Unaona lugha zote hapo juu? Tunatafsiri habari za Global Voices kufanya habari za kidunia zimfikie kila mmoja.

· Mei, 2015

Habari kutoka Muhtasari wa Habari kutoka Mei, 2015

ISIS Yashambulikia Kwa Mara Nyingine Msikiti wa Shia Nchini Saudi Arabia

kwenye dawati lakuthibitisha habari la Global Voices, mradi unaoendeshwa kwa ushirikiano kati ya Meedan Checkdesk, zana ya mtandaoni ya kufuatilia habari, na Global Voices Online, Joey Ayoub anaonesha miitikio ya awali kabisa kuhusu kupigwa bomu kwa msikiti wa pili wa Shia huko Dammam, Jimbo la Mashariki mwa Saudi Arabia, siku ya Ijumaa.

Watu watatu wameuawa kwenye shambulio hilo la kujitoa mhanga, na Walayat Najd, tawi la ISIS nchini Saudi Arabia, limedai kuhusika, na watu kumi wamejeruhiwa.

Mnamo Mei 22, mtu aliyekuwa na bomu alijilipua kwenye msikiti wenye watu wengi huko Al Qadih, kwenye jimbo la Qatif, na kuua watu wasiopungua 21, ikiwani pamoja na mtoto, na kujeruhi wengine 120, kwenye shambulio baya kuwahi kuonekana katika kipindi cha miaka kumi nchini Saudi Arabia.

Mwezi Novemba, watu nane waliuawa huko Al Ahsa, kwenye jimbo la Mashariki, baada ya wanamgambo kushambulia kituo cha kijamii kinachomilikiwa na Shia, mahali ambapo sherehe ya kidini ilikuwa ikiendelea.

Mjamzito wa Miaka 11 Agoma Kutoa Mimba Nchini Uruguay

Kugoma kwa mjamzito wa miaka 11 kutoa mimba kumesababisha utata.

Hivi karibuniTuliandika kuhusu msichana wa miaka 10 aliyekuwa mjamzito nchini Paraguay kwa kudaiwa kubakwa na baba yake wa kambo na namna alivyoshindwa kutoa mimba hiyo kwa sababu sheria za nchi hiyo zinazuia utoaji wa mimba. Sasa, nchini Uruguay, ambako utoaji wa mimba unaruhusiwa ndani ya majuma 12 ya mwanzo ya ujauzito, tukio la msichana wa miaka 11 aliyegoma kutoa mimba limeishangaza nchi.

Msichana huyu, anayesemekana kuwa na ulemavu wa akili, alibakwa na babu wa dada yake wa kambo mwenye miaka 41. Mwanaume huyu kwa sasa yuko kizuizini na anashitakiwa kwa makosa ya ubakaji, wanasema maafisa wa Uruguay walipozungumza na Agence France-Presse.

Wanafamilia, madaktari, mashirika ya kijamii, na vyombo vya habari vimemshawishi msichana huyu kuitoa mimba hiyo. Wameishinikiza serikali kujaribu kumlazimisha kufanya hivyo, kwa mujibu wa jarida la Pangea Today. Majibu, hata hivyo, hayajawaridhisha:

“Hakuna hatari yoyote kwa maisha yake wala mtoto, kwa hiyo hatuwezi kumlazimisha kutoa ujauzito huo,” mkurugenzi wa INAU, Monica Silva, alisema.

Lugha za Pili Zinazoongozwa Kuzungumzwa Zaidi Afrika

Don Osborne anajadili habari iliyowekwa kwenye tovuti ya Chuo Kikuu cha Olivet Nazarene ikionesha ramani ya “Lugha za pili kuzungumzwa zaidi duniani.” Anaeleza matatizo makuu kutokana na habari hiyo:

Suala la kwanza ni kudhani kwamba “lugha inayozungumzwa zaidi kwenye nchi yoyote huwa wazi; mara nyingi, ni lugha ya taifa husika.” Barani Afrika hali ni tofauti, kama kusema “lugha inayozungumzwa zaidi” maana yake ni kuhesabu idadi ya wazungumzaji. Kwa mfano nchini Mali, ambapo hali ya lugha iliangaziwa kwenye blogu hii katika kutazama uzungumzaji wa lugha – Kibambara kinaonekana kuwa lugha maarufu kuliko hata lugha rasmi ya Kifaransa.

Lugha rasmi si kigezo kinachoaminika katika kupima umaarufu wa lugha barani Afrika, zaidi ya mukhtadha (muhimu) wa matumizi rasmi na umaarufu wake. Kwa mifano ya nchi hizo mbili, kuna masuala mawili yanajitokeza:

•Afrika Kusini inazo lugha 11 rasmi (tovuti ya Olivet imetaja Kizulu pekee kuwa lugha rasmi). Kwa hiyo moja wapo ya lugha rasmi inakuwa lugha ya pili kuzungumzwa. Pengine lugha hiyo inaweza kuwa ki-Xhosa kama inavyooneshwa, lakini mtazamo wa kutumia lugha rasmi kama kigezo hauonekani kufanya kazi katika mazingira haya.

•Rwanda ina lugha tatu rasmi (Kinyarwanda, Kifaransa, na Kiingereza), na Jamhuri ya Afrika ya kati inazo mbili (Ki-Sango na Kifaransa). Kwa sababu tovuti haijazingatia lugha hizi rasmi katika kujadili lugha za pili zinazozunguzwa zaidi, imejikuta ikidai kwamba Kiswahili ni lugha ya pili kuzungumzwa zaidi nchini Rwanda, na kwamba lugha za asili ndizo zinazotumika zaidi nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati – jambo ambalo halitoi taswira halisi.

Soma sehemu ya pili ya hoja zake hapa.

Tunayoyajua na Tusiyoyajua Baada ya Jaribio la Mapinduzi Nchini Burundi

Shangwe na vifijo karibu na ikulu ya Rais nchini Bujumbura baada ya kupinduliwa kwa Nkurunzisa.

Kufuatia nia ya kugombea urais kwa kipindi cha tatu ya Rais wa Burundi aliye madarakani Nkurunziza, Jenerali Godefroid Niyombare alitangaza kwamba utawala uliopo umeangushwa rasmi na kwamba anatwaa madaraka mpaka itakapotangazwa vinginevyo. Serikali ilikanusha mapinduzi hayo kutokea na iliyaita “upuuzi”. Hali bado inaonekana kuwatete nchini Burundi, lakini hapa ni mhutasri wa kile kinachofahamika na kile kisichoeleweka vyema jijini Bujumbura, mji mkuu wa Penelope Starr (kupitia blogu ya UN Dispatch):

Rais Nkurunziza haikuwa nchini wakati mapinduzi yakitangazwa (lakini hakuna anayejua ikiwa amerudi au bado) : Rais alikuwa akihudhuria Mkutano wa Wakuu wa Nchi za Afrika Mashariki wakati mapinduzi hayo yakitangazwa. Amejaribu kureje kwa ndege jijini Bujumbura lakini haijulikani kama alifanikiwa.

Huu si mgogoro (tu) wa kikabila :

Nkurunziza na Jenerali Niyombare wote walikuwa viongozi wa waasi wa Ki-Hutu. Zote wako kwenye serikali ya chama hicho hicho, na Niyombare alikuwa balozi wa Kenya na mkuu wa ujasusi, nafasi ambayo alinyang'anywa mwaka huu.

Kama ilivyokuwa kwa Burkina Faso mapema mwaka huu, maoni ya wananchi nchini Burundi yanaonekana kuunga mkono mapinduzi ya kijeshi kama namna moja ya kupinga watawala wa Kiafrika wanaotaka kutawala milele:  

Kiel kinacotokea leo Burundi ni mapaki ya kile kilichotokea mwishoni mwa mwaka jana nchini Burkina Faso, wakati mkuu wa nchi aliyetawala muda mrefu Blaise Compaore alipong'olewa madarakani na jeshi  baada ya kutangaza dhamira yake ya kugombea tena kipindi kingine cha utawala. Wakati hali nchini Burkina Faso bado haijatengemaa, hatua hiyo ilikuwa ya muhimu, kwa sababu wananchi waliunga mkono mapinduzi hayo, kwa sababu ya kuchoka utawala wa miongo kadhaa wa Compaore(..)lakini hali nchini Burundi ni tofauti kidogo, hususani kwa kurejea historia ya vita ya wenyewe kwa wenyewe nchini humo iliyokwisha mwaka 2005.

Je, Saudi Arabia Imelishambulia Bwawa la Kale la Marib Nchini Yemen?

Kuna taarifa zisizodhibitishwa zinazosema kwamba vikosi vya pamoja vya Kisaudi, ambavyo vimekuwa vikiishambulia Yemen kwa mabomu kwa zaidi ya miezi miwili sasa vimelilenga Bwawa la Marib, moja wapo ya maajabu makuu ya katika ulimwengu wa ubunifu wa kale wa kiufundi.

Kwenye mtandao wa Twita, Hussain Albukhaiti anadai:

Taarifa zisizothibitishwa: Ndege za kijeshi zimeshambulia bwawa la Mariba

Akijibu twiti hiyo, Albukhaiti anaweka picha za bwawa hilo linalokadiriwa kujengwa katika karne ya nane kabla ya Kristo na linasemekana kuwa bwawa la zamani zaidi duniani:

Uharibifu wa Bwawa la Mariba limejengwa karne ya nane (KK) na limelengwa na ndege za kijeshi za Kisaudi

Kiwango cha uharibifu wa miundo mbinu na historia ya Yemeni bado hakijajulikana. Tunaendelea kukusanya taarifa na vyanzo zaidi viko hapa kuhusu tukio hilo kwenye dawati la Global Voices Uthibitisho, mradi unaowezeshwa kwa ushirikiano na Meedan Checkdesk, zana ya mtandaoni ya uthibitisho wa habari, pamoja na Global Voices Online.

Unaweza kuacha maoni yako hapa kuchangia dondoo kuhusu habari hii au hata kuungana na timu yetu ya habari.

Uchaguzi wa FIFA Unaendelea

Pamoja na kutiwa nguvuni kwa maafisa kadhaa wa FIFA kufuatia mashitaka yaliyofunguliwa na Wizara ya Sheria ya Marekani, chombo hicho kinachosimamia kandanda duniani kimesema kwamba uchaguzi wake, ambao utaunda baraza la 65 la FIFA, utaendelea kama ulivyopangwa hivi leo. Rais wa FIFA aliye madarakani Sepp Blatter, ambaye ameongoza chombo hicho katika kipindi cha miongo miwili inayodaiwa kugubikwa na ufisadi, rushwa na fedha haramu, anatafuta kuchaguliwa kwa muhula wa tano kwenye baraza la leo. Blatter amegoma kujiuzulu pamoja na kuzungukwa na tuhuma, pamoja na mashinikizo yanayomtaka aachie ngazi.

Unaweza kufuatilia matangazo ya moja kwa moja ya uchaguzi wa FIFA hapa.

Je, Utoaji wa Mimba Unaweza Kujadiliwa Kwenye Treni za Medellín?

Wakazi wa jiji la Medellín, Colombia, wanajiuliza kama treni inaweza kuwa eneo la kuzungumzia masuala ya utoaji mimba, kutokana na tangazo la kampeni ya #ladecisiónestuya (uamuzi ni wako) inayoendeshwa kwa mifumo mbalimbali ndani ya vyombo vya usafiri wa umma, hasa magari, kama inavyosimuliwa na mtumiaji wa twita aitwaye Jaime Andrés (@JAIM3_ANDR3S):

Uamuzi ni Wako pic.twitter.com/Nbaq2zJHXn

— Jaime Andrés (@JAIM3_ANDR3S) May 26, 2015

Uamuzi ni Wako

Kampeni hiyo inaendeshwa na shirika lisilo na kiserikali linalotoa huduma za afya ya uzazi, ikiwa na ujumbe “kutolewa kwa mimba 3980,000 isiwe kosa la jinai.”

Kwa kutumia alama ishara ya #Abortonoesculturametro (Utoaji Mimba si Utamaduni wa Ndani ya Treni) kwa kurejea sheria mbalimbali zinazoongoza treni za Medellín zinazoitwa “Cultura Metro” (Utamaduni wa Metro), watu wamekuwa wakiadili maoni kuunga mkono au kupinga utoaji mimba, kwa namna ile ile kama mifumo ya sauti kwenye magari inavyotumika kila siku kutuma ujumbe na habari nyingine za picha.