoja.

· Machi, 2015

Habari kutoka Muhtasari wa Habari kutoka Machi, 2015

Makampuni ya Teknolojia Nchini Kenya Yaliyofadhiliwa Mwaka 2014

Je, unayajua makampuni ya teknolojia nchini Kenya yaliyopata ufadhili kwa mwaka 2014? Erik Hersmann anayaorodhesha kwenye blogu yake:

Fedha za mtaji wa awali

Angani – Huduma za mtandao wa umma wa kompyuta
BRCK – Huduma za mtandao wa Si-Waya za WiFi
CardPlanet – Mfumo wa malipo kwa njia ya simu za mkononi unaolenga biashara na AZISE
iProcure – Zana za kuongeza upatikanaji wa huduma vijijini
OkHi – Mfumo wa anuani za makazi kwa masuala ya manunuzi
Sendy – Huduma za pikipiki
Tumakaro – Mfuko wa elimu unaoendeshwa na raia waishio ughaibuni
Umati Capital – Huduma za vyama vya ushirika, wafanyabiashara na shughuli za viwanda
GoFinance – Mtaji kwa fedha za wasambazaji wa FMCG
BuyMore – Kadi ya punguzo ya elekroniki kwa wanafunzi
TotoHealth – Teknolojia ya ujumbe mfupi wa maandishi kwa afya ya watoto
BitPesa – Huduma ya malipo kwa ajili ya Waafrika

Shambulio la Kigaidi Laua Watu Watano Mjini Bamako

Screen capture of police forces in Bamako, Mali after the terrorist attack

Picha ya majeshi ya polisi mjini Bamako, Mali baada ya shambulio la kigaidi

Shambuliko la kigaidi lilitekelezwa kwenye mgahawa jijini Bamako, makao makuu ya Mali, limechukua maisha ya watu watano usiku wa siku ya Ijumaa mnamo Machi, 6. Shambulio hilo lilifanyika usiku wa maneno kwenye mkahawa unaoitwa took Terrasse kwenye mitaa ya Bamako na watu zaidi ya kumi wamejeruhiwa vibaya. Washukuiwa wawili wamekamatwa na wanaendelea kuhojiwa na vyombo vya ulinzi na usalama. Afisa wa polisi aliripoti kwamba watu   hao wawili walikuwa na silaha kali pamoja na mavazi ya kijeshi. Mtu mmoja alilipua bomu kwenye mkahawa. Raia wawili wa watatu, Mfaransa mmoja na raia mwingine wa Ubelgiji waliuawa. Mwanablogu mmoja aliweka video inayoonesha vikosi vya polisi waliokuwa wakifanya uchunguzi kwenye eneo la tukio:

Mchangiaji wa Global Voices Marc- André Boisvert aliandika kwenye mtandao wa twita kwamba shambulio kama hilo halikuwa linaepukika, kwa sababu Mali bado inajitahidi kurudisha hali ya amani kwenye ukanda huo wa Kaskazini:

Sote tulijua tukio hili lingetokea mjini Bamako. Sote tunajua shabaha ilikuwa kuwalenga wapiga kelele. Lakini bado tunashangazwa

Philippe Paoletta, mkazi wa Bamako, anakubaliana na Marc-André:

Kila moja alijua yaliyotokea yangetokea wakati fulani hapa Bamako. Hata hivyo hiyo haifanyi hali hiyo isiwe ya kushangaza. Mwenyezi Mungu aziweke pema roho za marehemu

 

Tunawatakia majeruhi wa shambulio kupona kwa haraka.