Unaona lugha zote hapo juu? Tunatafsiri habari za Global Voices kufanya habari za kidunia zimfikie kila mmoja.

· Mei, 2013

Habari kutoka Muhtasari wa Habari kutoka Mei, 2013

Lebanon: Mwanablogu Apata Kipigo kwa Kupiga Picha

Mwanablogu wa ki-Lebanoni Habib Battah anaeleza namna alivyoshikiliwa bila hiari, akilazimishwa kufuta picha katika kamera ya simu yake na kudhalilishwa mfululizo katika posti hii inayohusiana na ripoti ya Beirut. Aliporipoti suala hilo katika kituo cha polisi mahali alipokuwa, mafisa wanaohusika walimkana na kumgeuzia kibao yeye. Anaongeza:

Walikuwa sahihi. Kama watu walikuwa eneo la tukio walikuwa tayari kunipa kichapo ili kumridhisha bosi wao, watu hao lazima wangeweza kudanganya kumridhisha. Na nilivyopigwa, hakuna mtu mtaani angekuwa tayari kutoa ushahidi namna walivyoninyanyasa namna ile.

Niliondoka polisi nikijisikia kuwa raia wa ki-Lebanoni hawalindwi na sheria. Matajiri wanaweza kutukanyaga kama sisimizi, kama tutajaribu kuwakasirisha.

Kwa nini Mashirika ya Umma Yameshindwa Nchini Zambia

Elias Munshya, mwanasheria na mchungaji wa Zambia, anaeleza kwa nini mashirika ya umma yamedumaa nchini Zambia tangu uhuru:

Mashirika ya umma hayajawahi kutengeneza faida tangu mwaka 1964. Yamekuwa yakiendeshwa kiholela bila utaalamu wa kibiashara bali kisiasa. Mashirika haya hayajawahi kuwa na wataalamu wanaoendesha bodi husika bali yamejaa wafanyakazi kwa misingi ya mahusiano ya undugu, ubinamu, upwa na ujukuu na wanasiasa

.

Rais wa Chama cha Madaktari Msumbiji Akamatwa

Baada ya mgomo wa madaktari uliodumu kwa takribani juma moja nchini Msumbuji, Dr. Jorge Arroz, Rais wa Associação Médica de Moçambique, amekamatwa usiku wa Jumapili, Mei 26, 2013, kwa tuhuma za “uchochezi” (kuhamasisha watu kutokuridhishwa au kuiasi serikali). Kwenye mtandao wa Twita na Facebook, @verdademz, @canal_moz na ripoti nyingine za watumiaji wa mitandaoni.

"Manu many health professionals here in the 6th police station of Maputo. Dr. Jorge Arroz is under arrest. Photo by @Verdade newspaper (used with permission)

“Watumishi wengi wa idara ya afya wakiwa katika kituo cha Polisi mjini Maputo. Dr. Jorge Arroz amekamatwa. Picha kwa hisani ya @Verdade (imetumiwa kwa ruhusa)

‘Igundue Somalia’ Blogu ya Picha na Utamaduni

Igundue Somalia ni blogu ya Picha na Utamaduni maalumu kwa Somalia. Blogu hiyo inakusudia kutangaza vyema sura sahihi ya Somalia kwenye vyombo vya habari na vipaji vya watu wake, masuala ya urembo na raslimali asilia.

Uchaguzi Tume ya Uchaguzi Msumbiji: Mwanaharakati Ajitoa Kugombea

Kutokuwepo uwazi na weledi katika mchakato wa kumchagua mgombea, mbali na kufahamika nani hasa watachukua nafasi zinazogombewa kabla hata ya uchaguzi katika taasisi hiyo. Hizo zilikuwa baadhi ya sababu zilizotolewa na mwanaharakati wa haki za binadamu, Benilde Nhalivilo, wakati akijitoa rasmi kugombea nafasi kwenye Tume ya Taifa ya Uchaguzi ya Msumbiji[pt], chombo kinachohusika na kuandaa na kusimamia chaguzi nchini humo. Taarifa zaidi zinapatikana kwenye gazeti la A Verdade [pt].

Michoro ya Dar: Sanaa kwa Maendeleo Endelevu

Dar Sketches (Michoro ya Dar) ni sehemu ya mradi unaoanzia ngazi ya Mtaa jijini Dar Es Salaam, Tanzania ulioanzishwa na msanii na mchoraji Sarah Markes:

Ni katika kuenzi urithi wa kitamaduni na wa sanaa ya ubunifu wa majengo kwa jiji la Dar Es Salaam sambamba na juhudi za kukuza uelewa kwa wananchi juu ua tishio la urithi huu linalotokana na kasi kubwa ya kupanuka holela kwa jiji hilo.

Wagombea wa Urais katika Uchaguzi wa Madagaska

Habari Mpya:  Hapa ni orodha kamili ya wagombea 49 [fr] wanaowania nafasi ya Urais katika uchauzi ujao. Orodha hiyo haina jina la rais wa sasa wa mpito.

Siku ya mwisho ya kurudisha fomu kwa ajili ya kugombea Urais katika uchaguzi ujao ilikuwa tarehe 28 Aprili, na inavyoonekana ni wagombea wachache sana wasiotarajiwa wamejitokea kuwania kiti hicho. Wakati wagombea wa awali walikuwa wapya kabisa wasiofahamika sana, wanasiasa wachache machachari wanaofahamika wanatarajiwa kugombea akiwemo rais wa zamani Didier Ratsiraka, rais wa sasa wa mpito Andry Rajoelina [fr] na mke wa rais wa zamani Ravalomanana, anayeitwa Lalao Ravalomanana.

Wafanyakazi Wavamia Majengo ya Serikali Nchini Mauritania

Photo of the clashes, uploaded by Abo Bakr Ahmado on his Facebook

Picha ya mapigano, iliyowekwa na Abo Bakr Ahmado kwenye ukurasa wake wa Facebook

Siku ya Jumanne asubuhi, Mei 28, 2013, maelfu ya vibarua, wanaolipwa ujira wao kwa kufanya kazi kwa siku, walianzisha maandamano makubwa [ar] huko Zouérat, mji mkuu wa jimbo la Tiris Zemmour kasikazini mwa Mauritania, wakidai mikataba inayoeleweka na haki zao nyinginezo ikiwa ni pamoja na kumalizwa kwa ukiritimba wa wafanyabiashara kwenye makampuni ya machimbo ya madini katika nchi za Kiarabu (ARMICO). Wafanyakazii hao waliandamana kuelekea kwenye makao makuu ya utawala wa jimbo hilo, majengo ya mmoja wapo wa makampuni ya wakandarasi, pamoja na majengo ya kituo cha redio ya taifa. Jeshi [ar] liliingilia kati kudhibiti hali hiyo na kuyatawanya maandamano hayo.

Mwanaharakati Magdy Ahmed alitwiti kuhusu kutoroka kwa gavana wa Tiris Zemmour baada ya wafanyakazi kuandamana [ar]:

@mejdmr :والي ولاية زويرات الجنرال ول باهية و الوالي المساعد وشرطة المدينة يفرون أمام غضب عمال الجرنالية الذين اقتحمو مبني الولاية والإذاعة الجهوية

@mejdmr: Gavana, Ould Bahia, naibu gavana na polisi walikimbia baada ya kushuhudia hasira ya wafanyakazi hao kwa siku moja walipovamia ofisi ya gavana na kituo cha redio ya taifa.

Botswana: Kuibwa kwa Kazi ya Sanaa ya “Bushman's Secrets”

MyWeku anaichambua filamu yenye maudhui halisi (documentary) inayoelezea wizi wa kazi ya sanaa ya Sana iitwayo “Bushman's secrets”:

Filamu hii inachora picha inayosikitisha ya namna ambavyo Uniliver, kampuni inayojinadi kama “mzalishaji mkubwa tena nambari moja duniani wa barafu zitengenezwazo kwa maziwa maarufu kama ice cream,” sasa linatumia bila aibu maudhui ya kazi ya sanaa ya Bushman's Secrets kujitangaza kama bidhaa ya kupunguza uzito.

Shambulio la Mabomu Mawili ya Kujitoa Muhanga Nchini Niger Yaua Watu 23

Benjamin Roger wa Jeune Afrique anaripoti [fr] kuwa wanajeshi 18, raia mmoja na magaidi wanne waliuawa mapema subuhi ya leo katika shambulio la mabomu ya kujitoa Muhanga kwenye gari mjini Agadez, Niger tarehe 23 Mei. Anaongeza kuwa wanafunzi wa chuo cha kijeshi wametekwa na gaidi mwingine kufuatia mabomu hayo. Wakati huo huo, gari jingine lilipuka kwenye mgodi wa madini ya Uraniam unaomilikiwana Kampuni ya Areva Group mjini Arlit, Niger. Kikundi cha kijeshi cha MOJWA kimedai kuhusika na mashambulio hayo mawili.

Msumbiji: Madaktari Watangaza Mgomo

Screenshot from press conference video

Picha ya video ya mkutano na vyombo vya habari

Madaktari nchini Msumbiji wametangaza rasmi kuwa wanaingia kwenye mgomo. Wanadhani “walikandamizwa, kutukanwa na kunyanyaswa” katika mkutano wao wa mwisho na serikali. Mgomo huu wa sasa unafuatia mgomo wa madaktari uliofanyika mapema mwaka huu. Tangazo kwa njia ya video linapatikana likiwa na tafsiri kwa maandishi ya kiingereza, na katika lugha kadhaa.

Mfululizo wa Tamthilia ya Runinga ya Nchini Tanzania

The Team Tanzania (Timu Tanzania) ni mfululizo wa Tamthilia ya Runinga yenye kuzungumzia:

[…] Bi. Wito, mwalimu mahiri wa somo la uraia, anaigeuza kabisa mitazamo ya vijana makinda watatu anapowauliza maswali mazito mfano “Wewe ni nani”? vijana wale wenye umri wa miaka 16, waliofahamiana vyema tangu wakikua. Katika kuingia katika umri wa utu uzima, vijana hao wanatafuta kujitambua huku wakikabiliwa na misongo mingi ya kifamilia na kiutamaduni.

TEDXSão Tomé: Mkutano Wanukia São Tomé na Príncipe

TEDXSão Tomé

TEDXSão Tomé

Uandikishaji wa awali kwa ajili ya mkutano wa TEDXSão Tomé umezinduliwa rasmi. Mkutano huo una kaulimbiu inayosema “Visiwa Vimeunganishwa : São Tomé + Príncipe = Áfrika Vimeunganishwa na Ulimwengu” na utafanyika tarehe 20 Juni. Wasemaji katika mkutano huo waliothibitishwa ni pamoja: Dynka Amorim, Ismael Sequeira, Profesa Robert Drewes na Aoaní d'Alva. Tiketi linapatikana kwa Euro 20. Zaidi kuhusu mkutano huo tembelea ukurasa wa Facebook na tovuti [viungo vyote katika lugha ya Kireno].