Unaona lugha zote hapo juu? Tunatafsiri habari za Global Voices kufanya habari za kidunia zimfikie kila mmoja.

· Juni, 2013

Habari kutoka Muhtasari wa Habari kutoka Juni, 2013

Rais Obama Kuitembelea Tanzania

Rais wa kwanza wa Marekani mwenye asili ya Afrika, Barack Obama anatarajiwa kuwasili jijini Dar es Salaam kesho alasiri kwa ziara ya kiserikali. Blogu ya Swahili Time imeweka ratiba ya ziara hiyo ya siku mbili. Issa Michuzi aliweka video inayomwonesha Rais Kikwete wa Tanzania akizungumzia ziara hiyo.

Wanaharakati 36 wa Azeri Wakamatwa nchini Iran

Wanaharakati thelathini na sita wa Azeri akiwamo mwanablogu mmoja, Kiaksar, walikamatwa siku ya Alhamisi, 27 Juni katika eneo la Urmia. Vikosi vya usalama viliwaachilia huru wanaharakati hao 300 baada ya kuwahoji kwa masaa kadhaa.

Athari za Mazingira kwa Uchimbaji Madini Nchini Indonesia

Makala iliyochapishwa katika mtandao wa mongabay.com imefichua athari za uharibifu wa kimazingira ziazotokana na shughuli za uchimbaji madini katika maeneo ya vijiji nchini Indonesia. Baadhi ya wanazuoni wanahofia kwamba maeneo mengi nchini Indonesia yana kiwango cha juu kabisa cha zebaki duniani.

Misri Inavyopoteza Miji ya Kihistoria

Cairo..The city of a thousand pillars? Photograph from CairoObserver Facebook page. The red lines show buildings which obscure the minerates of mosques which is a signature of the Cairo horizon being lost to new development

Cairo..Jiji la nguzo elfu? Picha kutoka kwenye ukurasa wa Facebook wa CairoObserver. Mistari myekundu ikionyesha majengo ambayo huziba minara ya misikiti ambayo ni alama muhimu ya jiji la Cairo inayopotea kwa ujenzi mpya unaondelea.

Cairoobserver atoa wito [ar] kwa wakaazi wa Misri kupitia mtandao wa Facebook na Twita [ar] kufanya maandamano mbele ya majengo ya serikali, yanayohusika na mipango miji, kote nchini Misri kudai kusitishwa kwa kuharibiwa na kupotezwa kwa sura halisi ya kihistoria katika miji.

Jiji lenye minara elfu sasa ni jiji lenye nguzo elfu! Mji wa kihistoria ambao uliorodheshwa kama urithi wa dunia katika miaka ya 70 sasa unakabiliwa na uharibifu na kubadilika kila sifa yake na viongozi wanaishughulikia hali hii kama jiji lisilo rasmi lisilodhibitika tena
[…]

Jiunge nasi Jumatano Juni 19, 2013, saa 05:00 ( Masaa ya Cairo) katika Maandamano mbele ya ofisi la Gavana wa Cairo

‘Sauti za Iran’ Mradi Unaowapa Sauti Raia Waishio Vijijini

Sauti za Iran ni mradi ulioundwa kwa kutumia mafanikio ya mradi wa Ushahidi.  Sauti za Iran inakusudia kuripoti habari kuhusu miji midogo na vijiji vya Iran na vile vile kukusanya maombi na matatizo ya wananchi na kuyatuma kwa serikali na wabunge.

Je, Italia Iko Tayari kwa Waziri Aliyezaliwa Afrika?

“Je, Italia iko tayari kwa Waziri wa Serikalki aliyezaliwa Afrika?,” Donata Columbro anauliza:

Miezi miwili baada ya uchaguzi wa hivi karibuni, Italia ina serikali mpya. Na Cécile Kyenge, mwenye umri wa miaka 48,  daktari wa upasuaji macho na raia wa Italia aliyezaliwa Kongo, ni Waziri mpya wa Ushirikiano katika baraza la mawaziri la Waziri Mkuu Enrico Letta.

Alfabeti Hufurahisha na Kuhuzunisha Nchini Bulgaria

[…] Mojawapo ya likizo safi na takatifu zaidi nchini Bulgaria! Ni sherehe itupayo fahari ya kuwa tumetoa kitu chochote duniani! Ni likizo isiyohusiana na waasi wowote, vita, wala vurugu, ingawa hutujaza uzalendo na furaha. […] Unapotembea katika mitaa, mabango ya ugenini na maelekezo, yanazidi haya tuliyonayo kwetu kwa mbali sana […]

Akibainisha kwa huzuni juu ya kuongezeka kwa matumizi ya miandiko ya Kilatini nchini Bulgaria, mwanablogu Stranniche anaandika [bg] kuhusu Siku ya Utamaduni, Elimu na Alfabeti za Kibulgeria, maadhimisho ya kitaifa kukumbuka Watakatifu Cyril na Methodius, ambao wanakumbukwa kwa kuunda alfabeti kongwe za Kislavoni ziitwazo -alfabeti za Glagoliti. Katika siku hii, pia, Kongamano la kimataifa la Tatu la Kibulgeria lilianza, likikusanya wasomi karibu 500 kutoka nchi 34 kwenye Chuo Kikuu cha Sofia.

Matatizo Makuu ya Raia wa Benin ni Yapi?

Tite Yokossi anafunua matokeo ya kura ya maoni iliyoendeshwa na Mfuko wa Zinsou ambao uliwauliza wananchi wa Benin ni yapi ndiyo matatizo yao makuu leo [fr]. Tatizo la kwanza lililoorodheshwa lilikuwa uwezo mdogo wa kufanya manunuzi miongoni mwa watumishi wa umma. Mengineyo ni uwezekano wa kupata fursa ya elimu, huduma ya maji safi, huduma za afya na umeme, ulinzi wa raia na misaada kwa wakulima.

Ukatili wa Polisi Nchini Macedonia: Miaka Miwili Baadae

Stop Police Brutality June 6 2013

Siku ya Alhamisi, Juni 6, katika kituo cha Skopje, Vuguvugu la Kupinga Ukatili wa Polisi litatimiza miaka miwili baada ya mauaji ya Martin Neshkovski, ambayo yalisababisha maandamano makubwa katika ngazi za chini kabisa nchini Macedonia katika majira ya joto ya 2011. Tukio la Facebook [mk] kuhusu ibada ya kumbukumbu linaeleza:

Siku ya Alhamisi, Juni 6, saa 11 asubuhi, tutatembelea eneo la ulipofanyikia uhalifu huo na kuwasha mshumaa wa ishara ya kutukumbusha tulivyopoteza maisha machanga ya kijana wetu. Na akumbukwe!

Wakati wa kusanyiko hilo Vuguvugu la “Kuzuia ukatili wa polisi” litafanya mkutano na waandishi kuwasilisha ratiba ya shughuli za maadhimisho yake ya pili. Kwa kuongeza, tutawaunga mkono kwa wa-Turuki ambao wametoa upinzani kwa kumwaga damu zao wakipinga ukatili wa polisi siku za hivi karibuni […]

Mradi wa Kumbukumbu za Kihistoria Nchini Singapore

Ukiwa umeanzishwa mwaka  wa 2011, Mradi wa Kumbukumbu za Singapore unalenga “kukusanya, kuhifadhi na kuhakikishia upatikanaji” wa historia ya Singapore. Zaidi ya hayo, “ina lengo la kutengeneza mkusanyiko wa maudhui ya taifa ikiwa ni pamoja na maandiko, kanda za sauti na video kwa ajili ya kuzihifadhi  katika mfumo wa kidijitali, na kuzifanya zipatikane kwa ajili ya ugunduzi na utafiti.” Mradi huu unatarajia kukusanya kumbukumbu wa watu binafsi zipatazo milioni 5 ifikapo mwaka 2015.

Kufilisika kwa Watu nchini Malaysia

iMoney.my wametengeneza mchoro unaoelezea takwimu za kufilisika nchini Malaysia. Wastani wa matukio 20,000 ya kufilisika yamerekodiwa mwaka 2012 hiyo na maana kwamba wa-Malaysia 53 wanafilisika kila siku.

Uzuri wa Mlima Everesti Nyakati za Usiku

Sinema fupi za Elia Saikaly zimenasa uzuri mkuu wa Mlima Everesti nyakati za usiku kwa kila sekunde.

Anasimulia kwenye blogu yake uzoefu wake wa kupanda hadi kilele cha Mlima Everest kwa mara ya pili.

Bajeti ya Bangladesh: Maoni na Uchambuzi

“Bajeti ya kifahari lakini mpango duni?” Raia wa kawaida anatoa maoni na kuichambua bajeti ya hivi karibuni ya Bangladesh kwa mwaka wa fedha 2013-2014.

Jamaica: Watoto kama Wasanii

Blogu ya Maonyesho ya Sanaa ya Taifa Nchini Jamaika inayo msisimko kuhusu maonyesho yajayo ya sanaa ya watoto, ambayo yataonyesha “mwitikio wa pekee wa watoto kwa maswali kuhusu udadisi wao na msukumo wa aina tofauti wa ubunifu unaokua.”

China Yadaiwa Kuchimba Dhahabu Kinyume cha Sheria Nchini Ghana

Shirika la Habari la Xinhua limeripoti kwamba raia 124 wa Kichina waliodaiwa kushiriki katika uchimbaji wa madini haramu ya dhahabu walikamatwa na kuwekwa kizuizini nchini Ghana. Serikali ya China imetakiwa kulinda na kuwatetea raia wake. Kwa upande mwingine, maoni yaliyotokana na tukio hilo yaliukosoa unyanyasaji unaofanywa dhidi ya watu wa Afrika katika biashara ya madini ya dhahabu inayosimamiwa na China nchini Ghana. Mtandao wa China offbeat unayo maelezo ya kina.

Vijiwe Vya Usomaji Gazeti Mjini Mumbai Vyazorota

Vachanalays (vituo vya kusoma magazeti) ni jambo la kawaida katika vitongoji vingi mjini Bombay ambapo wenyeji husoma magazeti na kujadili habari zilizotokea siku husika. Sans Serif anaripoti jinsi vituo hivyo vinavyozidi kupitwa na wakati pole pole. Blogu hiyo pia inaonyesha picha nzuri inayojieleza ya mwanablogu wa picha M.S. Gopal juu ya maudhui hayo kwenye Mumbai Yasimamishwa.

Kukamatwa kwa Mwandishi wa Habari wa Kimasedonia Kwachochea Maandamano

"Who's next for Liquidation?" - a poster at today's journalist protest in Skopje, referring to the official code name of the operation ("Liquidation"), in which journalist Tomislav Kezarovski was captured on May 28. Photo by Biserka Velkovska/@bvelkovska, used with permission.

“Nani anayefuata kufilisiwa?” – bango katika maandamano ya leo ya wandishi wa habari mjini Skopje, akimaanisha jina la kificho kwa mpango unaoendelea (“Kufilisi”), ambapo mwandishi wa habari Kezarovski Tomislav alikamatwa pamoja na watu wengine mnamo Mei 28. Picha kwa hisani ya Biserka Velkovska/@bvelkovska, imetumiwa kwa ruhusa.

Waandishi wa habari wa Kimasedonia walikusanyika [tazama video na soma nakala] mbele ya Mahakama ya Makosa ya Jinai hivi leo katika mji mkuu Skopje kupinga kukamatwa kwa mwenzao, Tomislav Kezarovski, kwa mujibu wa maandishi haya [en] yaliyoandikwa katika ukurasa wa kundi la Kimasedonia kwenye mtandao wa Facebook yaliyopewa kichwa cha habari cha “Waandishi wa habari na wananchi katika kutetea haki ya uhuru wa habari.” Inaonekana kwamba sababu rasmi ya kutiwa kizuizini kwa Kezarovski kwa siku 30 ni habari aliyoiandika miaka mitano iliyopita kwa ajili ya jarida ambalo  halipo tena. Kwa upande mwingine, amekuwa akichunguza kifo cha Nikola Mladenov, mchapishaji na mhariri wa kampuni huru ya habari, kwa miezi miwili iliyopita.

Ingawa sababu rasmi ya kifo  cha Mladenov ni “ajali ya barabarani,” mengi hayajulikani katika tukio hilo. Kezarovski aliandika makala [mk] kuhusu masaa ya mwisho mwisho ya Mladenov, akitumia ushahidi uliogunduliwa na waandishi wa gazeti la kila siku liitwalo Nova Makedonija, kubainisha kuwa baada ya polisi kuondoka katika eneo hilo la tukio lililokuwa linalindwa isivyo kawaida, ushahidi mwingi uliachwa huko, ikiwa ni pamoja na risiti ya kulipa ushuru wa maegesho na sehemu za gari hilo.

Gwaride la Kwanza la Mashoga Nchini Lesotho

Leila Hall anablogu kuhusu gwaride la kwanza la mashoga kuwahi fanyika nchini Lesotho:

Tukio hilo limeandaliwa na Kikundi cha Kutoa msaada cha MATRIX- Shirika lisilo la kiserikali la Lesotho- linatetea haki za watu kama wasagaji, mashoga, wenye hisia za mapenzi kwa jinsia zote mbili, Wanaogeuza jinsia nchini humo. Shirika hilo, ambalo lilitambuliwa kisheria mwaka 2010, kama lilivyo gwaride la mwaka huu ni shirika la kwanza la aina yake nchini Lesotho.

Iran: Utani Kuhusu Mdahalo wa Urais

Raia wa mtandaoni kadhaa walitwiti kuhusu mjadala wa pili wa rais na waliwakejeli wagombea. Potkin Azarmehr alitwiti “Wagombea urais wanaweza kuombwa kucheza muziki.”