Unaona lugha zote hapo juu? Tunatafsiri habari za Global Voices kufanya habari za kidunia zimfikie kila mmoja.

· Julai, 2012

Habari kutoka Muhtasari wa Habari kutoka Julai, 2012

Angola: Raia Wadai Kampeni za Uchaguzi za Wazi

Asasi za kiraia nchini Angola zinatoa wito wa uwazi zaidi [pt] katika maandalizi ya uchaguzi unaotarajiwa kufanyika tarehe 31 agosti, 2012. Moja wapo ya miradi iliyozinduliwa hivi karibuni kwa lengo hilo ni maombi ya mtandaoni [pt] ikiwataka viongozi wa vyama vinavyoshiriki uchaguzi huo kushiriki midahalo ya moja kwa moja kupitia televisheni za nchi hiyo.

Afrika: Usanii wa Kisasa wa ki-Afrika Mtandaoni

Usanii Afrika blogu inayoonyesha usanii wa kisasa wa ki-Afrika: Usanii Afrika ni blogu iliyozaliwa kutokana na upenzi. Akiwa amezaliwa na kipaji cha ubunifu yeye mwenyewe, mwanablogu, Kirsty Macdonald amekuwa na mahusiano ya karibu na masuala ya sanaa na kujieleza”

Togo: Muhubiri Asafirisha Kilo 4.2 za Madawa ya Kulevya Yaliyofichwa kwenye Pipi ‘k Build Church

Muhubiri wa Injili raia wa Togo, Woegna Yao Koufoualesse alikamatwa katika uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Accra akiwa na kiasi cha kilo 4.2 za madawa ya kulevya aina ya Cocaine akiwa kwenye safarini kutokea Sao Paulo, chapisho la Afrique Infos linaripoti [fr]. Madawa hayo yalikuwa yamefichwa ndani ya peremende za kijiti; Koufoualesse alijitetea kwamba hakujua kuhusu madawa hayo na kwamba piremende hizo zilikuwa ziuzwe kwa ajili ya kusaidia kupata fedha za kujengea kanisa.

Msumbiji: Je, Zana za Uandishi wa Kiraia Zimeua Blogu?

Katika mfululizo mfupi wa makala zake, Profesa Carlos Serra anabainisha baadhi ya sababu zinazoeleza kwa nini blogu za Msumbiji zinaendelea kupungua siku hadi siku. Msomaji mmoja anatoa maoni akidhani kwamba kublogu kunahitaji kazi kubwa katika kuhakikisha kuwa habari mpya zinaendelea kuwepo sambamba na kiwango cha habari hizo. Wakati Serra anasema kwamba zana za uandishi wa kiraia (kama vile twita na facebook) zinaweza kulaumiwa kusababisha hali hii, pamoja na faida za matumizi ya zana hizo.