Unaona lugha zote hapo juu? Tunatafsiri habari za Global Voices kufanya habari za kidunia zimfikie kila mmoja.

· Julai, 2013

Habari kutoka Muhtasari wa Habari kutoka Julai, 2013

Hali ya Uislamu Katika Asia ya Kusini

Murray Hunter wa Chuo Kikuu cha Malaysia Perlis anajadili hali ya jamii ya Kiislamu katika Asia ya Kusini pamoja na masuala yanayohusiana na kukua kwa Uislamu katika eneo hilo.

Umaskini, kujua kusoma na kuandika, elimu, kuhamishwa, ukabaila, ukosefu wa ajira, ukandamizaji, na udhibiti ni mambo yanayowaonea Waislamu ndani ya ASEAN. Serikali pamoja na Ulama wanajaribu kukuza utawala wa kidini kwa msingi mdogo wa utafiti wa kijamii na kiuchumi pamoja na maarifa, na badala yake kujaribu kukuza mila zinazolingana. Tafsiri za Kiislamu zimejikita katika fikra na mawazo yasiyobadilika ambapo tafsiri mpya zapaswa kujengwa kwazo.

Barua ya Wazi ya Kushinikiza Kuachiwa Huru kwa Mwanasheria

Mnamo Julai 23, 2013, zaidi ya raia 400 wa China wamesaini barua ya kushinikiza serikali ya China kumuachia huru Xu Zhiyong, ambaye ni mwanasheria mashuhuri na mpigania haki aliyekamatwa mnamo Julai 16 baada ya kushinikiza kuachiwa kwa wanaharakati pamoja na kuratibu kampeni dhidi ya uovu unaofanywa na serikali. MRADI WA VYOMBO VYA MAWASILIANO WA CHINA (CHINA MEDIA PROJECT) ulitafsiri barua hii kwenda katika lugha ya Kiingereza.

Mwana-Habari Menna Alaa Ashambuliwa na Wafuasi wa Morsi

Mwanablogu na mwanahabari wa video Menna Alaa leo hii ameshambuliwa na waandamanaji wenye hasira wanaomwunga mkono Morsi. Mwanablogu huyo ameweka ushuhuda wake kwa lugha ya kiingereza kwenye makala hii iliyo katika blogu inayokusanya matukio nchini Misri iitwayo Egyptian Chronicles. Anaandika:

Kofi nililopigwa usoni, alama iliyobaki usoni mwangu pamoja na kuibwa kwa kamera yangu hakutanizuia kuendelea kutoa habari. Ninatoa habari ya kile nikionacho na nitaendelea kuhabarisha pamoja na kuhatarisha maisha yangu. Ukweli ni kile kitakachonifanya niendelee kuipenda kazi yangu.

Shindano la Wanablogu wa Kiafrika wenye Fikra Pevu.

Mtandao wa Africa Brains watangaza Shindano la Wanablogu wa Kiafrika Wenye Fikra Pevu watakaowania kitita cha dola Hamsini ($50).

Ni muda muafaka wa kutangaza mada ya kwanza, ambayo ni “Teknolojia imekuwa na ushawishi gani katika elimu yako?”
Tufahamishe hali ya upatikanaji wa teknolojia ulipokuwa shuleni au chuoni? Tangu uanze kutumia teknolojia, kumekuwa na mabadiliko? Wewe na wanafunzi wenzako mmekuwa na ufahamu wa zaidi wa teknolojia kuliko walimu wenu?

Tanzania: Uchaguzi Mdogo wa Madiwani Arusha Waipa CHADEMA Ushindi

Uchaguzi mdogo wa Madiwani Jijini Arusha umefanyika kwa amani leo Jumapili Julai 14. Mtandao maarufu wa Jamii Forums uliripoti yanayoendelea Arusha wakati wote na baada ya uchaguzi. Blogu ya Wavuti imeweka matokeo ya uchaguzi huo pamoja na picha mbalimbali za uchaguzi:

Huku Tume ya Uchaguzi ikisubiriwa kuwatangaza rasmi washindi, taarifa za awali zinasema kuwa CHADEMA [chama kikuu cha upinzani nchini Tanzania] imepata ushindi kwa kunyakua Kata zote Nne

Mwandamanaji Amtaka Morsi Kuondoka Kwa Lugha ya Mafumbo

Maandamano makubwa ya kumtaka rais wa Misri Mohamed Morsi ajiuzulu yanaendelea nchini Misri kwa siku ya tatu sasa.

An innovative protest sign. Leave written in 14 languages coded in QR. Photograph shared on Twitter by @AssemMemon

Bango la Maandamano. Neno ondoka limeandikwa katika lugha 14 za mafumbo. Picha imewekwa kwenye mtandao wa Twita na  @AssemMemon


Kwenye mtandao wa Twita, Assem Memon anaweka picha iliyopigwa kwenye maandamano:

@AssemMemon: Bango la Maandamano. Neno ondoka limeandikwa katika lugha 14 za mafumbo. Picha imewekwa kwenye mtandao wa Twita na @ alaafareed pic.twitter.com/S7OOSDfpV6

Tamko la Kurekebisha Sheria Zinazokwaza Uhuru wa Vyombo vya Habari Nchini Vietnam

Zaidi ya wanablogu 60 wa Ki-vietinam walitia saini tamko la pamoja kuitaka serikali ya Vietnam kuboresha rekodi ya haki za binadamu na ahadi wanapowania uanachama katika Baraza la Umoja wa Mataifa ya Haki za Binadamu:

Serikali ya Vietnam pia inahitaji kutathmini  hali ya haki za binadamu katika nchi hiyo na wa-Vietinamu pia wana haki ya uhuru wa maoni na kujieleza, ikiwa ni pamoja na masuala haya.

Kama watetezi wa uhuru wa kujieleza nchini Vietnam na wahanga wa ukiukwaji wa haki za binadamu kwa sababu ya harakati zetu, sisi twaona mgombea Vietnam kwa Baraza la Haki za Binadamu kama jukwaa kwa ajili ya majadiliano ya kujenga haki za binadamu katika nchi yetu.

Maandamano ya Kudai Uchaguzi nchini Madagaska Yasababisha Vurugu

Protests in Antananarivo, Madagascar on July 22, 2013 photo via MaTV

Maandamano jijini Antananarivo, Madagaska tarehe 22 Julai, 2013. Picha kupitia MaTV

Blogu ya Vola R ya Ma-Laza inaandika kwamba watu 7 walijeruhiwa [fr] kufuatia matumizi ya nguvu yaliyofanywa na polisi dhidi ya waandamanaji waliokuwa wanadai kufanyika kwa uchaguzi mjini Antananarivo, Madagaska. Chama kinachoongoza maandamano kinasema kwamba utawala uliopo hauna dhamira ya kuitisha uchaguzi mwaka huu na kwamba serikali imeng'ang'ania madarakani. Kiongozi wa chama hiko alidaiwa kukamatwa kufuatia maandamano hayo.

Peru: Mchezaji wa Kandanda Afariki Dunia Uwanjani

Dakika tano kabla ya kumalizika kwa mchezo kati ya timu zaReal Garcilaso na Sporting Cristal, mchezaji nyota wa timu ya Sporting Cristal mwenye miaka 18 Yair José Clavijo alipata mshituko wa moyo na akapoteza maisha. Madaktari wa timu hiyo walijaribu bila mafanikio kunusuru hali yake akiwa kwenye sehemu ya kuchezea katika uwanja wa Manispaa ya Urcos, katika mkoa Cusco.

Mtangazaji wa zamani wa kandanda Elejalder Godos [es] aliungana na watumiaji wa mtandao wa Twita ambao waliamua [es] kuingia kwenye mtandao huo kuonyesha hisia zao kuhusu habari hizo za kusikitisha:

Rambirambi zangu kwa familia ya Yair Clavijo kwa kifo cha ghafla cha mchezaji kinda wa timu ya Sporting Crital akiwa uwanjani.

Watu Sitini Wauawa Kwenye Mapigano Mjini Nzérékoré, Guinea

Tovuti ya Guinee News inaripoti idadi ya vifo kufikia 60 kutokana na mauaji ya Nzérékoré, Guinea [fr] :

Les cinquante deux corps qui étaient non identifiables ont été enterrés dans une fosse commune hier. Les autres corps reconnaissables ont été remis à leurs familles.

miili 52 ambayo haikutambulika ilizikwa kwenye kaburi la pamoja jana. Miili minngine ilirudishwa kwa wafiwa.

Hali ya Kidiplomasia Kati ya Zimbabwe na Nchi za Magharibi

Simukai Tinhu, mchambuzi wa masuala ya siasa anayeishi London, anauliza, “Je, mahusiano ya Zimbabwe na nchi za kimagharibi yanaimarika kadri uchaguzi unavyokaribia?”

Kitu gani kinaifanya Brazil ifanane na Uturuki?

Nchi za Brazil na Uturuki zimetengwa na umbali wa maelfu ya kilomita, lakini zina kitu fulani cha kufanana: nchi zote mbili ziliingia mitaani kudai haki zao kama raia na sasa wanahangaika kujinasua na matumizi ya nguvu na unyanyasaji wa kupindukia unaofanywa na polisi.

V rVinegar ni tovuti iliyotengenezwa kufuatilia maandamano na kukuza uungwaji mkono wa matukio hayo katika nchi husika: nchini Brazil, kupinga uwepo wa polisi [pt], na kusitishwa mara moja kwa vurugu nchini Uturuki [tr]