Unaona lugha zote hapo juu? Tunatafsiri habari za Global Voices kufanya habari za kidunia zimfikie kila mmoja.

· Septemba, 2012

Habari kutoka Muhtasari wa Habari kutoka Septemba, 2012

Afrika: Tuzo la Mbuyu wa Dhahabu

Wasilisha kisa chako upate fursa kushinda Tuzo ya Mbuyu wa Dhahabu: “Tuzo ya Mbuyu wa Dhahabu ilianzishwa mwaka 2008 kuwahamasisha waandishi wa ki-Afarika waliojikita katika vitabu vya watoto na vijana.”

 

Global Voices Yashinda Tuzo Ya Highway Africa

Highway Africa Award for Global Voices

Washindi: Dorothee Danedjo kutoka Kameruni akiwa na Ndesanjo Macha wa Global Voices. Picha ya Ettione Ferreira (imetumiwa kwa ruhusa)


Timu ya Global Voices inayoandika habari za Nchi za Afrika zilizo Kusini mwa Jangwa la Sahara imeshinda Tuzo ya Telekom Highway Africa katika kundi la “Blogu bora ya TEHAMA ya Kiafrika”. Mhariri wa Eneo hilo Ndesanjo Macha alikuwepo Afrika Kusini kuipokea tuzo hiyo (na kikombe cha ushindi!) tarehe 11 Sepetemba, 2012 kwa niaba ya timu nzima. Mwanablogu na mwandishi wa habari Dorothy Dandejo kutoka Kameruni alikuwa mshindani wa karibu aliyeibuka mshindi wa pili katika kundi hilo hilo.