Unaona lugha zote hapo juu? Tunatafsiri habari za Global Voices kufanya habari za kidunia zimfikie kila mmoja.

· Septemba, 2013

Habari kutoka Muhtasari wa Habari kutoka Septemba, 2013

VIDEO: Shairi la Filamu “Maombi ya Woga” Latia Fora Misri

Mkusanyiko wa kiraia la Misri Mosireen umekuwa, bila kuchoka, ukiweka kumbukumbuza Mapinduzi ya Januari 25 na matukio yaliyofuata baadae kwa kutumia picha na dokumentari. Moja ya ubunifu wake wa mwisho mwisho ni “Maombi ya Woga”, shairi la filamu iliyotengenezwa na Mahmoud Ezzat na kusimuliwa na mwanachama wa Mosireen Salma Said. Kwa kumbukumbu zake zinazoishi na zenye uchungu, shairi filamu hilo linatia fora kwa uaminifu wake na ubinadamu.

…Je, tunashinda?
Au tunakubaliana na mauaji?
Je, swali ni la aibu?
Au kimya ni kibaya?
Turekebishe yaliyoharibiwa?
Au tuhesabu maiti?
Tulifungua njia?
Au njia imeharibiwa?…

Video ya shairi kamili hii hapa:

Boko Haram Waua Wanafunzi 50 wa Chuo Kikuu Nchini Naijeria

Kikundi cha kigaidi cha Naijeria Boko Haram kimewawasha moto bwenini na kuwaua wanafunzi wasiopungua 50 wa Chuo Kikuu cha Kilimo kilichopo kwenye Jimbo la Yobe, wakiwa usingizini. Rais Goodluck Jonathan alitangaza hali ya hatari katika eneo hilo kufuatia mfululizo wa vitendo vya kigaidi.

Bhutan: Sheria za Uchaguzi Zahitaji Mabadiliko

Yeshey Dorji anaunga mkono hatua ya Baraza la Taifa Butan kuanzisha mjadala wa rushwa wakati wa uchaguzi ambazo zimeripotiwa wakati wa Uchaguzi Mkuu uliopita zinazohitaji marekebisho yanayowezekana ya sheria ya uchaguzi.

Kwa nini Indonesia Haitakiwi Kupandisha Kima cha Chini cha Mshahara

Rocky Intan aneleza kwa nini kupandishwa kwa kima cha chini cha mshahara nchini Indonesia kutaathiri uchumi wa nchi hiyo:

Viongozi wa kitaifa na wale wa ngazi za chini lazima wapambane na shinikizo la baadhi ya viongozi wa vyama vya wafanyakzi wanaodai kupandishwa kwa kima cha chini cha mshahara. Ongezeko la kima cha chini limekuwa halihusiani na mfumuko wa bei, kinyume na madai ya waandamanaji. Zaidi, ongezeko hilo litasababisha matatizo zaidi ya wafanyakazi na hivyo kuathiri ushindani wetu katika uzalishaji unaotegemea nguvu kazi.

Picha Nyeusi: Waafrika Nchini Italia

Picha Nyeusi ni kazi za wapiga picha watatu – Marco Ambrosi, Matteo Danesin na Aldo Sodoma – Kituo cha Stadi za Uhamiaji mjini Verona, Majiji ya Verona na Padua, Chuo Kikuu cha Padua Idara ya Sosholojia ikiwaonyesha Waafrika nchini Italia.

Vyombo vya Habari vya Magharibi na Taswira ya Ellen Sirleaf Johnson

Aaron Leaf anajadili jinsi taswira ya rais wa Liberia, Ellen Johnson Sirleaf, hujengwa na vyombo vya habari kimagharibi kama alama ya mambo yote mazuri. Anasema kwamba hili ndiyo simulizi lililomwezesha Sirleaf kuwa mhimili wa maendeleo ya kimataifa na uwezeshaji wa wanawake.

Iran: “Mauaji” ya Wapinzani wa Iran 52 Wasiokuwa na Silaha

Vikosi vya usalama vya Iraq vilifanya “mauaji” ya wapinzani  wa Iran wapatao 52 ambao hata hivyo hawakuwa na silaha  asubuhi ya Jumapili ndani ya kambi yao kaskazini mwa Baghdad, mujahedeen-e-Khalq, wafungwa wa Iran walisema. Netizens in Balatarin, tovuti maarufu ya kusambaza habarii, iliweka picha kadhaa, filamu na posti kuhusiana na shambulio hilo.

South Korea: Ahadi ya Rais ya Ustawi Iliyoshindwa Yakosolewa

Rais Park yuko kwenye wakati mgumu kwa r  ahadi yake aliyoitoa wakati wa kampeni kuwa angepandisha ruzuku ya pensheni gharama za mafunzo. Wakosoaji wanasema kampeni yake iliahidi kinyume na sera yake kama mgombea mhafidhina, ilimsaidia kuzoa kura katika uchaguzi uliopita. Akaunti ya mtandao wa twita wa @metempirics ilikusanya viunganishi vinavyohusika na miitikio ya mtandaoni katika kipengele cha Habari (Storify).

India: Mgombea wa Uwaziri Mkuu na Historia yake ya Uhalifu

“Je, mtu anaweza kuwa na historia ya uhalifu na bado akawa Waziri Mkuu wa India?” – anauliza Dr. Abdul Ruff wakati anajadili uteuzi wa kiongozi wa mrengo wa kulia na Waziri Mkuu wa Gujarat Narendra Modi. Ni mgombea wa Uwaziri Mkuu wa chama cha National Democratic Alliance katika uchaguzi mkuu ujao wa India wa mwaka 2014.

Timu ya wanawake ya Mpira wa Kikapu ya Msumbiji Yafika Mbali

Kufuatia ushindi wa kishindo kwenye mashindano ya robo fainali (tazama habari zetu ), yaliyofanyika usiku wa jana timu ya mpira wa kikapu ya Msumbiji, wanawake, ilishinda nafasi ya kuingia kwenye Fainali za Mashindano ya Afrobasket usiku wa leo dhidi ya washindi watetezi Angola. Kwa staili nyingine ya kurudi kwa ushindi dhidi ya Kameruni kwenye hatua ya nusu fainali, waliweza kujihakikishia nafasi kwenye Mashindano ya Dunia, na kuandika historia mpya ya michezo nchini humo.

Serikali ya Tanzania Yafunga Magazeti Mawili

Serikali jana (terehe 27 Septemba, 2013) ilitangaza kuyafungia magazeti ya Mwananchi na Mtanzania kutokana na kuandika habari na makala zilizoelezwa zina nia ya kusababisha wananchi wakose imani kwa vyombo vya dola na kuhatarisha amani.

Taarifa ya kufungiwa magazeti hayo ilisema;

Gazeti la MWANANCHI limefungiwa kutochapishwa kwa siku kumi na nne(14) kuanzia 27 Septemba, 2013…
Gazeti la MTANZANIA limefungiwa kutochapishwa kwa siku tisini (90) kuanzia tarehe 27 Septemba, 2013

Daktari wa Peru ni Miongoni mwa Waathirika Waliopeza Maisha Westgate

Shirika la Habari la Andina limearifu [es] siku ya Jumamosi, Septemba 21, 2013, kwamba daktari wa ki-Peru Juan Jesús Ortiz ni mmoja wa watu waliuawa katika shambulizi la kigaidi lililotokea katika mji mkuu wa Kenya, Nairobi, lilisababisha idadi ya vifo vya watu 59 na wengine 175 wakijeruhiwa.

Hivi ndivyo Periodismo en Línea alivyotwiti habari hizo:

Daktari wa ki-Peru ni mmoja wa wahanga waliopoteza maisha katika shambulio la kigaidi lilitokea Kenya: Wizara ya Mambo ya Kigeni imethibitisha kwamba Juan Jesús Ortiz…

Kubusiana Kwenye Mitaa ya Misri

Picha inayosambazwa katika mtandao wa Facebook inayowaonyesha vijana wawili raia wa Misri wakibusiana barabarani iliibua hasira na wengine kuipenda. Ilitolewa na Ahmed ElGohary, mtangazaji aliyepingwa kwa ‘kukosa utu uzima’ kwa sababu ya kuweka picha ya jinsi hiyo. Wengine walisifu uzuri wa picha hiyo na tafsiri yake kwa mapinduzi ya kiutamaduni.

Two young lovers kiss on the street in Egypt, shared by Ahmed ElGohary  https://www.facebook.com/photo.php?fbid=10151429894938231&set=a.10151035748418231.432064.669983230&type=1&theater

Vijana wawili wakibusiana barabarani nchini Misri. Picha: Ahmed ElGohary http://tinyurl.com/l3rozz9

Kuonyesha mapenzi hadharanini si jambo linalokubalika nchini Misri, na sheria ya kuzuia kukosa maadili hadharani inaweza kutumika kuwashitaki wale wanaothubutu kuonyesha mapenzi hadharani au kunywa pombe katika mitaa.

Sambamba na picha, ElGohary aliweka mashairi ya wimbo wa Youssra El Hawary uitwao On The Street [Mtaani]. El Hawary mwimbaji huru chipukizi na nyimbo zake zimeonyesha mafanikio kwenye mtandao wa youtube. Mashairi ya On The Street yansema:

Baadhi ya watu kuwalaani wengine, kuua kila mmoja kwenye mitaani,
Watu wengine hulaaniana, huuana kwenye sakafu za mitaani,
Watu wengine huuza heshima zao mitaani,
Lakini ingekuwa kashfa ya kweli kama siku moja tutasahau na kubusiana kwenye mitaani!

Peru: Wafanyabiashara Wachoma Nguo Kupinga Bidhaa za Kichina

Wafanyabiashara kutoka eneo la Gamarra [es], kituo maarufu cha viwanda vya nguo na ambako ndiko lilipo eneo la kibiashara jijini Lima, walichoma nguo zilizoingizwa kutoka China [es] katika mitaa kupinga biashara hiyo ya nguo zinazouzwa bei ndogo ambazo, kwa mujibu wao, hufanya biashara zao kufilisika.

Kwenye mtandao wa Twita, Alfredo “Alial” (@ Alfredo_jch) [es] alipendekeza matumizi bora kwa nguo hizo zilizoteketezwa kwa moto:

Jijini Gamarra wanachoma moto nguo za Kichina, huko Puno watu wanaganda hadi kufa [kwa kukosa nguo]. #Perú

Mwishoni mwa wiki iliyopita, Jimbo la Carabaya, lililoko katika mkoa wa Puno, lilishuhudia dhoruba kali ya theluji mbaya zaidi kuwahi kutoka katika kipindi cha muongo, ikiathiri familia zaidi ya 1,200 na kuwaacha watu wengi wasiojulikana walipo na kusababisha vifo vya wanyama ambao ni riziki ya watu wa eneo hilo.