Unaona lugha zote hapo juu? Tunatafsiri habari za Global Voices kufanya habari za kidunia zimfikie kila mmoja.

· Novemba, 2009

Habari kutoka Muhtasari wa Habari kutoka Novemba, 2009

Malawi: Rais Ataka Nguvu Zaidi

Rais wa Malawi ataka nguvu zaidi!: “rais wa Malawi Bingu wa Mutharika, ambaye chama chake kina wabunge wengi katika bunge, anataka kunonesha nguvu zake kabla hajatoka kwenye ulingo wa siasa mwaka 2014.”

China: Obama ni Mshabiki Mkubwa wa Kutokuchuja Habari

Adam Minter amesikitishwa na maoni ya Obama kwenye Mkutano uliofanyika kwenye Ukumbi wa Jiji la Shanghai, hasa, maelezo yake kuwa “Mimi ni muunga mkono mkubwa wa kutokuchuja habari“.

Finland: Suala la Lugha

Nordic Voices anaandika kuhusu ‘suala la lugha” huko Finland.

Palestina: Mtaa wa Twita

Eman katika AquaCool anatoa maoni kuhusu mtaa wa kwanza kupata jina linalotokana na huduma ya Twita, katika kambi ya wakambizi huko ukingo wa Magharibi.

Uganda: Ugonjwa wa Panzi Waota Mizizi

Wanasiasa wa Uganda wanakuwa kama panzi: “kufuatia hali ya kufikia kikomo kwa tawala nyingi za kiimla, Museveni na washirika wake katika ukaliaji wa mabavu wa Buganda kwa kutumia silaha wanaanza kuwa kama panzi.”

Naijeria: Ken Saro-Wiwa Akumbukwa

Chidi Opara anamkumbuka Ken Saro-Wiwa, Mwandishi wa Kinaijeria, mwanaharakati wa mazingira na haki za walio wachache ambaye aliuwawa na watawala wa kijeshi wa Naijeria tarehe 10 Novemba, 1995.

Cuba: Ukweli wa Sanchez Kutiwa Mbaroni Waibuka

Kukamatwa, kupigwa na kuachiwa huru kulikofuata kwa wanablogu Yoaní Sánchez, Claudia Cadelo na Orlando Luis Pardo kulikofanywa na majeshi ya usalama ya Cuba tarehe 6 Novemba, kunapata matangazo mengi katika vyombo vikubwa vya habari na katika ulimwwengu wa blogu pamoja na ule wa Twita. Yoani ameandika (es) kuhusu tukio hilo kwenye blogu yake, Generación Y, na blogu za Kiingereza kama vile Babalú Blog, Repeating Islands pamoja na Uncommon Sense zinafuatilia habari hiyo. Mahojiano ya sauti (es) na Sanches kuhusu tukio hilo yamepandishwa kwenye YouTube.

Ghana: Vionjo Sehemu ya Kwanza

Sehemu ya kwanza ya vionjo vya Ghana iliyotayarishwa na Gayle: Nchini Ghana, kila kanda ina kitu cha kutoa. Utamaduni, historia, pwani, wanyama na mimea, unaweza ukavivinjari nchini kote, kutokea kwenye mitisitu ya kitropiki kule kusini mpaka mbuga za savana za kaskazini. kama ni mpenzi wa pwani au historia, utaburudika na ziara hii ya sehemu za pwani.

Vietnam: Matangazo Mengi Katika Uwanja wa Ndege

Charvey amebaini matangazo mengi kuliko kawaida katika uwanja wa ndege wa Vietnam.

Kenya: Ramani Mpya Ya Wazi ya Kitongoji Cha Kibera Kwenye Blogu

Mradi wenye lengo la kutengeneza ramani mpya ya wazi ya kitongoji cha Kibera mjini Nairobi, Kenya: “Na jana tulimaliza siku nzima pale MS Action Aid kenya, ambako wanafunzi wa ki-Denmark pamoja na wengine waliotokea kwenye mashirika mbalimbali kama vile Ushahidi, UNICEF, Umande Trust na World Bike, walipoonyeshwa mbinu za kutengeneza ramani.”

Afrika: Haki za Wanawake

Sokari anaandika kuhusu Toleo Maalum la Masuala ya Wanawake la Pambazuka linaloangalia miaka 15 iliyopita tangu mkutano au Jukwaa la Vitendo mjini Beijing pamoja na mustakabali wa haki za wanawake barani.

Karibea: Tuzo za Fasihi ya Kifaransa

Wiki hii, waandishi wawili wenye asili ya Kiafrika wanaoandika kwa Kifaransa walipewa tuzo mbili zenye kuheshimika sana katika fasihi ya Kifaransa: Ulimwengu wa blogu za wanaozungumza Kifaransa katika Karibea umekuwa ukinguruma juu ya kutosheka kwao mara mbili kwa mpigo, katika makala hii kutoka Haiti, na hii kutoka Guadeloupe na hii kutoka Martinique [Fr].

India: Usawa

“Takriban asilimia 15 ya watu ambao ni viongozi wa siasa na watumishi wa serikali, kwa kupitia vitendo vya kifisadi, wamejilimbikizia asilimia 85 ya utajiri wote wa India, na kuwaachia asilimia 15 tu ya utajiri huo asilimia 85 ya wananchi,” anasema Ram Bansal katika blogu ya India in Peril.

Jordan: Barua kwa MBC

M-jordan Ola Eliwat, kutoka Cinnamon Zone, anaandika barua ya wazi kwa makapuni ya televisheni ya MBC. Katika barua hiyo anaandika: “Na tafadhali fikirieni kufunga 90% ya idhaa zenu, nadhani itakuwa hisani KUBWA kwa taifa la Kiarabu!”

Afrika Kusini: Wimbo wa Taifa kwa Wanaoongea Kiingereza

Wimbo wa Taifa wa Afrika Kusini kwa wanaoongea Kiingereza: Ni njia kuu iliyoje ya kufafanua kwa kuonyesha Wimbo wa taifa wa Afrika Kusini kwa wale kati yetu ambao kwanza hatuufahamu mpaka sasa, pili tunaoufahamu lakini pengine hatujui jinsi ya kutamka maneno yake na tatu ambao hatuongei lugha iliyo kwenye wimbo huo.

Kenya: Mwai Kibaki na Odinga Budi Washirikiane na ICC

Ubia wa Kuleta Mabadiliko umetoa tamko linalowataka mwai kibaki na raila odinga kushirikiana na mahakama ya kimataifa ya Jinai na kuhakikisha muswada wa Tume Maalum unapitishwa nchini kenya na kurasimishwa kama sheria ndani ya wiki mbili.

Yoani Sanchez Pamoja na Wanablogu Wengine wa Cuba Wakamatwa na Kupigwa

Jioni ya tarehe 6 Novemba, blogu ya Babalú iliweka kiungo kuelekea makala iliyoandikwa na Penultimos Dias (es) ilitoa taarifa kuwa baadhi ya wanablogu mashuhuri wa Cuba, wakiwemo Yoaní Sánchez na mchangiaji wa Global Voices Claudia Cadelo, walitiwa mbaroni na majeshi ya usalama. Habari mpya kutoka kwa Penultimos Días zinataarifu kuwa Sanchez na Orlando Luis Pardo “walipigwa vibaya na kutukanwa”.

Tunisia: Mwanablogu Fatma Arabicca Awekwa Kizuizini

Mwanablogu wa Kitunisia Fatma Riahi ambaye hublogu kama Fatma Arabicca, ameshtakiwa kwa udhalilishaji katika blogu yake na hivi sasa amewekwa kizuizini.Kundi limeundwa kwenye Facebook kumuunga mkono mwanablogu huyu mwenye umri wa miaka 34, ambaye pia anatuhumiwa kublogu kwenye Debat Tunise (Mdahalo wa Tunisia).

Afrika: Chungu cha Kuiyeyusha Afrika

Marvin anaandika kuhusu Afripot, tovuti ya habari inayotilia makini habari za Afrika: “Hivi sasa anatambulisha chungu cha kuyeyushia Afrika – Afripot. Tayari nimo ndani ninayeyuka na ninatumaini kukuona pale na wewe pia kwani mazungumzo kuhusu Afrika na Waafrika yanachukua kasi na kupamba moto. Ni nani ajuaye, inaweza kutengeneza joto la kutosha na kulazimisha mabadiliko tuayoyahitaji sana.”

Iran: Majeshi Ya Usalama Yawashambulia Waandamanaji

Kwa mujibu wa Kian majeshi ya usalama yaliwashambulia waandamanaji katika viwanja vya hafteh tir mjini Teheran na kuwajeruhi watu kadhaa.