Unaona lugha zote hapo juu? Tunatafsiri habari za Global Voices kufanya habari za kidunia zimfikie kila mmoja.

· Machi, 2014

Habari kutoka Muhtasari wa Habari kutoka Machi, 2014

Mkuu wa Upelelezi wa Jeshi la Sudani Kusini Akana Jaribio Mapinduzi ya Kijeshi

Mkuu wa upelelezi wa jeshi nchini Sudani Kusini amekana kuwa kulikuwa na jaribio la mapinduzi ya kijeshi tarehe 15 Desemba, 2013.

PaanLuel Wel anaripoti:

Taarifa kutoka Juba zinasema mkuu wa upelelezo wa jeshi, Jenerali Mac Paul Kuol Awar, ametupilia mbali madai ya jaribio la kijeshi la Desemba 15, 2013. Mac Paul alitwa na serikali kutoa ushahidi dhidi ya mahabusu wanne wa kisiasa (Pagan, Oyai, Majak na Gatkuoth) waliopandishwa kizimbani wakijibu mashitaka ya uhaini.

Kimsingi, Mkurugenzi wa upelelezi wa kijeshi, aliyeitwa kuyapa nguvu madai ya serikali kuwa kulikuwa na mapinduzi, alikuwa imara kudai hapakuwa na kitu kama hicho. Badala yake, alisema, palitokea hali ya kutokuelewana miongoni mwa wanajeshi wa Tiger Battalion, ambao hawakudhibitiwa mpaka kutokuelewana huko kukaeneza uasi nchini kote.

Ufisadi Nchini Nepal: Umeanza Kuwa Tabia Inayokubalika Kijamii?

Watu wana hasira na wamechoka, na mashirika ya habari mara nyingi huchapisha habari kuhusu uhusiano kati ya viongozi wa kisiasa na wezi wa mali za umma lakini hakuna anayezungumzia kuingia mtaani kuandamana kupinga ufisadi -hali isiyotarajiwa kwenye nchi ambayo watu hugomea kila kisichokwenda sawa

Siromani Dhungana anaandika uchambuzi kwenye blogu ya United We Blog! akieleza mwenendo wa hali ya mambo nchini Nepal kwa kuonyesha ufisadi namna ufisadi unavyoanza kuwa sehemu ya maisha na kukubalika.

Kurudisha Mabaki ya Miili ya Binadamu tu Haitoshi, Ombeni Radhi, Namibia Yaiambia Ujerumani

Mabaki ya watu waliouawa wakati wa vita vya kikoloni (kwenye karne ya 20) yalirudishwa Namibia na Ujerumani mwezi Machi. Hata hivyo, Wanamibia bado wanadai tamko rasmi ya kuomba radhi kutoka kwa serikali ya Ujerumani kama  Tendai Marima,  mwanazuoni mtafiti wa fasihi za Afrika , aliandika kwenye tovuti ya Think Africa Press:

Mafuvu na mifupa yaliyorudishwa nyumbani mwezi huu yalichukuliwa na Ujerumani wakati Namibia -wakati huo ikiitwa ‘Ujerumani ya Kusini Magharibi ya Afrika’ -ikiwa ni moja la koloni lake. Namibia ilitawaliwa kwanza na mabeberu wa kizungu mwaka 1884, na 1904, watu wakabila la Waherero na Wanama − walionyang'anywa ardhi yao na mifugo -waliazimia kwa pamoja kupambana ili  kujaribu kuwafukuza Wajerumani.

Katika maasi hayo ya mwanzo, zaidi ya makabaila 100 wa Kijerumani na askari waliuawa, lakini juhudi za kupambana na mapinduzi hayo zilikuwa za kikatili na kinyama. Baada ya miaka mitatu ya kujaribu kuzima mapinduzi hayo, kadri ya watu wa kabila la Waherero na Wanama 10,000 waliuawa, hiyo ikiwa ni asilimia 80 na 50 ya makabila yao. Inasemekana kuwa hayo ndiyo yalikuwa mauaji ya kwanza ya kimbari katika karne ya 20.

Watumiaji wa Huduma ya Tor Waongezeka Nchini Uturuki

Mtetezi wa haki za binadamu na maadili Frederic Jacobs anabainisha kuwa idadi ya watu wanaotumia huduma ya Tor imeongezeka nchini Uturuki:

Uturuki ndio kwanza imeufunga mtandao wa Twita.

Katika Kutetea Lugha za Malawi

Kufuatia uamuzi wa serikali ya Malawi kuanza kutumia Kiingereza kama lugha ya mawasiliano kuanzia darasa la kwanza, Steve Sharra anatetea lugha la asili na anajenga hoja yake katika kutetea matumizi ya lugha zaidi ya moja:

Walimu na wahadhiri katika shule zetu za sekondari na vyuo vikuu wanashuhudia mwenendo wa mambo unaoonyesha kuwa wanafunzi wa shule binafsi wanazungumza Kiingereza fasaha, lakini uwezo wao wa kufikiri, kuandika na uwezo wa kufanya mahesabu uko chini. Hili limeonekana kwenye ripoti ya Chama Huru cha Shule nchini Malawi (ISAMA) kuwa wanafunzi wanaochaguliwa kwenda kwenye vyuo vikuu vya Malawi wanatoka kwenye shule binafsi.

Watafiti wa lugha wamegundua kuwa watoto wanaozungumza lugha zaidi ya moja wanafanya vizuri zaidi kitaaluma kuliko watoto wanaofahamu lugha moja tu, bila kujali ni lugha gani. Hii ndiyo sababu sera yetu ya lugha ya kufundishia inatakiwa kukuza matumizi ya lugha zaidi ya moja, na sio kutumia lugha moja tu. Ni katika kipindi cha kizazi kimoja tu kilichopita ambapo Wamalawi wengi walikuwa wakizungumza lugha zaidi ya moja, kwa wastani wa lugha mbili au zaidi. Katika kizazi cha leo, wengi wanafahamu lugha mbili tu, Kiingereza na Ki-Chichewa, kwa wastani. Kama hatutaweka sera za kuendeleza lugha zetu za asili, vizazi vijavyo vya Malawi vitabaki na lugha moja tu, Kiingereza.

Kuzungumza lugha moja kunasababisha kuwa na mtazamo finyu, kuyatazama mambo kwa uelewa mdogo kwa sababu ya ukweli kwamba maarifa yote ayanayopatikana yanakuwa kwenye lugha moja tu. Hatari ya sera hii mpya, kama ilivyo, ni uwezekano wake wa kuathiri lugha za asili za Malawi. Sera hii pya itamaanisha kuwa nchi itatumia raslimali zake zaidi kwenye Kiingereza kwa gharama ya kulea na kuendeleza lugha za asili.

Trinidad na Tobago: Washindi wa Tuzo za Hollick Arvon

Blogu ya Bocas Lit Fest imewatangaza waandishi chipukizi kutoka Jamaica, Grenada, St. Vincent na Trinidad na Tobago kuwa washindi wa Tuzo zinazovuta watu wengi za Waandishi wa nchi za Karibiani za Hollick Arvon kwa mwaka 2014, ambazo kwa mwaka huu zilifanyika kwa mara ya pili.

Uchambuzi zaidi Kuhusu Muswada wa Kupinga Ushoga Nchini Uganda

Kristoff Titeca anaangalia mbali zaidi ya sababu moja kuhusiana na muswada wa kupinga ushoga nchini Uganda:

Pointi muhimu ni kuwa Rais Museveni hajawahi kuwa shabiki mkubwa wa muswada huu na badala yake amekuwa mtu wa kuutilia mashaka: alikuwa anafahamu matokeo mabaya kimataifa. Katika majibu yake ya wazi kwa mara ya kwanza baada ya muswada huu kuletwa, alisema muswada huu “haukuwakilisha sehemu ya msimamo wa serikali” na namna “Uganda isivyoweza kuwa tayari kuhatarisha sera yake ya mambo ya nje kwa kuruhusu muswada huu kupia ukiwa katika sura iliyopo”. Mwaka unaofuata, muswada ulififia na ukawekwa kapuni, (mwaka 2009, 2011 na 2013), mpaka ulipoonekana tena Desemba 20, 2013, ulipopitishwa na bunge.

Baada ya kupitishwa, Museveni aliendelea kuwa na msimamo usioeleweka: alidai imekuwaje muswada upitishwe bila yeye kujulishwa, na kwa haraka kiasi kile, tena na idadi ndogo ya wabunge wakiongozwa na spika Kadaga. Kufanya hivyo kulimlazimu kulitazama suala hili kwa kina zaidi. Katika mahojiano yake pamoja na matamko, Museveni mara zote alikuwa amejikita katika masuala mawili: Kwenye ufundishaji wa watu kuwa mashoga (na linalofanana na hili, ni, wale wanaofundishwa, wale ambao wanageuka kuwa mashoga kwa sababu za kibiashara) na pili, kuonyesha hadharani tabia ya ushoga. Katika kufanya hivyo, aliacha upenyo, kuwa kuna uwezekano wa kuwa watu fulani wanazaliwa mashoga (…) tabia zisizo za kawaida kwa binadamu na zinazotokea mara chache. Katika kufanya hivyo, angeweza kuwaridhisha wananchi wake wa ndani -aliwakosoa mashoga – lakini na watu wa nje, kwa kuacha upenyo wazi. Kwa mfano, hata baada ya kutangaza kwamba ataenda kusaini muswada huo, kama majibu baada ya Obama kumkosoa, Museveni alidai kuwa anaiomba Marekani utoe ushahidi kuwa kuna watu wanazaliwa mashoga, hatua ambayo ingemwezesha kuipitia upya sheria hiyo.

Fasiri ya Lugha ya Kikannada ya Karne ya 11 Yapatikana kwenye Mfumo wa Wikisource

Vachana Sahitya ni aina ya uandishi kwa mtindo wa sauti katika lugha ya ki-Kannada ambao ulianzia karne ya 11 na kukua sana kwenye karne ya 12. Makala ya Subhashish Panigrahi inaripoti (ikiwa imeandikwa kwa ushirikiano wa Pavithra Hanchagaiah na Omshivaprakash) kwenye blogu ya Wikimedia kwamba waandishi wawili wa Wikimedia wakishirikiana na mtaalamu wa lugha ya ki-Kannada wamegeuza beti 21000 za Vachana Sahitya katika mfumo wa Unicode na hiyo kwa sasa zinapatikana kwneye Wikisource, maktaba ya kidigitali ya mtandaoni ambayo ina maudhui ya nyenzo za maandishi yanayopatikana bure.

Msichana Nchini Madagaska Ajiua Baada ya Picha Zake Kusambazwa Facebook

Koolsaina anaandika kwamba msichana mmoja wa ki-Malagasi alijiua [fr] baada ya picha zake kusambazwa kwenye ukurasa wa Facebook unaoonyesha picha za wasichana wa Madagaska bila ruhusa yao. Wito ulitolewa kwa utawala wa Facebook ulitolewa ili kuufunga ukursa huo. Mpaka leo (Machi 16, 2014), Koolsaina anasema ukurasa huo bado unapatikana.  

Shule 2,715 Kuunganishwa na Mtandao wa Intaneti Nairobi

Shule 2,715 jijini Nairobi, Kenya hivi karibuni zitaunganishwa na mtandao wa intaneti wa bure:

Wanachi Group [kampuni] imefikia makubaliano ya kutekeleza mradi wa thamani ya Dola za Marekani milioni 3 (Takribani KSh milioni 270) na kaunti ya Nairobi, ili kuunganisha shule 2,715 jijini Nairobi na mtandao wa intaneti.

Mradi huo ulizinduliwa leo na ifikapo mwezi Juni mwaka huu (ndio, ndani ya miezi mitatu), shule 245 za mfano zinatarajiwa kuwa zimeunganishwa tayari. Baada ya hapo, mradi huo utatathiminiwa na awamu ya pili itaanza ndani ya miaka mitatu hadi mitano.

“Pamoja na mtandao wa bure wa intaneti, kampuni hiyo itaipatia kila shule vifaa vya kidijitali kwa ajili ya kuunganisha televisheni kwa ajili ya matumizi ya kupata maudhui ya elimu kwa njia ya sauti kwa faida ya wanafunzi. Watoto wa shule za awali watapata vifaa hivyo pia ikiwa ni pamoja na televisheni ndogo,” ilisema taarifa ya kampuni hiyo ya Wananchi.

Wanawake wa Sri Lanka na Mbinu za Kuzuia Mimba

Mwandishi, Mpiga picha na mwanablogu Meg at Life in Lanka anaripoti kuwa kwenye sehemu za vijini nchini Sri Lanka baadhi ya wanawake hawana kauli kuhusu aina ya mpango wa uzazi wanaoutaka.

Waume zao hawatumii kondomu na wanapenda wake zao watumie mbinu nyingine za kupanga uzazi; kwa hiyo njia rahisi inayopatikana kirahisi na yenye ufanisi ya kutumia kondomu haipendwi na wanaume, hiyo ikifanya suala la kujikinga na mimba zisizotarajiwa kuwa ni wajibu wa mwanamke.

Kwa sababu ya ukweli kuwa madawa ya kupanga uzazi mara nyingi yana madhara kwa wanawake, mateso hayo huwa hayaishi.

Mlipuko wa Homa ya Ebola Waua Watu 59 Nchini Guinea

Ebola virus virion via wikimedia Commons -  Public Health Image Library, #10816- public domain

Virusi vinavyosababisha Ebola viitwavyo virion kupitia wikimedia Commons – Picha ya Maktaba ya Afya ya Umma, #10816- kwa matumizi ya umma

Mlipuko wa homa ya Ebola umeua watu wasiopungua 59 nchini Guinea na matukio kadhaa yanayohofiwa kuwa ya homa hiyo yamekaribia kwenye mjini mkuu Conakry hiyo ikimaanisha kuwa ugonjwa huo unaweza kuenea kwenye mji mkuu wa Guinea. Barbara Krief anatoa taarifa za hivi karibuni [fr]:

Au moins huit agents de santé ont été tués à ce jour. En collaboration avec le ministère guinéen de la Santé, l'Unicef a rapidement livré dans les zones les plus affectées cinq tonnes de médicaments et d'équipements médicaux tels que des gants, nattes plastiques, couvertures, protège-nez, et des solutions de réhydratation orale et intraveineuse pour protéger le personnel médical et traiter les malades

Kadri ya wafanya kazi wa afya nane wamepoteza maisha mpaka sasa. Kwa kushirikiana na Wizara ya Afya ya Guinea, UNICEF imepeleka tani tano za madawa na vifaa vya matibabu kama vile glovu za mikononi, vitambaa, mablanketi, vitambaa vya kufunika uso, na maji ya kupunguza upungufu wa maji mwilini kuwalinda wafanyakazi wa afya na kuwatibu wagonjwa.

Hapa kuna video yenye taarifa za namna ya kujilinda na virusi vya Ebola :

Twiti ya kwanza kutoka kwa Rais wa Madagaska

Madagascar president Hery Rajaonarimampianina - Public domain

Rais wa Madagaska Hery Rajaonarimampianina – Picha ya matumizi ya umma

Rais mteule wa Madagaska Hery Rajaonarimampianina amefungua akaunti yake ya mtandao wa twita mnamo tarehe 23 Machi, 2014. Hii ndiyo twiti yake ya kwanza : 

First tweet by president of Madagascar

Twiti ya kwanza ya rais wa Madagaska

Kuna uwezekano mkubwa kuwa hiyo ndiyo twiti maarufu kutoka kwa mkuu wa nchi. Ni Rupert Murdoch anaweza kuwa na wasiwasi na kiwango cha “ukubwa/umaarufu” wa twiti yake ya kwanza. Rais wa Madagaska ana sifa yake ya pekee kuwa mkuu wa nchi mwenye jina refu kuliko wengine /a>.

Saudi Arabia Inadhibiti Majina ya Watoto

Huruhusiwi kumwita mwanao wa kike majina kama Eman, au Sandy, au Yara. Na kama ni mvulana, majina kama Abdelnasser, Amir au Abdulmoeen hayaruhisiwi. Lakini hiyo si Saudi Arabia pekee. Kwenye mtandao wa twita, Iyad El Baghdadi anaorodhesha majina ya watoto yaliyopigwa marufuku kabisa kwenye ufalme huo:

Orodha ya majina yaliyopigwa marufuku Saudi Arabia ni pamoja na Abdulnasser, Amir, Maya, Linda, Sandy, Loren, Benjamin, Yara, Eman.

Na kuna picha muhuAnd there is a photograph of an officially stamped list to go with this notice.

Maombi ya Mtandao wa WeChat na ‘Self-Media’ kwa Raia wa China

Mitandao ya ’s , huduma ya ujumbe binafsi kwa namna fulani imechukua nafasi ya mtandao unaofanana kidogo na Twita uuitwao Sina Weibo kama chombo kinachoongoza kwa mawasiliano mbadala. Mtandao wa Tea Leaf Nation  umeelezea maombi ya mtandao wa WeChat na “self-media” kwa ujumla/a> kwa kizazi cha Wachina vijana, na maana ya  hatua yake ya dharura/a>. 

Je, Sheria Mpya ya Ubakaji India Inawasaidia Wanawake?

Tumepata sheria ambayo inaelekeza kuadhibu ubakaji, na ambayo imebanua tafsiri ya ubakaji na kujumuisha watu wengi zaidi – wakati tatizo kubwa lilikuwa kwamba watu waliokuwa wanabakwa kwa mujibu wa tafsiri na adhabu za zamani hawakuwa wanatendewa haki katika nchi ambayo kuna ubakaji kw akila dakika saba, lakini hakuna hata tukio moja la ubakaji linahukumiwa.

Vidyut katika blogu ya AamJanata anauliza ikiwa sheria mpya ya ubakaji nchini India inawasaidia wanawake.

Trinidad na Tobago: Tume ya Mapinduzi

Je, Trinis inajali ripoti ya dat de iliyotolewa na Tume ya kuchunguza jaribio la mapinduzi ya Abu Bakr mwaka 1990 ambayo ndio kwanza imetoka?

Trini inapendekeza kwamba kutolewa kwa matokeo haya kunaweza kuchukuliwa kuwa ni ya kiwango cha chini, na yamekuja kwa kuchelewa.

Namna Tabia ya Kula Hotelini Inavyoathiri Utamaduni wa Kula Mtaani Indonesia

Ismanto kutoka Yogyakarta nchini Indonesia anabainisha namna mtindo mpya wa kimagharibi wa kula mikahawani unapunguza tabia ya kula “vyakula vya kufunikwa na plastiki” inayofahamika kama ‘angkringan':

… vyakula vya angkringan vimepungua. Wanafunzi hawazitumii tena, wakifurahia kulipia vyakula ghali bei iliyo mara mbili zaidi, kunywa na kujumuika na watu katika mtindo wa mikahawa. Kama wanafikiria chakula cha angkringan, basi itakuwa ni cha tofauti, chenye hadhi ya chini kinachopondwa na watu wasio na fedha, tabaka la masikini na watu wa kizamani. Na mara nyingi panakuwa hakuna hali kujiona fahari kwa wanafunzi kwenye ‘kampani’ yake.

Korea Kaskazini: Ni Lini Itaanguka?

Ingawa Korea Kusini inaonekana kutengeneza mahusiano na Korea ya Kaskazini, wataalamu wana wasiwasi kidogo kuhusu kubashiri kuanguka kwa Korea Kaskazini. NKnews.org ilichapisha posti nzuri kuhusu uwezekano wa kutawanyika kwa utawala wa kidikteta, akihitimisha kuwa ‘mageuzi ya kiuchumi ya Pyongyang yanaongeza uwezekano wa tukio la kuanguka vibaya’.

Teknolojia ya Kiafrika: Mradi wa TechAfrique Watathmini Hatua Iliyofikiwa

 Le continent africain apparaît comme la nouvelle frontière mondiale du développement numérique. Ce développement provoque une nouvelle impulsion entrepreneuriale en Afrique, et notamment en Afrique francophone. Mais ce potentiel reste très largement méconnu en Europe ainsi qu'en France. 

Bara la Afrika linaonekana kuwa kiongozi mpya wa dunia katika maendeleo ya kidijitali. Maendeleo haya yamesababisha kukua kwa ujasiria mali mpya barani Afrika, hususani kwenye nchi zizungumzao Kifaransa. Lakini uwezo huu unabaki kuwa siri isiyofahamika huko Ulaya na Ufaransa.

Kubadili hali hii, Samiri, mwandishi wa blogu ya  Startup BRICS [fr] ilijikita kwenye miradi mipya katika nchi zinazoendelea, aliandaa safari za kiuchunguzi zilizoitwa  Mradi wa TechAfrique ili kugundua na kuorodhesha miradi iliyopo na ile mipa, miradi ya Fablabs, na kwenye maeneo mengine yanayofanana na hayo katika ubunifu wa kiteknolojia katika nchi zizungumzao Kifaransa pamoja na Kenya.