Unaona lugha zote hapo juu? Tunatafsiri habari za Global Voices kufanya habari za kidunia zimfikie kila mmoja.

· Januari, 2014

Habari kutoka Muhtasari wa Habari kutoka Januari, 2014

UBUNIFU: Makontena Yatumika Kama Hosteli za Wanafunzi wa Vyuo Vikuu Ulaya

 "Containers" at DTU Campus Village in Kongens Lyngby, Denmark via wikipedia CC-BY-SA-3.0

“Makontena” katika kamapasi ya DTU huko Kongens Lyngby, Denmark kupitia wikipedia CC-BY-SA-3.0

Ili kuondoa uhaba wa hosteli kwa ajili ya wanafunzi unaovikabili vyuo vikuu barani Ulaya, baadhi ya vyuo vikuu nchini Denmaki, Ujerumani, Ufaransa (Le Havre) [fr] na Uhispania vimejaribu kubadili makontena na kuyafanya yawe hosteli za wanafunzi. Makontena yanaonekana kufaa kwa sababu hayana gharama kubwa na yanazoeleka kirahisi. Hata hivyo, taasisi kadhaa tayari zimeibua masuala kadhaa  [fr] kuhusiana na mifumo ya kuyapasha “makazi” hayo joto pamoja na masuala ya usalama. 

Mwaliko wa Mapendekezo ya Tuzo za Blogu Nchini Kenya 2014

Waandaaji wa Tuzo za Blogu nchini Kenya 2014, ambao ni Umoja wa Wanablogu nchini humo (BAKE) kwa sasa wanakaribisha mapendekezo ya wawaniaji wa tuzo hizo mpaka Februari 10, 2014.  Watumiaji wanaweza kupiga kura kwa njia ya mtandao kuanzia Machi 1, mpaka April 30, 2014 kupendekeza blogu wanazoona kuwa ni bora katika makundi 17 tofauti, ikiwa ni pamoja na kundi jipya la Blogu bora ya Afya na Blogu Bora ya Kaunti/Wilaya.

Bake logo

Nembo rasmi ya BAKE. Picha imetolewa: http://bloggers.or.ke.

Tuzo za Blogu nchini Kenya,  ni mradi wa  Umoja wa Wanablogu wa Kenya (BAKE) , wanakusudia kuwazawadia wnaablogu wanaobandika posti zao mara kwa mara, wenye maudhui sahihi na yenye kusaidia, wabunifu na wenye mambo mapya. Makundi mengine ni pamoja na: 

 • Blogu bora ya Teknojia
 • Blogu bora ya Picha
 • Blogu bora ya Uandishi wa Kiubunifu
 • Blogu bora ya Biashara
 • Blogu bora ya Chakula
 • Blogu bora ya Kilimo/Mazingira
 • Blogu bora ya Mitindo/Urembo/Nywele
 • Blogu bora ya Siasa
 • Blogu bora Mpya
 • Blogu bora ya Shirika
 • Blogu bora ya Mada
 • Blogu bora ya Michezo
 • Blogu bora ya Burudani/Mtindo wa Maisha
 • Blogu bora ya Kusafiri/li>
 • Blogu bora ya Mwaka nchini Kenya

Hapa chini kuna video ya kuzinduliwa kwa Tuzo za Blogu Nchini Kenya:

Blogu zinaweza kupendekezwa kwa kutumia kiungo hiki.  

PICHA: Kimbunga BEJISA Chasababisha Uharibifu Mkubwa katika Visiwa vya Reunion

Cyclone Bejisa by @delarue_julien on twitter

Kimbunga Bejisa na @delarue_julien katika twitter

Januari 2, Kimbunga Bejisa kilisababisha uharibifu mkubwa katika kisiwa cha Reunion kilicho chini ya mamlaka ya Ufaransa. Mtu mmoja alifariki na wengine 15 kujeruhiwa vibaya, huku idadi ya nyumba zinazokadiriwa kufikia 82,000 zikiripotiwa kukosa huduma ya nishati ya umeme. Kimbunga hiki kimeshatulia na hali ya hatari imeshatangazwa kisiwani humo. Zifutazo ni picha nyingine zilizopigwa na raia waishio nchini humo:

http://www.youtube.com/watch?v=_mXLMJe7oKM
Video ioneshayo kimbunga Bejisa katika Kisiwa cha Reunion. Video imewekwa na animax2013 katika mtandao wa Youtube.

Uharibifu uliofanywa na kimbunga Bejisa katika jiji la Mtakatifu Denis

Uvumbuzi: Kompyuta Inayotumia Nishati ya Jua Nchini Mali

Limmorgal, a low power PC made in Mali via Tech of Africa with permission

Limmorgal, Kompyuta inayoendeshwa kwa nishati ya jua iliyotengezwa nchini Mali na Kampuni ya Tech of Africa kwa ruhusa

Kama sehemu ya mfululizo wetu juu ya teknolojia na ugunduzi unaofanyika Afrika, hivi karibuni tulionyesha Mashine ya Kuchapishia picha zenye umbo halisi yaani 3D iliyotengenezwa kutokana na taka pepe nchini Togo na mashine ya kukagua usahihi wa maneno katika lugha ya spell ki-Bambara . Leo, tunawaletea kompyuta ya kwanza kutumia umeme mdogo iliyotengenezwa nchini Mali. Kompyuta hiyo inayoitwa Limmorgal (ikiwa na maana ya kikokotozi kwa lugha ya ki-Peul) ni zao la bongo za vikundi viwili vya raia wa Mali, Jumuiya ya Intaneti Mali (ISOC Mali) na Intelec 3. Mamadou Iam Diallo, rais wa ISOC Mali, anaeleza mahitaji wanayohitaji kuyatatua kwa kutumia kompyuta hiyo akiongea na Blogu ya Bamako[fr]:

Nous avons conçu cette machine pour contribuer à la réduction du fossé numérique, mais également à la vulgarisation de l’outil informatique surtout en milieu scolaire. Limmorgal est aussi un ordinateur adapté à l’alimentation par l’énergie solaire grâce à sa faible consommation d’énergie.

Tulibuni kompyuta hii kusaidia kupunguza pengo kati ya walio mtandaoni na wale wasiomudu huduma za kidijitali, lakini pia  upanuzi wa matumizi ya kompyuta mashuleni. Limmorgal ni kompyuta ilitengenezwa mahususi kutumia umeme wa nishati ya jua na inatumia nishati kidogo sana (Watt 24 tu zinahitajika).

Sifa za kompyuta hiyo ni kama ifuatavyo :

 • Mfumo wa Ufanyaji kazi (Operating system): Ubuntu (zana huru) 
 • Uwezo wa kutafuta ni 1.4 G Hertz
 • 1GB RAM
 • Bei : 171000 Fcfa (Tsh 650,000 hivi)

Uajemi: Washairi Wawili Watiwa Nguvuni

Washairi Mehdi Mousavi na Fatemeh Ekhtesari wametokomea nchini Uajemi. Kwa mujibu wa taarifa za habari, washairi hao wamewekwa kizuizini tangu mwanzoni wa mwezi Desemba. Zaidi ya watu mia mbili wametia saini hati ya malalamiko mtandaoni na kutoa wito kwa Umoja wa Mataifa kuchukua hatua kuhusiana na hali za wanaharakati wa utamaduni hususani suala la washairi hao vijana nchini Irani.

Shindano la Kuchochea Uanzishwaji wa Biashara Mpaya Nchini Madagaska

Harinjaka, mwanzilishi wa mradi wa Habaka na mwanablogu anayeishi Madagaska, ameanzisha Shindano la biashara mpya Antananarivo 2014  [fr] lenye lengo la kuchagua na kuunga mkono wazo la biashara nchini Madagaska. Anaamini kwmaba kuna  mustakabali mzuri kwa ujasiriamali na ubunifu [fr] nchini Madagaskari. Hapa unaweza kuona tangazo la tukio hilo[fr] :   

"The objective of the Start Up Cup is to connect founders with business investors and VCs." on the Facebook Page of the event

“Lengo la Shindano hilo la miradi mipya ni kuwaunganisha waanzilishi wa biashara hizo na wawekezaji na wadau wengine” kupitia Ukurasa wa Facebook wa tukio hilo kwa ruhusa

Trinidad & Tobago: Mambo Madogo Yaweza Kuleta Utofauti

ban-d-wagonist aweka video yenye “maoni rahisi ya namna ambavyo raia wa kawaida wanavyoweza kuijenga Trinidad na Tobago yenye mafanikio.”

Rais wa Korea Kusini Aapa Kupambana Uzushi Unaoenezwa katika Mitandao ya Kijamii

Je, serikali ya Korea Kusini imejiandaa kwa kufuatilia mitandao ya kijamii? Matamshi ya hivi karibuni ya Rais Park (full transcript [ko]) yamewashitua wa-Korea wanaotumia mtandao. Park, akiwalenga “uvumi ule unaosambaa kupitia mitandao ya kijamii”, alisema “kama serikali ikiachia mambo haya yakaendelea, itakuwa ghasia nchi nzima” na kuongeza “kumbukeni mamlaka za nchi zinahitaji kuchukua hatua kwa haraka sana na  kwa hisia zinazotakikana dhidi makundi yale yanayoharibu hali ya hewa”. Watumiaji wengi wa mtandao wa twita walipigia kelele wasiwasi wao na kuonyesha ukweli (kama twiti ya @ppsskr [ko] ambayo ilizunguka zaidi ya mara 500) kwamba vyombo vya serikali vimelituma zaidi ya twiti milioni 24 ili kumpa nafuu Park   wakati wa uchaguzi wa rais uliofanyika hivi karibuni.

Wa-China Wametafuta Nini Zaidi Mtandaoni mwaka 2013

Mtandao wa kutafutia habari mtandaoni nchini China uitwao Baidu umetoa orodha ya maneno yaliyotumika zaidi kusaka habari. Orodha ya maneno kumi yaliyotumika zaidi ni kama ifuatavyo:

 1. Hali ya Hewa
 2. Taobao (tovuti ya kufanyia manunuzi ya mtandaoni nchini China)
 3. Wu Dong Qian Kun (kitabu cha mtandaoni cha Li Hu)
 4. The Tang Door  (kitabu cha mtandaoni)
 5. Mang Huang Ji (kitabu cha mtandaoni)
 6. Zhe Tian (kitabu cha mtandaoni)
 7. Double Chromosphere (Mchezo wa kamari wa Kichina)
 8. Baidu (!)
 9. Da Zhu Zai (kitabu cha mtandaoni)
 10. Qzone (a new mtandao wa kijamii from Tencent)

Kwa orodha kamili, fuatilia mtandao wa  China Internet Watch.