Unaona lugha zote hapo juu? Tunatafsiri habari za Global Voices kufanya habari za kidunia zimfikie kila mmoja.

· Mei, 2014

Habari kutoka Muhtasari wa Habari kutoka Mei, 2014

Je, Madaraka ni Matamu Kiasi cha Watawala wa Afrika Kushindwa Kuyaachia?

Gershom Ndhlovu anaangalia sababu za kwa nini watawala wa Afrika hawataki kuachia madaraka:

Kumekuwepo na tetesi, dondoo na hata uvumi kuhusu afya au basi udhaifu wa afya ya Rais wa Zambia Michael Chilufya Sata, aliye madarakani tangu Septemba 2011. Tetesi hizi zimekuwa zikisambaa kwenye mitandao ya kijamii kiasi kwamba serikali ya chama chake cha Patriotic Front (PF) imekuwa ikifanya jitihada za kuzidhibiti au hata kuzizima kabisa tetesi hizo.

Serikali haijajibu tetesi hizi ukiacha matamko ya mstari mmoja yanayokanusa habari kuhusu hali ya afya ya mkuu huyo wa nchi mwenye miaka 76 ambaye vile vile ni mwanasiasa wa siku nyingi.

Hata hivyo, Sata mwenyewe alipoonekana hadharani kwneye maadhimisho ya siku ya wafanyakazi Mei Mosi kupokea heshima kutoka kwa wafanyakazi nchini humo, na kukaa kwa muda mfupi hapo, na kutoa hotuba fupi ya dakika moja kabla ya kuingia kwenye msafara wake kurudi ikulu, watu wengi walianza kuamini kuwa Rais si mzima.

Macau: Watu 3,000 Wazunguka Baraza la Wawakilishi Kukwamisha “Muswada wa Walafi”

More than 3,000 protesters sit outside the Macau Legislative Council calling for the withdrawal of the out-going top official compensation bill, which is also known as "bill of greeds and privileges". Photo from All about Macau Facebook Page. Non-commercial use.

Zaidi ya waandamanaji 3,000 wakiwa wamekaa je ya Baraza la Wawakilishi kushinikiza kufutwa kwa muswada unaopendekeza masurufu kwa vigogo wa serikali wanaoondoka madarakani, muswada unaofahamika kama “muswada wa walafi”. Picha kutoka kwenye ukurasa wa Facebook wa All about Macau. Kwa matumizi yasiyo ya kibiashara.

Taarifa zaidi zinapatikana kwenyetaarifa yetu ya awali ya GV.

Uchaguzi wa Malawi 2014

Malawi inapiga kura kumchagua rais siku ya Jumanne Mei 20, 2014. Fuatilia taarifa za moja kwa moja kwenye mtandao wa Twita @Malawi2014 na @MEIC_2014.

“Hatujaweka Mkazo vya Kutosha Kwenye Afya ya Vijana”

Ripoti ya hivi karibuni kutoka kwa Shirika la Afya Duniani (WHO) kuhusu afya ya vijana duniani inabainisha kwamba

 Sababu kubwa za vifo vya vijana duniani ni ajali za barabarani, VVU?UKIMWI, na kujiua. Duniani kote, wastani wa vijana milioni 1.3 walipoteza maisha yao mwaka 2012.

Ripoti inaongeza vile vile kuwa :

Kiwango cha vifo kimeongezeka miongoni mwa vijana wa umri wa miaka  15  na 19 na pia wale wa umri kati ya miaka 10 na 14. Ingawa baadhi ya sababu za vifo hivyo zinafanana miongoni mwa jinsia, vijana wa kiume wako wanapoteza maisha kwa kasi zaidi kwa sababu ya kujiingiza kwenye vitendo vya matumizi ya nguvu wakati wasichana wakipoteza maisha kwa sababu ya matatizo ya uzazi.    

Baadhi ya sera zinapendekezwa kama hatua nzuri ya kukabiliana na mahitaji ya afya ya akili na ya mwili kwa vijana. Dk. Flavia Bustreo, Mkurugenzi Mkuu Msaidizi wa shirika la Afya ya Familia, Wanawake na Watoto, na Shirika la Afya Duniani   anataja kwamba:

Dunia haijaweka mkazo vya kutosha kwenye afya ya vijana. 

 

Simulizi za Jinsia na Wajibu

Kwenye blogu ya EnGenerada kuna tafakari ya kina [es] juu ya ujenzi wa utambulisho wa jinsia na masimulizi yanazyohusishwa na wanawake na wanaume. Wanahitimisha kwamba, licha ya kuwa ndugu katika hali halisi, wanafanya kazi kama utaratibu wa kawaida wa kijamii.

Makala iliyopitiwa upya hapa ni sehemu ya pili ya #LunesDeBlogsGV [Blogu za Jumatatu kwenye GV] Mei 12, 2014.

Gharama na Faida ya Kombe la Dunia Nchini Brazil

Blogu ya Daniel Bustos kutoka Colombia kuhusu uchumi wa Kombe la Dunia nchini Brazil na baada ya kugusia suala lisilo epukika la rushwa, inasema:

Hatimaye, Brazil itatumika kama “panya” kwa mataifa ya Amerika ya Kusini ambayo yalikuwa na ndoto kuwa siku moja itaandaa tukio hili kubwa, itatumika kuuliza kama Brazil itapata mapato mazuri na miundombinu yote iliyobadilishwa au kama, kinyume chake, lilikuwa ni kosa kubwa na la gharama kubwa, kama itafanya nchi kama yetu kutafakari juu ya kile kinachofanywa katika serikali katika masuala ya miundombinu, ajira, elimu, na bila shaka, kuwekeza katika michezo ili siku moja Kombe la Dunia litaweza kuandaliwa.

Posti iliyoainishwa ilishiriki katika #GVBlogsMondayya pili [es] Mei 12, 2014.

Jumuiya ya Kimataifa na Mgogoro wa Ukraine

guest blogs [es] ya Angie Ramos [es] katika Tintero kuhusu mgogoro wa kisiasa nchini Ukraine na baada ya kuchambua mambo mbalimbali muhimu husika anahitimisha kwa majibu ya Jumuiya ya Kimataifa:

Jambo ni, jumuiya ya kimataifa, inayokabiliwa na kesi kama hii, hufanya vitendo watakavyo kwa kuwa inategemea ukubwa wa maslahi yanayoshiriki kusaidia au kuelezea kukataliwa kwa baadhi ya uingiliaji kati katika nchi mbalimbali. Ni kwamba baadhi ya nchi wana mapendeleo kwa jumuiya ya kimataifa? Kwa mfano, katika kesi ya vita kati ya Uingereza na Argentina kuhusu Visiwa vya Falkland, kura ya maoni iliofanywa kuhusu idadi ya watu, ambapo 98% ya idadi walipiga kura kwa ajili ya kuwa chini ya utawala wa Uingereza, waliungwa mkono, wakati katika Crimea, hakuna wasia wa kukubali uhalali wa mchakato.

Posti iliyopitiwa upya hapa ni sehemu ya pili ya #LunesDeBlogsGV [Blogu za Jumatatu kwenye GV] Mei 12, 2014.

Ethiopia: #FreeZone9Bloggers Yavuma Kwenye Mtandao wa Tumblr

tumblr_n575s45oAT1tacd1co1_1280 Global Voices Advocacy ilianzisha mtandao wa Tumblr mapema mwezi Mei kutafuta uungwaji mkono kwa wanablogu tisa na waandishi wa habari – ambao wanne kati yao ni wanachama wa Global Voices – ambao kwa sasa wako kizuizini nchini Ethiopia shauri ya kazi zao. Washirika kutoka duniani kote waliwasilisha picha, ujumbe wa mshikamano, video na michoro kuonyesha kuunga mkono shinikizo hilo la kuachiliwa huru kwa wanablogu hao. Mei 19 #FreeZone9Bloggers Tumblr ilianza kuvuma katika tovuti ya vyombo vya habari vya kijamii. Unaweza kuwasilisha picha kwa Tumblr au jifunze njia nyingine unazoweza kuzitumia kusaidia kampeni hiyo ya utetezi.

Wanawake na Matumizi ya Mamlaka ya kisiasa

EnGenerada anauliza [es] wasomaji wake kama wana kile wanahitaji kutumia nguvu ya kisiasa.

Kila siku, tunasoma, kusikia, na kusema maneno: “Siasa ni chombo cha mageuzi ya jamii”. Mawazo yetu yanapokomaa, sisi huangalia katika baadhi ya uhakika wa mazingira yetu, hizo dhana za awali ambazo tumeziingiza kwa vizazi. Wakati huo huo uwezekano wa shaka wajitokeza na sisi kujiuliza: Je, siasa ni chombo cha mabadiliko? Je mamlaka ni muhimu kwa zoezi la siasa? Ni nini siasa hatimaye? Hatimaye, tunaweza pia kujiuliza na kuwa na shaka ifuatayo: Je, usawa wa kijinsia upo katika siasa? Kwa nini?

Baada ya kusema kwamba ni bora kusema kuhusu ujenzi wa kitamaduni na kijamii kama kinyume na utambulisho wa jinsia, wanahitimisha:

Kidogo kidogo, pamoja na ushirikiano, inawezekana kuunda mtandao wa uwezekano inayoruhusu mahusiano ya haki sawa zaidi, kwa kuweka kando mawazo ya awali kama “katika siasa, ni sawa daima“; au “mamlaka daima huharibu” ili kuanza kufikiria kwamba watu ambao wana uzoefu wa nguvu ya kisiasa wanaweza kubadilika, lakini kama utaratibu na njia ya kutekeleza mamlaka ya kisiasa haitabadilika, hakuna uwezekano kwamba uhakika wetu utabadilika.

Makala yaliyoainishwa yalishiriki kwanza katika blogu ya kwanza ya[es]#LunesDeBlogsGV [Blogu za Jumatatu kwenye GV] Mei 5, 2014. 

Maktaba na Utamaduni Huru

Blogu kutoka Parque Biblioteca Tomás Carrasquilla – La Quintana, huko Medellin, Colombia, inaelezea [es] msaada wake kwa utamaduni huru. Baada ya kueleze namna ya kuleta utamaduni wa uhuru [es], blogu hiyo inaelezea jinsi inavyoweza kufanya kazi inayofanana na maktaba:

Maktaba za umma zaweza kujifunza katika uhuru huu wa kubadilishana taratibu za ubunifu zilizofanywa ndani ya jamii wanazozihudumia, na hii inaweza kuwawezesha kwenye huduma za habari za mitaa, zilizoundwa kwa ushirikiano, zilizo shirikishwa, zilizoonekana na kupatikana kwa kila mtu ili maktaba nyingine, mashirika, vikundi vya utafiti na watu binafsi waweze kuwa na uwezo wa kuiga hayo, kuziboresha na kukabiliana nazo kwa mahitaji yao wenyewe na vifaa muhimu, hivyo kwa wakati wanaweza kutoa ule uzoefu wa awali na kutoa vyanzo mbalimbali kwa yale wamejifunza.

Makala yaliyopitiwa upya hapa ni sehemu ya kwanza ya #LunesDeBlogsGV [Blogu ya Jumatatu kwenye GV] Mei 5, 2014, iliyowasilishwa na María Juliana.

Changamoto za Elimu kwa Karne ya 21

Mikel Agirregabiria kwa kujifunza kutoka kwenye filamu Dead Poets Society aliweza kubainisha [es] mahitaji ya sasa ya elimu:

Elimu katika karne ya 21 yahitaji kushughulikia masuala ambayo hayakuwa bayana siku za nyuma, kama vile wapi unapotaka kuishi au kufanya kazi, kwa kutumia lugha gani au kwa utamaduni upi unaweza kujisikia vyema, unawezaje kujenga maisha yako ya kazi mara kadhaa,…

Makala haya yamepitiwa hapa kama sehemu ya pili ya #LunesDeBlogsGV [Jumatatu ya Blogu GV] Mei 12, 2014, iliyoletwa na @jgdelsol.

Naibu Waziri Ajinyonga baada ya Kushindwa Uchaguzi Nchini Malawi

Blogu ya City Press inaandika kwamba kujinyonga  kwa Godfrey Kamanya,  Naibu Wairi wa Malawi, baada ya kushindwa kukitetea kiti chake cha ubunge kwenye uchaguzi mkuu uliofanyika Mei 20, 2014 :

Matangazo rasmi ya uchaguzi huo uliofanyika Jumanne bado yanaendelea kutangazwa. Lakini matokeo ya awali ya uchaguzi huo yaliyotangazwa na kituo cha redio yalionyesha kuwa Kamanya alikuwa anafanya vibaya kwenye uchaguzi huo na alikuwa na uwezekano mkubwa wa kupoteza kiti chake chake cha ubunge.

Kupitia ujumbe aliouacha ambao kwa sasa upo mikononi mwa polisi, Kamanya anasemekana kusema kuwa aliamua kujinyonga kwa sababu ya migogoro ya kisiasa. Alieleza namna utajiri wake utagawanya na kumwomba Rais aliyeko madarakani Joyce Banda, ambaye alimtumikia, kumsaidia kulipa ada ya shule kwa mwanae.

Mapigano ya Wanakijiji Kugombea Ardhi Yasababisha Maafa Nchini Madagaska

Blogu ya L'Express Mada ilitoa taarifa kwamba kijiji kizima cha Andranondambo kilichoko Kusini mwa Madagascar kiliharibiwa [fr] kufuatia mapigano ya wanakijiji yaliyosababishwa na mzozo wa kumiliki ardhi. Vita vya wenyewe kwa wenyewe, ambayo ilidumu kwa siku tatu kati ya Mei 20-22, ilipoteza maisha ya wanakijiji wote. Akikumbuka tukio hilo, mmoja wa maafisa wa polisi anasimulia [fr]:

A notre arrivée, un chien errant était en train de dévorer un bras arraché d’ un corps. Dans une maison anéantie par les flammes, nous avons mis la main sur une dépouille. L’air était irrespirable [..] Même l’école publique et l’église d’Andranondambo ont été ravagées. Les toitures en tôle ont été arrachées avec tous les mobiliers.

Tulipowasili, mbwa alikuwa akila mabaki ya maiti. Katika nyumba jirani iliyokuwa imeharibiwa kwa moto, tulikuta maiti zaidi na uvundo usiovumilika. Hata shule za umma na makanisa vyote vilikuwa zimeharibiwa. Vifaa vyote kutoka kwa nyumba vilikuwa vimetawanyika.

Mgogoro wa ardhi ulianza mwaka wa 1991 wakati madini ya mica yilipogunduliwa katika kijiji hicho cha Andranondambo. Kukimbilia kwa wachimbaji wa ardhi kulipelekea wanakijiji kuhamia mbali katika kijiji kingine cha Ambatotsivala. Tangu wakati huo, vijiji hivi viwili vimekuwa na mgogoro juu ya haki za ardhi lakini mgogoro haujawahi kufikia kiwango cha taabu ya vurugu hadi hivi karibuni.

Jamaika: Alama Zinapoashiria Kikomo

Blogu ya Active Voice imetoa mkusanyiko wa twiti zenye mitazamo ya kupendekeza ufumbuzi kuhusu kampeni ya #bringbackourgirls inayodai kurudishwa kwa wasichana waliotekwa na magaidi wa Boko Haram.

Wajibu wa Kisayansi katika Mawasiliano

Katika mfululizo mpya wa Cosmos, Víctor R. Ruíz anaonyesha jinsi ambavyo kutafuta maarifa ya kisayansi limekuwa ni jukumu la kijamii na kisayansi katika nyanja za umma:

Kabla na wakati huo, makampuni binafsi na serikali yalikuwa na ajenda ambazo daima hazikuwa zikiambatana na maslaha mapana ya jamii. Makampuni ya mafuta yaliendelea kuhusiana na wanasayansi kwa malipo yenye kutia shaka. Nchi zinaendelea kufadhili maendeleo ya silaha za hali ya juu. Na wakati mwingine, mipaka kati ya maslahi binafsi na ya umma haiko wazi. Kama nilivyoeleza katika mazungumzo yangu ya Naukas Bilbao mwaka jana, Shirika la Usalama wa Taifa (NSA) huajiri theluthi tatu ya wataalamu wa hisabati kote duniani. Nyaraka zilizofichuliwa na Edward Snowden zinaonyesha kwamba wametekeleza na hata kuhujumu teknolojia ya mtandao kwa upelelezi wa ngazi za kimataifa, si kwa minajili ya kupambana na ugaidi kama kama ambavyo imekuwa ikifanyika kwa upelelezi wa kibiashara.

Víctor anahitimisha kutoka maoni yake hayo ya kisayansi:

Maneno matupu ya mwanasayansi wazimu yanaweza kuonekana kama hadithi, lakini mabomu yaliyoanguka Hiroshima na Nagasaki hayakutengenezwa na majeshi ovu. Hatuwezi kugeuza shavu la pili na kujifanya kwamba si wanasayansi wala wahandisi huendeleza teknolojia ambazo baadaye hutumika kwa minajili ya kupeleleza mabilioni ya wananchi au kuua raia kwa vifaa vya udhibiti. Leo, kama jana, ni wajibu wetu wote kuzungumza juu ya shauku ya elimu na kukosoa ushirikiano wa wanasayansi katika miradi ambayo hutishia jamii yetu.

Makala yaliyoainishwa yalishirikishwa katika blogu ya kwanza ya #LunesDeBlogsGV [Blogu za Jumatatu kwenye GV] Mei 5, 2014.

Colombia: Watoto 32 Wafariki Kwenye Mkasa wa Moto

Vyombo ya habari Colombia vinaripori [es] vifo vya watoto 32 uliosababishwa na moto katika basi, katika kitongoji cha Fundación mjini Magdalena, Kaskazini mwa Colombia. Tukio hilo la kutisha lilitokea Jumapili mchana, Mei 18, 2014. Hata kama ukweli bado unachunguzwa., Kuna uvumi kwamba gari lilikuwa linasafirisha petroli kimagendo.

Rais wa Colombia Juan Manuel Santos alionyesha huzuni wake kwenye mtandao wa Twita:

Huzuni mkubwa kama baba na kama M-Colombia kwa janga la watoto wetu katika Fundación. Mshikamano, maombi na msaada kwa familia zao.

Twaomboleza kwa ajali katika Fundación, Magdalena, ambapo kwa mujibu wa ripoti ya hivi karibuni, angalau watu 15 walifariki, kati yao watoto.

Mashindano ya Kublogu ya AFKInsider

AFKInsider imeandaa mashindano ya kublogu ambapo mwanablogu bora kila mwezi atahitajika kuandika hadithi ya kulipiwa kila wiki kwa AFKInsider mwezi ujao:

Mashindano ya wanablogu ya AFKInsider inanuia kugundua ubunifu wa wanablogu wa Biashara Afrika ambao huandika na wana nia ya teknolojia, kilimo, ujasiriamali, mali isiyohamishika, burudani, siasa, madini na habari nyingine za jumla ambazo hujumuisha bara la Afrika.

Ni aina gani ya wanablogu AFKInsider inatafuta na jinsi gani mtu anaweza kuchaguliwa?

AFKInsider inatafuta maudhui halisi ya kiasili ambayo imeripotiwa vizuri na yenye burudani kwa watazamaji wa Afrika. Sisi twatafuta mtu ambaye anaweza kujaza pengo katika nafasi ya vyombo vya habari Afrika kwa kuandika habari za kipekee ambazo vyanzo vingine vya vyombo vya habari havijaripoti. Kuchukuliwa kama mwanablogu mgeni katika AFKInsider unahitajika tu kuwasilisha blogu yako au hadithi kutoka blogu yako kwa mapitio na jopo letu la wahariri kupitia anwani ya barua pepe info@afkinsider.com.

Ousmane Sow : Mwafrika Mweusi wa Kwanza Kushiriki katika Taasisi ya Kifaransa ya Sanaa

Mchonga sanamu Msenegali, Ousmane Sow, alikaribishwa kwenye Académie des Beaux-Arts de Paris [Taasisi ya Sanaa ya Paris] tarehe 11, mwezi wa DisembaAfrica-top-talents.com inaripoti kwamba:

Une belle consécration pour ce sculpteur sénégalais connu pour ses séries de sculptures monumentales consacrées aux ethnies africaines (noubas, peuls, masaï, Zoulou). « Mon élection a d’autant plus de valeur à mes yeux que vous avez toujours eu la sagesse de ne pas instaurer de quota racial, ethnique ou religieux pour être admis parmi vous (…)  Comme mon confrère et compatriote sénégalais Léopold Sédar Senghor, élu à l’Académie française il y a trente ans, je suis africaniste. Dans cet esprit, je dédie cette cérémonie à l’Afrique toute entière, à sa diaspora, et aussi au grand homme qui vient de nous quitter, Nelson Mandela. »

Mchonga sanamu Msenegali, anayejulikana kwa kuchonga mafuatano yake ya sanamu muhimu zinazosawiri kabila za Kiafrika (Wanuba, Wafulani, Wamasai, Wazulu) ametunukiwa tuzo la ajabu. Anasema: “Kuchaguliwa kwangu ni muhimu zaidi kwangu, maanake, kwa hekima yenu [washiriki wa taasisi] hamujawahi kuunda viti maalumu vya kirangi, vya kikabila, wala vya kidini (…) Na kama mwandani wangu na Msenegali mwenzangu, Leopold Sédar Senghor, aliyechaguliwa kuingia Taasisi ya Kifaransa miaka thelathini iliyopita, mimi ni mtaalamu wa mambo ya Kiafrika. Kwa moyo huu, naiweka wakfu hafla hii kwa bara la Afrika, Waafrika wanaoishi nje ya bara hilo, na kiongozi mkuu aliyetuacha hivi juzi, Nelson Mandela.”

Video ya Dakika 5, Yaweza Kuwa Tiketi Yako ya Kwenda Mjini New York

Muungano wa Ustaarabu wa Umoja wa Mataifa (UNAOC) inawaalika vijana chini ya umri wa miaka 25 kuwasilisha video walizozitengeneza wenyewe zenye urefu wa dakika 5 juu ya uhamiaji, tofauti na kuingizwa kijamii kwa ajili ya tamasha kubwa la filamu 2014. Video tatu zitakazoshinda zitazawadiwa Dola za Marekani 1000 na watengenezaji wataalikwa jijini New York kuhudhuria sherehe za tuzo hizo.

Tarehe ya mwisho ya kuwasilisha ni Juni 27, 2014.

Kutana na Joshua Beckford Aliyehudhuria Chuo Kikuu cha Oxford Akiwa na Umri wa Miaka 6

Blogu ya Omg Ghana iliripoti kuhusu mafanikio bora ya kielimu ya Joshua Beckford:

Katika umri wa miaka 8, wewe pengine ulikuwa unafanya mazoezi ya michezo au ulikuwa ukifanya maandalizi ya kujiunga na daraja la tatu. Naam, kutana na Joshua Beckford mwenye umri wa miaka 8. Huyu yuko juu ya wastani wa mtu mwenye umri wa miaka 8. Alisoma katika Chuo Kikuu cha Oxford akiwa na umri wa miaka 6, na ni mfano wa kampeni ya wagonjwa wa akili katika jamii ya watu weusi na wachache (BME). Kampeni hiyo ilianzishwa ili kuonyesha vikwazo watu wenye asili ya weusi ambao mara nyingi hukutana nayo wanapojaribu kupata huduma ya kusaidia na huduma wanazohitaji. Beckford ni wa pekee, yuko juu zaidi kwa Kiwango cha daraja la shule alilohitajika na ilimlazimu kusomea nyumbani. Yeye hufanya vizuri katika Hesabu, Lugha za Kigeni, historia, falsafa, teknolojia na Sayansi.